Francis12
JF-Expert Member
- Sep 30, 2016
- 7,533
- 22,278
SIRI YA UCHAFU.!!
By Malisa GJ,
Kwa kuwa "mkuu wa wakuu" amekataa kuwapa semina elekezi wateule wake, mimi nitakua natoa vi-course vifupi vifupi vya Management ili kuwasaidia wateule wa mkuu, pamoja na watanzania wengine walioko kwenye nafasi za uongozi.
Kuna hadithi moja ya kiingereza kuhusu mambo ya management, inaeleza mambo yanayofanana na haya yanayoendelea nchini kwa sasa. Ngoja nikusimulie kwa tafsiri isiyo rasmi ya Kiswahili.
Ndege mmoja alikua anaruka kutoka maeneo ya Kaskazini kwenda Kusini huko nchi za Ulaya akikimbia baridi kali iliyokua Kaskazini. Katikati ya safari akazidiwa na baridi na hivyo kuanguka chini. Akakaribia kuganda kwa ajili ya baridi (freeze). Mara akapita ng'ombe jirani yake akamuangushia uchafu (kinyesi). Ule uchafu ukamfunika. Akahisi joto na mwili wake uliokua umepoa, ukaanza kuchemka tena.
Akafurahi na kuanza kuimba kwa shangwe. Wakati akiendelea kuimba kwa furaha, paka akasikia sauti yake. Yule paka akaanza kutembea kufuatilia ile sauti. Akafika na kukuta inatoka chini ya uchafu. Ndege amefunikwa na uchafu. Akatoa ule uchafu juu ya ndege, kisha akamkamata yule ndege, akamrarua na kumtafuna. Akawa kitoweo.!
[HASHTAG]#FunzoNo1[/HASHTAG]:
Si kila anayekurushia uchafu ni adui yako. Kuna uchafu mwingine ni wa kukusaidia. Ngo'ombe alimrushia ndege uchafu, na ule uchafu ukamsaidia asife kwa baridi.
[HASHTAG]#FunzoNo2[/HASHTAG]:
Si kila anayekuondoa kwenye uchafu ni rafiki yako. Wengine wanakuondoa kwenye uchafu ili wapate nafasi nzuri ya kukuangamiza. Paka alimuondoa ndege kwenye uchafu kisha akamrarua na kumtafuna.
[HASHTAG]#FunzoNo3[/HASHTAG]:
Unapokua katikati ya uchafu jifunze kukaa kimya. Acha kupiga kelele. Unapopiga kelele utawafanya watu waanze kukufuatilia na kugundua umefunikwa na uchafu. Watagundua kinachokupa kiburi cha kupiga kelele ni joto la uchafu uliokufunika. Watautoa huo uchafu na kukurarua na utaangamia.
Laiti ndege angetulia kimya kwenye ule uchafu asingeliwa na paka. Kwahiyo na wewe jifunze kukaa kimya kama upo kwenye uchafu. Kama umepata kazi kwa kubebwa kaa kimya, kama umepata utajiri kwa wizi tulia, kama umepata madaraka kwa kuhonga ngono funga mdomo. Ukipiga kelele utasababisha watu wakufuatilie na watagundua umefunikwa na uchafu. Watakutoa na kukuangamiza. Kelele za ndege zilimfanya paka amfuatilie akamuondoa kwenye uchafu kisha akamuangamiza. Na wewe ukiwa kwenye uchafu jifunze kukaa kimya ili usiangamizwe kama yule ndege.
Natumaini somo limeeleweka. Kwangu hakuna "Fafa" wote nimewapa 100%.
Malisa GJ (Mwalimu wa zamu).!