wambeke
JF-Expert Member
- Aug 30, 2013
- 2,655
- 2,650
nabiii gani mwendawazimu huyo? pelekeni muone usije shangaa mmeo hasimamishikuna nabii anasema wamama wapeleke boxer za waume zao na wanaume wanapeleka bikini zikaombewe
nabiii gani mwendawazimu huyo? pelekeni muone usije shangaa mmeo hasimamishikuna nabii anasema wamama wapeleke boxer za waume zao na wanaume wanapeleka bikini zikaombewe
Wewe sio muumin acha uongome nilishaachaga kwenda kanisani kwenyewe maana ni ujinga mtupu, eti madhabahuni kasimama mwanamke, mwaka mzima mfululizo hapo ina maana kuna siku kasimama yupo hedhi, si upumbavu huo
wewe unasema kuwa muumini mimi nishasimama hadi mimbarini kuhubiria watuWewe sio muumin acha uongo
Duh! Hii hatari, yaani nichukue boxer ya mume wangu napelekea Jinaume jingine eti linabii au litume siwezi hata siku. Ila utashangaa kuna watu wanapeleka mpka chupi zao za ndani kuombewa.kuna nabii anasema wamama wapeleke boxer za waume zao na wanaume wanapeleka bikini zikaombewe
Hakuna neno pale, zaidi majisifu/majigambo na fix nyingitutanunua tu...haitupi shida mbona kwa waganga tunanunua zaidi ya hayo mafuta? ntanunua na wakinitapeli ni sawa pia ila kwa upande mwingine neno la mungu ntanufaika nalo wakat naendelea na hayo mafuta ya upako
Ushakamatwa wewe, pole sanaHujui biblia,kupaka mafuta ni sawa kabisa na sii mafuta pekee hata kitambaa chaweza kuombewa na akapelekewa mgonjwa akapona.kuwa mwangalifu na kazi za Mungu,kuna watumishi wa Mungu ukuwanenea vibaya waweza hukumiwa,tulia kimya mwache Mungu awahukumu kama unafikiri ni matapeli.
Hahahaha kakamatwa patamu kweli ndio maana povu likamtoka. Wameona biashara yao inafichuliwa.Ushakamatwa wewe, pole sana
Ukienda pale posta kuna duka kubwa tu wanauza mafuta ya upako. Kichupa kidogo kabisa laki na 20, kikubwa laki 2. Na watu wananunua sana. Wanasema yanatoka Israel. Watu wamekuwa matajiri sana kwa biashara hii sio siri.kuna hadi unga wa upako
Mkuu hii biashara ukianzisha kama huna gari, fasta unapata gari tena ya maana na nyumba za kutosha. Ni biashara moja tamu sana kikubwa ujue kucheza na akili za wajinga. Utawavuna wengi sana. Ukitaka kuamini nenda huko vijijini kama utayakuta hayo mafuta ya upako. Lakini mjini yapo ya kutosha maana ndiko penye pesa.Ukienda pale posta kuna duka kubwa tu wanauza mafuta ya upako. Kichupa kidogo kabisa laki na 20, kikubwa laki 2. Na watu wananunua sana. Wanasema yanatoka Israel. Watu wamekuwa matajiri sana kwa biashara hii sio siri.
Hii biashara nzuri sana, unatumia matatizo ya watu kupata pesa balaa.
View attachment 379008
Hawa ni kama nabii wa uganda KIBWETELE......,aliwachoma moto wengi sana kwe kanisa lake kwa imani aliyowapandikiza yeye mwenyewe.....TUWE MAKINI JAMANI WATANZANIA.Wajinga ndo waliwao wameshamezeshwa sumu na manabii wao fake basi kwao kila kitu ni ndio tu
Pole sana madam, umeweka mpaka jina...,safi iyo nimeipenda..mana ukweli utakuweka huru siku zote.Mtumishi umenena vyema sana, kweli tunaangamia kwa kukosa maarifa. Hawa manabii wanapitia katika ujinga wetu kupata utajiri wa ajabu. Mimi niliwa kwenda kununua hayo mafuta pale Miracle center kwa Mtume Peter Nyaga, nilinunua kichupa kidogo laki moja(100000). Nilipokunywa Yale mafuta, nilikuwa na mimba ya miezi 3 ikatoka. Niliugua sana sikujua kwa nini ilitokea kwangu. Tokea kipindi hicho mume wangu alinizuia kabisa kukanyaga katika makanisa hayo.
kweli kabisa, sisi tunasema , imekula kwake.......a take careHahahaha kakamatwa patamu kweli ndio maana povu likamtoka. Wameona biashara yao inafichuliwa.
Teh teh teh ,janja ya nyani iyo....., watu waamke kwa kweli..........ila wengi wao ni wamama.......,wanapenda miujiza sanaUkienda pale posta kuna duka kubwa tu wanauza mafuta ya upako. Kichupa kidogo kabisa laki na 20, kikubwa laki 2. Na watu wananunua sana. Wanasema yanatoka Israel. Watu wamekuwa matajiri sana kwa biashara hii sio siri.
Hii biashara nzuri sana, unatumia matatizo ya watu kupata pesa balaa.
View attachment 379008
Asee wamama wamekuwa wahanga sana, hata mi najiran yangu alishaw kwenda kuchukua mafuta ya upako umwekee mumewe kwenye chakula asitoke nje ya ndoa. Yaan mambo ya waganga wa kienyeji yameamia kanisani.Teh teh teh ,janja ya nyani iyo....., watu waamke kwa kweli..........ila wengi wao ni wamama.......,wanapenda miujiza sana
hata kwa waganga miujiza ipo.
usijidanganye Mungu hadhihakiwitutanunua tu...haitupi shida mbona kwa waganga tunanunua zaidi ya hayo mafuta? ntanunua na wakinitapeli ni sawa pia ila kwa upande mwingine neno la mungu ntanufaika nalo wakat naendelea na hayo mafuta ya upako
Waumini walishageuzwa madondocha ukiwagusa manabii wao, mapovu yatawatoka kweli. Ngoja waendelee kutapeliwa maana hakuna namna.Hawa ni kama nabii wa uganda KIBWETELE......,aliwachoma moto wengi sana kwe kanisa lake kwa imani aliyowapandikiza yeye mwenyewe.....TUWE MAKINI JAMANI WATANZANIA.
Hivi watu kama nyie tuwaweke kwenye kundi gani? Unaropoka ujinga tu, sasa umeandika nini hapo kichwa maji wew. Toa hoja inayoeleweka kutushawishi kuendelea kununua hayo mafuta au maji ya upako. Sasa unakurupuku dishi limeyumba so what. Elimu, Elimu, Elimu.We ndo akili huna wanzako wapo mirembe we unaendelea kutusumbua tu, nmekufatilia kwamakin nmegundua dishi limeyumba ngoja tukusamehe bure
Hahahaaa usikute ni msomi huyo, alafu mawazo anayotoa utazani unajifunza kuongea. Ndalichoka ana kazi ngumu, kuelimisha wajinga kama hawa kazi hipo.Hivi watu kama nyie tuwaweke kwenye kundi gani? Unaropoka ujinga tu, sasa umeandika nini hapo kichwa maji wew. Toa hoja inayoeleweka kutushawishi kuendelea kununua hayo mafuta au maji ya upako. Sasa unakurupuku dishi limeyumba so what. Elimu, Elimu, Elimu.
Mkuu umesema ukweli kabisa bila kuficha chochote ubarikiweShetani ametupofusha na kutufanya tusione wala kusikia, ametuteka nyara na kutupumbaza kiasi kwamba tumeshindwa kuutambua ukweli. Ni nani asiyejua shetani ndiye mshitaki wetu? Ana orodha ya dhambi ya kila mwenye dhambi; Hutoa hati yake ya makosa mbele Mungu wetu. Ndiye adui yetu mkubwa, malaika mkuu aliyeanguka ambaye amejaa chuki, fitina, dhuluma, ukatili, husuda, Utapeli, uongo, tamaa, udanganyifu, unafiki, ushirikina, mateso, magonjwa n.k
Shetani ni mtawala wa roho katika ufalme wa giza, hivyo adui wetu ni wa rohoni, basi ni lazima tutumie silaha kuu za roho dhidi yake. Baada ya Yesu kutabiri juu ya kifo chake kule Yerusalemu, Simoni Petro akasema " Hasha, Bwana , hayo hayatakupata" Yesu akamjibu Petro " Nenda nyuma yangu, Shetani; ukikwazo kwangu, maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu" (Mathayo 16: 21-23). Bwana Yesu hamkemei Petro bali anakemea nguvu za pepo zilizoko nyuma ya maneno ya Petro. Shetani alizungumza kupitia kwa mawazo na sauti ya Petro.
Leo shetani anazungumza kupitia kwa mawazo na sauti ya watu waliojipachika majina makubwa, wanaojiita "mitume na manabii" Baadhi yao wamegeuka kuwa wafanyabiashara wa mafuta ya upako, maji, chumvi na vitambaa. Naomba nizungumzee juu ya siri ya mafuta ya upako ambayo wamekuwa wakiyauza kwa gharama kubwa sana.
"Upako" ni neno la Kiebrania katika Agano la kale yaani " Masah" lenye maana Kuwekea mafuta kwa kumimina, kupaka au kutia kwa kusukuma na kueneza kwenye kitu au mtu mwenye kupakwa. Mazoea ya kupaka mafuta yalikuwepo katika makabila mengi ya mashariki ya kati ya awali. Mazoea haya yalikuwa na matumizi ya kawaida na pia matakatifu. Kwa mfano kumpaka mgeni mafuta kama tendo la ukarimu, Kulifanyika hata kwa Yesu (taz. Yohana 12:3, Luka 7:46 , Zaburi 23: 5). Mazoea haya ya kupaka mafuta yalikuwa na maana kubwa sana kwa watu wa Israeli, katika Agano la kale. Tukisoma habari ya Yakobo alipoweka kumbukumbuku ya kukutana kwake na Mungu mara ya kwanza. Yakobo alimimina mafuta juu ya jiwe alilokuwa amekalia, kichwa chake akilala na kuota ndoto (Mwanzo 28 : 10-18). Baadaye mafuta yalipakwa kwenye madhabahu na vitu vingine vilivyotumiwa katika ibada. ( Kutoka 30:26-29, Walawi 8:10-11). Mazoea ya kutia mafuta yalipanuliwa kwa wafalme mpaka kwa manabii (1 Samweli 9:16). Kwa upande wa Agano jipya, kila neno lilidhihirisha namna tofauti ya upako. Kwa mfano "Aleipho" hili ni neno la kiyunani lenye maana ya kupaka na kusugua mafuta mwilini (Marko 6:13, Luka 7:38-46). Upako haukuhusu uponyaji wa ugonjwa, ila upako huu ulikuwa ishara ya uwepo wa Roho mtakatifu na kumweka wakfu mtu aliyekuwa mgonjwa ili amuombe Mungu uponyaji katika imani.
Nazungumza na hawa matapeli waliogeuza maandiko kwa upofu wao kwa sababu ya tamaaa ya mali, umaarufu na Pesa, kugeuza kanisa kuwa duka la biashara ya mafuta ya upako. I have seen on television and heard on radio fake prophet selling oil and water; These are false things, miracles are free. Many people are following this trend because of lack of knowledge; Jesus Christ never sold oil, where in the Bible do we see people selling oil? There is no power in those oil and water no matter where they come from whether from Israel or Jordan.
View attachment 378647
Ndugu zangu hawa watu hawatofutiana na waganga wa kienyeji. Je wajua hayo mafuta yao ya upako yanatokana na nini? Mafuta haya yanatokana na mchanganyiko wa Mafuta ya "Mzeituni" Mafuta ya "Vituguu swaum" mafuta ya "Nguruwe" pamoja na mafuta ya "Alizeti". Hakuna ubishi mafuta haya wanatumia hata waganga wa kienyeji, kuondoa mikosi, kuzuia wachawi kuingia ndani kwa kunyunyuzia pande nne za nyumba, kufukuza majini ndani ya mwili, kupaka mwilini kuondoa maumivu na magonjwa mengine.
View attachment 378648
Hatuwezi kuruhusu shetani kutuchezea kiasi hiki. Nabii au mtume Yeyote anayeuza mafuta haya ni tapeli; inabidi tumkemee. Haijalisha ni nani, wauza mafuta mnawajua. Wengine wamefungua maduka makubwa ndani na nje ya nchi. Majina yao yanajulikana na yako wazi. Ni wakati wa kuwafunua hawa matapeli, wanafiki, wafitini, waongo, wapiga ramli, waganga wa kienyeji, wauwaji wa roho na wenye tamaa ya Mali, vyeo na pesa. Na sasa wameukwaa utajiri wa ajabu kwa biashara isiyolipiwa hata kodi.
Tunatakiwa kusimama imara dhidi ya mbinu za shetani. Ni wakati wa kumkabiri adui. Na silaha yetu kubwa ni maombi, maombi ndio njia ya pekee katika pambano la kiroho. Mwana wa Mungu aliyejazwa roho, anapoanza kuomba kwa dhati, Shetani hutetemeka. Shetani hawezi kushinda katika silaha ya maombi. Elewa kuwa maombi ni vita, kuomba ni zaidi ya pambano, ni jambo zito. Maombi ni mwito wa kujiami, kupitia kwa maombi tunagusa mbigu, ni ushindi dhidi ya magonjwa, laana, mikosi na umasikini(Waebrania 13:14). Shetani anajua nguvu iliyo katika maombi ndio maana anapinga vikali maisha yako ya maombi. (Waefeso 6:10-12).