Siri ya kudai serikali tatu yagundulika

Siri ya kudai serikali tatu yagundulika

Nimegundua kumbe kuna agenda ya siri kwa watu fulani wa makundi fulani walioko na nafasi fulani kisiasa kwa vyama tofauti kutaka serikali tatu ili vyeo viwe vingi , vyeo kibao , serikali kibao ofisi kibao , semina kibao, safari kibao , posho kibao , sadakalawe amina, mwenye kupata apate mwenye kukosa akose! kumbe madaraka matamu jamani hata wale waliopita nao wanayataka.

Zikiwa serikali tatu, uongo hata kama ulistaafu miaka hamsini iliyopita ila kwa CV yako uongo hukosi nawewe japo Naibu Waziri.

Ila serikali zote kama kawaida zitaendeshwa kwa kodi zetu na majasho yetu.

Mwenye masikio na asikie.

Ni mtazamo tu wa mimi kijana nisietaka kusikia mawazo ya wazee na sina chama wala itikadi wala manifesto.

Mwenye busara huongea inapobidi, mjinga huongea ili mradi!
 
Ujinga mwingine bwn, hilo la serikali 3 lingekua linaombwa na wana ccm ningeelewa point yako cause wao ndio wanayo hiyo fulsa ya kupeana vyeo, si ndio chama kilichopo madarakani bwna? Sasa ccm hawtaki hata kusikia hiyo kitu, hayo madai na eti kuwaonea huruma watanzania masikini linatoka wapi, wakati nikiwa shule ya msingi kulikua na mikoa 25 tu Tanzania nzima, yaani Tanzania bara 20 na 5 kule visiwani, leo kila wilaya inataka kua mkoa, huruma kwa wananchi hapo iko wapi? Wilaya Fulani/sasa ni mkoa, wenye maduka wanatakiwa kuanza kulipia matangazo waliyabandika kwenye madirisha, milango, kuta za maduka yao, hivi huko sio kuwaongezea gharama za uendeshaji wafanya biashara!? Maneno kama M-Pesa, tiGo Pesa na Airtel moneye inapatikana hapa, kwasasa huo mkoa/wilaya yana chajiwa KODI! Halafu eti mwana ccm 1 anakuja kutudanganya eti serikali 3 zitaongeza kodi kwa mwananchi, kweli!? Tokea lini nyinyi mmewahi kua na huruma kwa Mtanzania!?
 
Mkuu uko sahihi.Kwa miaka 50 tiliyokaa pamoja ungetarajia tume ya warioba ipendekeze serikali moja ili tujue mbishi hasa ni nani kati ya CCM na hao UKAWA.hAPO NDIPO MBIVU NA MBICHI ZINGEELEWEKA.Lakini tume warioba ikaona ibebe wanasiasa badala ya wananchi walipa kodi ambao ndio wanakamuliwa kugharimia serikali ya zanzibar,tanzania bara na muungano.Tume ya warioba ilichofanya ni kuchonganisha vyama na kuviacha vitwangane ulingoni na kuacha wananchi wasijue ni nini.Katika tume zote ya Warioba HOVYO

East African Eagle
sijui leo umeamkia upande gani, maana unatema vitu vya akili kweli kweli..analysis yako hapo juu ni EXCELLENT, inawavua nguo wanasiasa wachumia tumbo wa Tanzania. If you want any progress katika muungano, Tume ilipaswa either ije na rasimu ya serikali MOJA, au basi tupa MUUNGANO kule..!! Sio kuzidi ku-complicate na kutuchangaya kwa kuongeza serikali ya tatu.
Nje ya serikali 1 au kuvunja Muungano, ni ku-service matumbo ya wanasiasa na misukule yao...
 
watu masikini wa fikra wanalazimisha mawazo yao kwa wengine!siku zote hudhani wao tu ndo wanawaza kwa usahihi, watu wenye busara hukubali kichwa kingine kuwa na haki ya kuwaza vingine!bado tupo kwenye stone age na ujima!chifu akisema tuingie shimoni wote tunaingia!siku zote amini kichwa chako usifuate mkumbo!

Dada NGowi, achana na hao wanaokutukana akili zao wameziacha kwenye majukwaa ya siasa,.. Ujue mtu ambaye badala ya kujibu hoja kistaarabu analeta matusi au hawezi kuvumilia hoja mbadala ni INTELLECTUALLY DEAD, hana originality yoyote katika kufikiri na kuamua mambo. Watu hawa wanaaribu hata heshima ya JF (Great Thinkers), fb ndipo panapowafaa.
Ndio maana nasema watanzania siasa esp. za vyama vingi wamezivamia with mob psychology wanafuata upepo na maagizo ya vyama vyao tu..NACHELEA KUSEMA KWAMBA SIASA ZA MKUMBO ZA NAMNA HII IPO SIKU ATACHAGULIWA KICHAA AWE RAISI WA TANZANIA.
 
An intelligent person thinks alone! and he thinks INDEPENDENTLY! he thinks backward and forward! ukweli unauma siku zote na mti wenye matunda tu ndo hupigwa mawe! akili za kushikiwa ni zile za kufuata mkumbo wa ile staili , kama alivyosema flani namimi hivyo hivyo! ukiulizwa flani kasemaje fafanua , huna unalojua! daima kila agendum huwa na hidden agenda yenye wenyewe nyuma ya pazia! demokrasia ya kweli ya kutafuna na kumeza uchungu wa mawazo kinzani iko mbali sana hapa bongolala kwa maana wengi wetu tunaenda shule ila ujinga haututoki milele na milele! kwa IQ zetu ndogo hudhani wengine ni punguani na mawazo yao ni duni ! nani anaempa mtu haki ya kuona mwenzake ni mpumbavu? tuamke wana bongolala tunaouza wanyama hai!! tumsome Thomas Kuhn na theory yake inayoendeleza wenzetu huko mbele nasi kubakia na umaskini tu na mawazo mgando ya kufuata mkumbo!
Wewe Beki3 nani aneuza wanyama wetu kama sio nyie Manyang'au ccm? ukiwa CCM lazima akili uiweke likizo kabisa
 
Nimegundua kumbe kuna agenda ya siri kwa watu fulani wa makundi fulani walioko na nafasi fulani kisiasa kwa vyama tofauti kutaka serikali tatu ili vyeo viwe vingi , vyeo kibao , serikali kibao ofisi kibao , semina kibao, safari kibao , posho kibao , sadakalawe amina, mwenye kupata apate mwenye kukosa akose! kumbe madaraka matamu jamani hata wale waliopita nao wanayataka.

Zikiwa serikali tatu, uongo hata kama ulistaafu miaka hamsini iliyopita ila kwa CV yako uongo hukosi nawewe japo Naibu Waziri.

Ila serikali zote kama kawaida zitaendeshwa kwa kodi zetu na majasho yetu.

Mwenye masikio na asikie.

Ni mtazamo tu wa mimi kijana nisietaka kusikia mawazo ya wazee na sina chama wala itikadi wala manifesto.

An intelligent person thinks alone! and he thinks INDEPENDENTLY! he thinks backward and forward!

citation required...
ukweli unauma siku zote na mti wenye matunda tu ndo hupigwa mawe!
ukweli ni nini ? Mti wenye matunda ni upi ?

akili za kushikiwa ni zile za kufuata mkumbo wa ile staili , kama alivyosema flani namimi hivyo hivyo!

Mmmh...

daima kila agendum huwa na hidden agenda zenye wenyewe nyuma ya pazia!
Prove it !

demokrasia ya kweli ya kutafuna na kumeza uchungu wa mawazo kinzani iko mbali sana hapa bongolala kwa maana wengi wetu tunaenda shule ila ujinga haututoki milele na milele!

Vipi kuhusu demokrasia ya uwongo ya kuunganisha nchi mbili, huku moja ikiendelea kuwa nchi na nyingine ikiwa ni nchi ndani ya nchi ?

kwa IQ zetu ndogo hudhani wengine ni punguani na mawazo yao ni duni !

Wewe na nani mna iq ndogo...kwa mawazo uliyoweka ni mawazo ya IQ kubwa sana kwa House girl

nani anaempa mtu haki ya kuona mwenzake ni mpumbavu?
usipoonwa na watu unafikiri utajuaje kwamba kweli ni pumbafu ?

tuamke wana bongolala tunaouza wanyama hai!!

Jitahidi kusoma makala za Richard Mabala zitakusaidia kuamka wewe na bongolala wenzenu.
 
Acha kukurupuka, jibu hoja... Hao mawaziri wasiokuwa na wizara maalumu wanaisaidia nchi nini zaidi ya kula fedha za walipa kodi? Wakuu wa mikoa, Wakuu wa wilaya wanafanyakazi gani ya maendeleo kwa wananchi? acha kushupaa bora uwe unaduwaa pengine utakuwa na nafasi ya kujifunza Mkuu...
Hawa mabeki tatu wenye kuchukua ubin wa Mabosi zao huwa mnashida sana... Nani amekuambia kuwa Serikali tatu itakuwa na vyeo vingi. posho nyingi, na safari nyingi kama JK? ... Kwataarifa yako wenye akili wanataka kufuta vyeo vya Upendeleo vya CCM kama DC, RC, Wabunge wa Kuteuliwa na Mawaziri kibao wengine eti hawana wizara maalumu?... wewe unajua kuwa Sitta na watu wake wakikaa pale Dodoma kwa siku wanakunja kiasi gani? Unafahamu kuwa Msafara wa Pinda Pekee kwa siku unagharimu mishahara ya Waalimu wasiopungua 100 kwa mwaka? talking shit ... Hizo safari za JK mpaka sasa unafahamu kuwa zingetosha kujenga Hospitali za kisasa mikoa yote ya Tanzania?... Unajua kuwa Ufisadi unaofanywa kwenye sekta ya Nishati pekee inatosheleza kutoa huduma bora ya elimu na afya bure kwa Watanzania wote?... Ukoo wa Ngowi tunaufahamu una watu wengi wazalendo wenye akili, usiwavunjie heshima ...[/QUOTE

Kwa hiyo Mzee wa matukio hayo matukio yote uliyoorodhesha jibu lake ni serikali tatu? Hivi kukiwa na serikali tatu hakutakuwa na msafara wa Waziri Mkuu ehee, maana kunaweza kukawa hakuna wakuu wa mikoa lakini kukawa na magavana, au mameya wote ni mbadala yaani ni kama kutoka sangara, ukaita m4c na kuongeza chopa lakini kiti ni kilekile au wali ukaita ubwabwa. ingekuwa vyema uache kwenda na hali ya hewa, msimu na matukio kama mzee wa onyo jenga hoja.
 
haya sawa mmeona s3 wafugaji na wakulima hawatanufaika na chocho lakini s2 kwa miaka yote 50 sio tu kutowanufaisha wakulima bali imewafirisi kabisa na msaada wao mkubwa ni kuvunja kabisa muungano ili kuchoma kichaka cha ccm mfilisi
 
Mbona huzungumzii serikali mbili nani alishilikishwa na nani anazihitaj? Kwakua moja haiwezekani njia nyingine ni tatu nakama unahitaji moja basi tuzalisha mataifa mengine duniani kwa maana ya nchi ya Zanzibar na nchi ya Tanganyika lakini kwa mfumo wa mbili kwa sasa watanganyika wengi tumechoka kama bado nahisi ni ww tu
 
Haya yote ni bure. Kwa nini Zanzibar isiwe mkoa tu kama Kigoma? Serikali moja inatosha
 
Nimegundua kumbe kuna agenda ya siri kwa watu fulani wa makundi fulani walioko na nafasi fulani kisiasa kwa vyama tofauti kutaka serikali tatu ili vyeo viwe vingi , vyeo kibao , serikali kibao ofisi kibao , semina kibao, safari kibao , posho kibao , sadakalawe amina, mwenye kupata apate mwenye kukosa akose! kumbe madaraka matamu jamani hata wale waliopita nao wanayataka.

Zikiwa serikali tatu, uongo hata kama ulistaafu miaka hamsini iliyopita ila kwa CV yako uongo hukosi nawewe japo Naibu Waziri.

Ila serikali zote kama kawaida zitaendeshwa kwa kodi zetu na majasho yetu.

Mwenye masikio na asikie.

Ni mtazamo tu wa mimi kijana nisietaka kusikia mawazo ya wazee na sina chama wala itikadi wala manifesto.
Jifunze kujenga hoja, sio kutuletea mambo ya udaku. Umegunduaje? Ushahidi uko wapi? N.k
 
Nimegundua kumbe kuna agenda ya siri kwa watu fulani wa makundi fulani walioko na nafasi fulani kisiasa kwa vyama tofauti kutaka serikali tatu ili vyeo viwe vingi , vyeo kibao , serikali kibao ofisi kibao , semina kibao, safari kibao , posho kibao , sadakalawe amina, mwenye kupata apate mwenye kukosa akose! kumbe madaraka matamu jamani hata wale waliopita nao wanayataka.

Zikiwa serikali tatu, uongo hata kama ulistaafu miaka hamsini iliyopita ila kwa CV yako uongo hukosi nawewe japo Naibu Waziri.

Ila serikali zote kama kawaida zitaendeshwa kwa kodi zetu na majasho yetu.

Mwenye masikio na asikie.

Ni mtazamo tu wa mimi kijana nisietaka kusikia mawazo ya wazee na sina chama wala itikadi wala manifesto.

Katika waliovurugwa ww ni wakwanza kuvurugwa tena umevurugwa mpaka unapoteza mwelekeo. na ni bora umejisemea ukweli kuwa huna chama hii ni kutokana na kuvurugwa vibaya mpaka unakisahau chama chako. chama unacho lkn kwa kuwa umevurugwa hujitambui na hata chama chako umekisahau.
 
mary ngowi i think your head isnt right,ccm imekufanyia nini miaka yote hii,please jisikie hata huruma kwa watanzania ambao wanaishi maisha ya shida,
 
Mkulima hahitaji serikali tatu anachotaka ni serikali moja itakayompa uhuru wa kumiliki ardhi na kulima popote na kuuza popote

Mfanyabiashara anachotaka ni serikali moja yenye sheria za biashara na kodi za aina moja na taratibu za aina moja zinazomwezesha kufanya biashara popote bila bughudha ya aina yoyote

Mfanyakazi angependa kuwe na serikali moja ambapo yuko huru kufanya kazi popote na kwa viwango sawia vya mishahara na marupurupu

Mvuvi angependa serikali moja inayomwezesha kuvua popote na kujiuzia popote

Kiongozi wa dini angependa serikali moja yenye sheria moja ambayo inamwezesha yeye kutangaza dini yake na kuabudisha popote bila vikwazo

Mwanafunzi angependa awe huru kusoma popote na kupata mkopo wa kusoma popote

Lakini wanasiasa ndio wanataka serikali tatu ili wawe na nyimbo zao,majeshi yao,balozi zao,na vyeo vyao vya kisiasa na mafungu yao ya kugawana mapato yatokanayo na kukamua kodi wanyonge

Wakili wa kujitegemea angependa serikali moja ya kumwezesha kufanya kazi zake popote bila vikwazo ndani ya nchi moja.

Mfugaji wa kuhama hama angependa serikali moja inayoruhusu yeye kujichungia mifugo yake popote penye malisho mazuri ya mifugo yake

Hivi hiyo tume ya Warioba ina uhakika kuwa wananchi ndio wanataka serikali tatu?

Mimi baada ya kuwahoji wanachi wa kawaida wengi wameruka kuwa hilo la serikali tatu anayelijua vizuri ni huyo warioba na tume yake na hao wanasiasa wa UKAWA.

Wataka serikali tatu wanaotoa hadi mapovu ni wanasiasa ambao wanaishi kwa kutegemea siasa tu na wanaofaidika na ulaji kodi za wananchi ila wanajaribu kutumia wananchi kama ngao ya ubaradhuli wao.

Chadema na CUF wanajua kuwa si rahisi wao kushika nchi ikiwa moja kwa sababu CUF ina nguvu sana Zanzibar lakini bara haina nguvu hivyo nchi ikiwa moja wanajua hawatapata kura bara na CHADEMA wanaona kukiwa na serikali moja watakwama kwa kuwa wana nguvu sana Tanzania bara lakini Zanzibar hawana nguvu hivyo kukitokea uchaguzi kukiwa na serikali moja wanajua watakwama. Hivyo makundi haya mawili ya CUF na CHADEMA yanapigania serikali tatu kwa kuota ndoto za Alnacha kuwa zikipatikana basi CUF itashika Zanzibar CHADEMA tashika BARA na CCM itaambulia hako kaserikali ka muungano kasikokuwa na NGUVU wala raslimali bali kanategemea michango ya washirika.

Ukweli ndio huo wanasiasa ndio wanataka serikali tatu na warioba akaona muhimu kuwasikiliza hao na akayaita eti ndio maoni ya wananchi sio kweli.

Katika vitu vya aibu ambavyo tume imefanya ni kuchukua maoni ya wanasiasa kuhusu serikali tatu na kuyaita maoni ya wananchi .Ni aibu kwa tume. Najisikia vibaya tume kwa hili imekula posho ZA KODI ZA WANANCHI bure kabisa.

Umeolewa?
 
Back
Top Bottom