Siri ya kufukuzwa Wanachuo nje | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siri ya kufukuzwa Wanachuo nje

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by USTAADHI, Dec 18, 2011.

 1. USTAADHI

  USTAADHI JF-Expert Member

  #1
  Dec 18, 2011
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 1,518
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Siri ya kufukuzwa Wanachuo nje

  *Chadema yaibua nyaraka za CCM, yasema inahusika

  *Heche adai ni hasira za Kikwete kuzomewa Mlimani

  Na. Waandishi Wetu
  SIKU chache baada ya kufukuzwa kwa takribani wanafunzi 100 wa vyuo vikuu nchini, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA), John Heche, amesema kufukuzwa kwa wanafunzi hao ni utekelezaji wa maazimio ya vikao vya juu vya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambavyo viliitaka Serikali ianze kuwachukulia hatua wanafunzi wote wanaokuwa mstari wa mbele kupinga mapungufu ya kielimu vyuoni.

  Kiongozi huyo amewataka viongozi wa dini, vijana, asasi zisizo za kiserikali, wasomi na Watanzania wote bila kujali itikadi zao, kuungana na kupinga kwa pamoja uonevu na ukatili unaofanywa na Serikali ya CCM dhidi ya vijana wanaotafuta elimu, lakini wanafukuzwa kwa makusudi kwasababu tu ya kulinda maslahi ya chama hicho.

  Heche alitoa kauli hiyo jijini Dar Es Salaam jana kupitia mkutano wake na waandishi wa habari ambao aliutumia kueleza kile alichokiita "ushahidi wa jinsi CCM ilivyoagiza kufukuzwa kwa wanafunzi wanaodai haki zao za kielimu". Alisema kati ya mwezi Julai na Desemba mwaka huu, jumla ya wanafunzi 100 kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dodoma na Chuo Kikuu cha Muhimbili, wamefukuzwa masomoni kwa sababu ya kuhisiwa kufanya siasa dhidi ya CCM, wakati walichokuwa wakidai ni kupatiwa mikopo ya elimu na fedha za kugharamia mafunzo ya vitendo, madai ambayo alisema ni ya msingi na halali.

  Mwenyekiti huyo wa vijana wa Chadema alisema kufukuzwa kwa wanafunzi hao pia kumetokana na Rais Jakaya Kikwete kuzomewa na kupokewa kwa mabango yenye madai mbalimbali alipotembelea chuo kikuu cha Dar es Salaam hivi karibuni wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya chuo hicho.

  Katika kuthibitisha hayo, mwanasiasa huyo alionyesha kabrasha kubwa lenye nyaraka za vikao vilivyopita vya halmashauri kuu ya CCM (NEC) na kuwasomea waandishi wa habari baadhi ya mapendekezo ya siri ambayo Idara ya Oganizesheni ya CCM inadaiwa kuitaka Serikali iyatekeleze, mojawapo likiwa ni kutaka kufukuzwa kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu wanaoonekana kuwa mstari wa mbele katika kudai haki au kufanya kile kinachodaiwa kuwa ni "siasa vyuoni".

  "Kufukuzwa kwa wanafunzi hawa ni utekelezaji wa maazimio ya vikao vya CCM vilivyofanyika na haswa vile vya Halmashauri Kuu yao (NEC) ambavyo vimetoa maelekezo mbalimbali kwa Serikali juu ya kuwachukulia hatua wanafunzi wa vyuo vikuu ambao wamekuwa wakiikosoa serikali waziwazi", alisema Heche na kuongeza"Na hata wahadhiri ambao wamekuwa wakitumia taaluma zao kwa uwazi na kusema juu ya mapungufu ya serikali, CCM iliagiza wachukuliwe hatua ya ama kufukuzwa kazi na au ajira zao kusitishwa.

  Hivyo kilichotokea Mlimani, Muhimbili na kule Dodoma , ni muendelezo tu wa utekelezaji wa maamuzi hayo ya kikatili yanayojali zaidi maslahi ya chama chao kuliko elimu na maisha ya vijana wa kitanzania"Alisema kwasababu ya shinikizo hilo la CCM ndio maana wanafunzi wote hao walifukuzwa vyuoni bila hata kupewa haki ya kusikilizwa, kwasababu tu ya kuhisiwa ni wanachadema huku wale wanaojulikana kuwa ni makada wa CCM wakiachwa.

  Heche alinukuu sehemu ya kabrasha linalodaiwa kuwa ni la kikao cha NEC ya CCM kilichoketi Dodoma , mwezi Novemba mwaka huu, ambayo inasomeka kama ifuatavyo: "Vyama vya upinzani hasa Chadema vimeendelea kutumia vijana wa vyuo vikuu na mazingira ya vurugu za vyuo vikuu kuchochea chuki dhidi ya viongozi wa serikali ya CCM na viongozi wake.

  Kilele cha vurugu hizi ni kundi la vijana walioingilia kati hotuba ya rais na mwenyekiti wa CCM alipotembelea Chuo Kikuu cha Dare Es Salaam kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya chuo hicho", kisha alisema:"Kwa hiyo, wanafukuza wanafunzi hovyo hovyo kwasababu tu ya hisia na hasira za mwenyekiti wao Kikwete kuzomewa, kama hawataki kuzomewa basi serikali ihakikishe inaboresha mazingira ya elimu na sio kufukuza wanafunzi wenye malalamiko ya msingi"

  Alisema matatizo ya migogoro na migomo isiyokwisha vyuoni hayajaanza leo na wala hayasababishwi na Chadema, bali Serikali yenyewe, kwani imekuwa ikiwadharau wanafunzi na kuacha kutimiza mahitaji yao.

  Akitoa mfano alisema Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa alichochea mwenyewe mgogoro Juni 22 mwaka huu pale alipoandika dokezo kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo akitoa maelekezo ya kutaka bodi ya mikopo isimamishe kutoa mikopo ya mafunzo ya vitendo kwa wanafunzi hadi hapo uongozi wa UDOM utakapoamua nani alipwe na nani asilipwe.

  "Tunaitaka Serikali na menejimenti za vyuo vikuu nchini ziwarudishe wanafunzi wote hawa vyuoni, vinginevyo hatutachelewa kuwaongoza Watanzania kudai vijana wao wapewe haki ya elimu… tusije kulaumiwa", alisema Heche.

  Katika hatua nyingine, BAVICHA wamelaani kitendo cha Jeshi la polisi kumkamata Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima, Absalom Kibanda na mwanasafu ya gazeti hilo , "Kalamu ya Mwigamba", Samson Mwigamba, kwa tuhuma ya kuchapisha makala inayodaiwa kuwa ya uchochezi, wakisema kuwa hatua hiyo inalenga kuwanyamazisha wanahabari wasifichue maovu ili mafisadi waendelee kutafuna nchi.

  "Tunatoa pole kwa jamii ya wanahabari wote nchini kwa unyanyasaji huu wanaofanyiwa na serikali ya CCM, tunasema haki haina itikadi…tushirikiane kukomesha uovu huu kwa nguvu ya umma. Dunia imewahi kuwa na watu wengi katili lakini mwisho wa yote walishindwa na hawa pia tutahakikisha wanashindwa", alisema.

  MWISHO
  source Tanzania Daima
   
 2. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #2
  Dec 18, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Aksante xana
   
 3. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #3
  Dec 18, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,422
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  sioni kile kibatani ningekugongea thanksi!
   
 4. Bei Mbaya

  Bei Mbaya JF-Expert Member

  #4
  Dec 18, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,265
  Likes Received: 226
  Trophy Points: 160
  Mzee wa visasi

  bado kwa EL alivyomuumbua kwamba anaijua richMOND
   
 5. Idimulwa

  Idimulwa JF-Expert Member

  #5
  Dec 18, 2011
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 3,384
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Haohao waliofukuzwa chuoni ndiyo watakaoiondoa ccm madarakani.
   
 6. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #6
  Dec 18, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  huu ni uchochezi wa wazi usio na maana.kule udom mliwahamasisha ma dent wakafanya fujo siku ya mwisho mkazima simu mlipoona maji yamefika shingoni.hakuna jamii inayoweza kuishi bila sheria kufuatwa,kabla ya kumlaumu mtu yeyote tuangalie kwanza makosa ya wanafunzi,tusikurupuke na matamko yasiyo na kichwa hapa.huyo heche hana jipya atumie muda huu kukijenga chama badala ya kuhadaa wananchi kwenye vyombo vya habari.
   
 7. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #7
  Dec 18, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  hivi kwa nini wale madiwani arusha walifukuzwa uanachama?nidhamu kwanza wazee.
   
 8. W

  Wakurogwa JF-Expert Member

  #8
  Dec 18, 2011
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 216
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sasa anawasaidiaje hao waliofukuzwa? maana pale Udom mpaka sasa zaidi ya madent 400 hawajarudi chuo tangu june na hii ilitokana na wao kuwajaza ujinga.Kukaa mbele ya vyombo vya habari na kusema haoitoshi.Muungwana ni vitendo bana!!
   
 9. MKWECHE

  MKWECHE JF-Expert Member

  #9
  Dec 18, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 299
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kufukuza wanafunzi sio Jawabu!Cha msingi ni Kusikiliza Kilio Chao na Kuwatatulia Kero zao wasome kwa Raha!
   
 10. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #10
  Dec 18, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Sheria ipo kwa ajiri ya walalahoi na upinzani?Swala la Magamba,Jairo na ufisadi kibao kwanini sheria isichukue mkondo wake kwa hao mafisadi waliojaa katika serikali na chama tawala au CCM ni chanjo au ngao ya UFISADI MUNGU IBARIKI TANZANIA.
   
 11. remon

  remon JF-Expert Member

  #11
  Dec 18, 2011
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 295
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  serikali iliyopo madarakani ni ya kishenzi , kizalimu , inayoendeshwa kibabe , ni serikali ya visasi tena inayongozwa na wapumbavu!!!!. ila kila kitu kinamwisho. ahsanteni!!!!!!
   
 12. kaburungu

  kaburungu JF-Expert Member

  #12
  Dec 18, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,608
  Likes Received: 2,461
  Trophy Points: 280
  Hivi kwani wanafunzi huwa wasoma kwa raha! Heri yao..
   
 13. t

  tisa desemba JF-Expert Member

  #13
  Dec 18, 2011
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 439
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  wale wanaharakati wa haki za binadamu na utawala bora ni wakati wenu kuwasimamia hawa vijana ili wapata haki yao kwa mujibu wa sheria.
   
 14. Scolari

  Scolari JF-Expert Member

  #14
  Dec 18, 2011
  Joined: Aug 4, 2008
  Messages: 273
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Watu wengine bana. Kama vipunguani flani hivi. Alikuambia nani CDM haijajengeka pimbi wewe ?
   
 15. m

  mark11 Member

  #15
  Dec 18, 2011
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wewe sijui akili umepeleka wapi au umekurupuka!

  ngoja nikupe hii

  Chuo cha St Joseph wanafunzi hawajapewa pesa ya kujikimu kwa muda wa wiki 5 sasa bila maelezo yanayoeleweka. Unajua wanaishije?
  1. Mabinti wanajiuza/kujirahisi wapate hela ya matumizi
  2. Wamefukuzwa hostel kwa kushindwa kulipa
  3. Wapo wanaopitisha siku bila kula
  etc
  na kesho wamepanga kugoma kuingia darasani na kuandamana. Unadhani hapo nani hana nidhamu kati ya serikali na wanafunzi?
  ungejisikiaje kusikia dada yako / mwanao wa kike anajiuza/ kujirahisi Dsm ili apate hela ya matumizi?
  AMKA ACHA UJINGA, UNADHANI NANI ANAPENDA FUJO?!
   
 16. d

  dada jane JF-Expert Member

  #16
  Dec 18, 2011
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kama uko fair, uchunguzi ufanyike kwa wanafunzi makosa yao na serkali nayo ichunguzwe makosa yake. Usilete hoja tete kama jina lako.
   
 17. k

  katatuu JF-Expert Member

  #17
  Dec 18, 2011
  Joined: Nov 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 45
  Acha kuropoka wewe.ndio maana hata hao wanafunzi mnawajaza ujimga badala ya kusoma wanawasikiliza watu kama nyie.hata angekuwa mwanangulazima afuate kilichompeleka siasa ataikutapindi atakapomaliza shule.cdm acheni wanafunzi wasome siasa chuoni sio mahala pake
   
 18. M

  MCHUMIA NCHI Member

  #18
  Dec 18, 2011
  Joined: Nov 22, 2011
  Messages: 96
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Atasoma na njaa?Atasoma ikiwa hana pa kulala??Hivi watu wengine hua mnafikia kwa kutumia MASABURI au?Nina hasira sana na watu kama nyie!
   
 19. LOOOK

  LOOOK JF-Expert Member

  #19
  Dec 18, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 3,392
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  hulijui ulisemalo mkubwa ongea kama mtu uliekamilika kiakili na kimawazo , rudi shuleni kwanza inaoneka hako kaelimu hakajakutoa gizani bado au uliunga unga vyeti{{{{{ ZZZZZZZZzzzzzzzzzzzzz}}}}}
   
 20. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #20
  Dec 18, 2011
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  JK ataishia kuwaonea dagaa tu .Amguse EL auone moto
   
Loading...