Siri ya majina ya ukoo

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
75,227
157,425
Majina ya ukoo ni majina tunayoyarithi kutoka kwa mababu na vizazi vilivyotangulia.

Majina ya ukoo ni yale ya asili ya Afrika mathalani Mbegale, Manyenye, Igembe nk.

Majina haya huwa yana maana fulani, hata kama huijui, lakini kwenye ulimwengu wa kiroho majina haya yana maana kubwa.

Majina haya yanatumika sana wakati wa matambiko na ibada za mizimu. Kwenye ibada za mizimu au matambiko hutatumia jina lako la John au Ally, utatumia jina lako la asili ili kukuunganisha wewe na mizimu ya kwenu.
Matambiko, ibada za wafu, ibada za mizimu ni ibada zilizo machukizo kwa mwenyezi Mungu.

Ukiwa na jina la ukoo ni rahisi sana kurogeka ndio maana leo watu wengi hawataki kutumia majina ya ukoo, utakuta mtu anaitwa Twaha Juma, ukimuuliza wewe ukoo wenu ni upi,? Atakujibu Khalfan .

Watu wanaficha majina yao ya ukoo na ya kijadi kwa ajili ya usalama.
Nakaribisha michango yenu.

CC:- mshana jr, jichawi, Tuyuku, MziziMkavu, FaizaFoxy
 
Bujibuji majina yetu ya ukoo yanakwenda mbali zaidi ya hapo yanabeba uasili utambulisho na mizizi ya ukoo
Makafara matambiko mila desturi na hata maagano ya hizi koo roho zake ziko kwenye majina ya kiasili ya ukoo husika
Halafu kuna kitu kinaitwa roho za familia. Hizi huleta magonjwa ya kurithi, tabia, na vitu kama hivyo. Roho hizi huhamisha laana na mateso kutoka kizazi kimoja kwenda kingine, ndio maana utakuta kuna baadhi ya koo hawaolewi, wakiolewa mume anakuga
 
Lakini pia kuna upande wa mema yake kwa mfano ukoo wa pesa au ukoo wa vipaji au ukoo wa elimu nk nk na mara nyingi hizi koo huwa hazitaki kuchanganya ili ID isipotee au wasiletewe contamination mbovu kwenye ukoo
1456120725876.jpg
 
Mtoa mada unaongea nini asee unasikia raha kuitwa Mohammed jina la asili ya waarabu au John ile hali ww ni mwafrika na hayo majina si asili yako? Tenda unaenda mbali na kuyaponda mimi natamani ningeandikishwa majina haya asilia ila ndo ivo but wanangu sitaakaa niwape majina haya ya Wageni
 
Bonesmen,?
 
Huku ni kutishana tu,kwani majina yote ya asili hayafai?,ukijua utamu wa jina lako hutatamani kuitwa jina la ughaibuni.Hizo roho zinasafiri kwny majina ya asili tu ama ndo unataka kutushawishi hao wakina joni wao hawakuwa na matambiko?
 
Hamna lolote. Mimi natumia majina yangu yote ya ukoo na sijawahi kurogeka,
Kwanza huwa najivunia mtu akiniita kwa jina la nyumbani, hayo mengine ni kasumba za wazungu kuupoteza utamaduni wa kiafrika
 
tatizo ni lugha tu.
majina yetu kama mabula ni mvua,
majina ya ughaibuni petro au peter ni jiwe au mwamba
hapo cha kujivunia majina ya ughaibuni ni kipi au kwa kuwa hatujui maana za majina yao?
 
Mtoa mada unaongea nini asee unasikia raha kuitwa Mohammed jina la asili ya waarabu au John ile hali ww ni mwafrika na hayo majina si asili yako? Tenda unaenda mbali na kuyaponda mimi natamani ningeandikishwa majina haya asilia ila ndo ivo but wanangu sitaakaa niwape majina haya ya Wageni
Watu wengine nadhani ndo wale uwezo wa kuelewa unaishia darasa la tatu.
 
Back
Top Bottom