Siri ya mafanikio yako ipo chumbani kwako

Siri ya mafanikio yako ipo chumbani kwako

lui03152

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2020
Posts
273
Reaction score
385
Binafsi imani yangu ipo hivi. Siri ya mafanikio yetu ni chumba chetu. Dari linasema anga ndicho kipimo cha kufikiria; Dirisha linasema utazame nje uone fursa zilizopo ulimwenguni; Feni inasema uwe mtulivu usikurupuke kufanya lolote; Kalenda inasema uwe mtu anayekwenda na wakati; Kioo kinasema ujitazame na ujiamini kabla ya kutenda lolote.

Kitabu cha dini kinasema unapaswa kumwamini Mungu ili uishi; Kitanda kinasema ujifunze kuwa na likizo; Mlango unasema usipitwe na fursa ya aina yoyote ile hapa duniani; Saa inasema kila sekunde ina thamani sana katika maisha yako hivyo tumia muda wako vizuri.

Amka uishi
 
Amka uende kibaruani acha kuhusisha mambo ya ajabuajabu na mafanikio mkuu
 
Chumba changu hakina kalenda, hakina saa na hakina kioo na hakina feni kina kiyoyozi
 
Kwa hiyo wasiomwamini Mungua hawaishi??
Maisha sio hapa duniani tu, kuna maisha baada ya haya ya kidunia ambayo ili uyaishi yakupasa kumuamini na kumtii Mungu. Otherwise haiwezekani ndugu.
 
Kwa hiyo wasiomwamini Mungua hawaishi??
Hamna asiyemwamin MUNGU
Tofauti Ni Kila mtu anamwamin mungu wake
Mkurugenzi ,mungu Yesu, mungu Kaka yako tajirj, mungu mkuu wako kazini, mungu mizimu ya kwenu
Kila mtu ana anachokiona msaada zaidi ktk maisha ambacho ndio MUNGU wake
 
Hamna asiyemwamin MUNGU
Tofauti Ni Kila mtu anamwamin mungu wake
Mkurugenzi ,mungu Yesu, mungu Kaka yako tajirj, mungu mkuu wako kazini, mungu mizimu ya kwenu
Kila mtu ana anachokiona msaada zaidi ktk maisha ambacho ndio MUNGU wake
Dunia ni Mungu ni mmoja, hao wengine wakwako mkuu!...
 
Back
Top Bottom