Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,576
- 729,450
Lakini hapa ni zaidi ya hicho kinachotupeleka kwenye fikra za kawaida..kwenye maisha kuna siri nyingi
Siri za mafanikio
Siri za ndoa
Siri za watu wa kaliba fulani
Siri za serikali nk nk
Siri zote hizi zinaangukia kwenye hali moja tu kwamba kuna jinsi ya kufanya kitu fulani ili uweze kufanikiwa vile inavyotakiwa
Ni kawaida sana kusikia watu wakisema kwa dhihaka kwamba mchezo huu hautaki hasira...! Ni kweli kabisa kwakuwa hata mchezo wa kupigana ukitanguliza tu hasira unadundwa
Wahenga walisema hasira hasara...! Hakuna hata mmoja ambaye alitanguliza hasira kisha akafanikiwa
...! Watu wamepoteza maisha fedha na hata mali kwa sababu tu walitanguliza hasira jabza na kukosa subra, hawa hawakujua siri ya mchezo
Tuna members wenzetu humu wamepigwa ban kwasababu tu ya kuruhusu hasira itawale kuliko hekima, busara na tafakuri
Tunakutana na changamoto nyingi tu za kimaisha, tunakwazwa sana na kuna wakati kwa kiwango kisichovumilika...na kuamua kuchukua hatua za kulipa kisasi bila tafakuri ya kina
Kumbuka hekima ya mtu busara ya mwanadamu huonekana wakati wa shida kubwa wakati wakutatizwa na kukwazwa, wakati wa kuguswa hisia zetu za ndani kabisa kwa namna ya kuumiza sana...maamuzi yako ya busara kwenye kilele cha ghadhabu ndio kipimo cha hekima yako katika maisha..na hii ndio siri kuu ya mchezo