Siri ya mafanikio

Siri ya mafanikio

Galacha Maestro

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Posts
1,353
Reaction score
2,231
Leo tuzungumze kidogo juu ya maombi. Je huwa unaomba? maombi yako yanajibiwa? Kama hayajibiwi umeacha kuomba? Kama unaendelea kuomba umetafuta kwanza kujua sababu za kutojibiwa maombi yako au unaomba tu kutimiza wajibu?
Kwa wewe ambaye huna utaratibu wa kuomba anza kuomba sasa maana maombi ndiyo njia kuu ambayo Mungu huitumia kuzungumza na wanadamu. Usipoomba usitegemee muujiza mwingine wowote wa kubadilika kutoka hapo ulipo.
Usi-assume Mungu anajua matatizo yako so atakusaidia tu bila kuomba. Jifunze kuomba.
Wakati fulani Yesu aliwahi kutembea juu ya maji; Petro nae akaingia kwenye maji kumfuata.. Kutokana na imani haba Petro akaanza kuzama.. Lakini alipoona anazama akapaza sauti "Eeh Yesu niokoe". Yesu akamshika mkono na kumuokoa.
Unajifunza nini hapa? Tunajifunza kuwa Petro asingeomba msaada angezama. Kwa lugha rahisi ni kuwa Petro ange-assume kuwa Yesu anamuona hivyo definately angemsaidia, basi Petro angekufa maji na Yesu angemuacha afe, Kwa sababu hakuna msaada unaotolewa bila kuombwa. Lakini alipoomba msaada Yesu alimsaidia mara moja.
Therefore kuna nguvu kubwa ktk maombi. Usipoomba usitegemee muujiza wa kupata suluhisho la matatizo yako. Usi-assume kuwa Mungu anajua, omba, mwambie nae atatimiza haja ya moyo wako.
Pili, kuna wenzetu wanaomba lakini maombi yao hayajibiwi.. Umewahi kujiuliza kwanini? Zipo sababu nyingi za kutojibiwa maombi lakini leo nitakufundisha moja; nayo ni MAHUSIANO yako na Mungu.
Wewe na Mungu mna mahusiano gani? Unaposogea mbele za Mungu na kuomba unaenda kama nani? Wanadamu wana namna mbili za kumtizama Mungu. Mosi ni Mungu kama baba (mzazi), pili Mungu kama baba (mlezi). Sasa wewe unaenda kwa Mungu kama mzazi wako au kama mlezi wako?
Katika utaratibu wa kawaida wa kibinadamu ikiwa una watoto wawili; mmoja unamlelea na mmoja wa kumzaa then wote wakakuomba msaada utampa kipaumbele yupi? Bila shaka ni yule wa kumzaa.
Mtoto wa kumzaa anapoomba mahitaji yake kama karo ya shule anadai, na ni lazima mzazi atimize. Lakini mtoto wa kumlelea anapoomba mahitaji yake anategemea 'rehema' ya mlezi wake.. Kama mlezi hana basi, mtoto hawezi kudai.
Sasa na Mungu wetu yupo vivyo hivyo. Unapoenda mbele zake ukiwa mwenye dhambi unaenda kwa Mungu kama baba yako mlezi, lakini unapokwenda ukiwa umetakasika unakwenda kwa baba yako mzazi.
Hivyo katika kujibu maombi, Mungu hujibu maombi ya watoto wake kwanza (waliotakasika) kabla ya kujibu maombi ya wale anaowalelea (wenye dhambi).
Kwa hiyo Inawezekana unasumbuliwa na magonjwa kwa muda mrefu na umeomba sana lakini huponi. Inawezekana umehitimu masomo yako na hujapata ajira wala hujaweza kujiajiri na umeomba sana lakini huoni tumaini.
Jitathimini upya juu ya maombi yako. Unaendaje mbele za Mungu? Unaenda kwa Mungu kama baba mlezi au kama baba mzazi.? Je una tabia ya kutubu kabla hujaanza maombi?
Ukitubu kwanza ndio ukaanza kuomba unajibiwa haraka kwa sababu wewe ni mtoto wa kuzaliwa na maombi yako yanapewa kipaumbele.
Ukianza kuomba tu bila kutubu kwanza maombi yako yanaweza yasifike (maana maombi ya wasio haki ni kelele machoni pa Mungu), au yakifika yasijibiwe au yakijibiwa basi kwa kuchelewa simply bcoz wewe ni mtoto wa kulelewa tu wa Mungu si wa kuzaliwa.
Ukijua siri hii utakuwa huna hofu ya maombi yako kujibiwa. Mwenye masikio na asikie.
 
Asante sana mtumishi wa Mungu. Nimejifunza kitu hakika, ngoja sasa nianze kukifanyia kazi kuanzia sasa. [emoji120][emoji120][emoji120]
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom