Mwenge wa UHURU hukimbizwa kila mwaka nchi nzima ukiwa na kauli mbiu mbalimbali, katika mbio hizo mwenge huzindua majengo mbalimbali ya umma kama vile Ofisi, Zahanati na Shule ambapo zaidi ya 95% ya majengo hayo yanakuwa yamejengwa chini ya kiwango. Utasikia ndugu mgeni rasmi ofisi hii imegharimu shilingi milioni 10 wakati ujenzi wake halisi umeghlimu shilingi milioni 2. Hamisi Kagasheki mkoani Kagera aliwahi kuamuru shule iliyofunguliwa na Mwenge ipigwe nyundo yote kabla haijatumika kisa ilikuwa na nyufa za kuweza kupitisha simu ya mkononi.Mwenge wa uhuru una gharama zifuatazo:a) Mafuta ya magari kuzunguka nchi nzima.b) Malipo kwa wanaoukimbiza nchi nzima.c) Magari ya kuzunguka nchi nzima na matengenezo yake ya mara kwa mara.d) Gharama za maandalizi ya kila mahali utakapolala nchi nzima.e) Gharama za walinzi mahali unapolala kila usiku nchi nzima.f) Muda wananchi wanaopoteza kuusubiri na kukesha nao n.kMaswali ninayohitaji wenzangu mnisaidie majibu yaje:a) Mbona kila mwaka mwenge unapozimwa hatujawahi kusomewa mapato ya mbio hizo?b) Tunapata faida gani kutokana na kuukimbiza mwenge kila mwaka?c) Hivi kweli viongozi wa mbio za mwenge wanapozindua majengo yanayotaka kubomoka hawaoni kuwa yako chini ya kiwango?WABUNGE WETU MWENGE HATUUTAKI,,,,,,,,,,,,,. HAUNA TIJA KWETU
..