Kwa mantiki yako mkuu unamaanisha kuwa ili usichapiwe umeainisha mambo mawili.Wapi nimesema umridhishe mwanamke?
Mkuu mbona mada ipo wazi lakini unapuyanga tuu.
Nimesema ili usichapiwe kitu cha kwanza, shika amri na maagizo ya Mungu. Cha pili, Oa Bikra.
Sasa sijui hayo maneno umeyatoa wapi.
Kwa mantiki yako mkuu unamaanisha kuwa ili usichapiwe umeainisha mambo mawili.
Msimamo wangu ni kwamba HAYATOSHI KUKUFANYA USICHAPIWE.
Nafikiria vizuri tu mkuu.Utakuwa hufikiri vizuri Mkuu.
Hivi unajua kushika amri za Mungu ndio kila kitu kwenye huu ulimwengu?
Nafikiria vizuri tu mkuu.
Tatizo wewe unaweza imani kubwa sana kwenye hii jinsia, wapo walioamini kuwa wanawake wao kupita kiasi.
Hujawahi sikia thread humu kuwa pastor anakula mke wa jamaa?
Mada tamu sana.Narudia, sijasema mtu amuamini mwanamke. nilichosema Shika amri na Magizo ya Mungu.
Mhubiri 12
12 Tena, zaidi ya hayo, mwanangu, kubali maonyo; hakuna mwisho wo wote wa kutunga vitabu vingi; na kusoma sana huuchosha mwili.
13 Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu.
14 Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya.
Mada tamu sana.
Ngoja nivute seat niendelee kuona michango mingine ya wadau.
Vp wanawake decent waliobakwa na kutolewa bikira wanaangukia kund gan?! Unadhan yule aliembaka akimpenda huyo dada na kumjali anaweza kuweka moyo wake wote hapo?!
Sent using Jamii Forums mobile app
Haya ni maandiko enzi za hukumu kwa torati. Sahv tunakombolewa kwa Neema. Ina maana dhambi imekuwa kubwa kias kwamba tukitumia torati haponi mtu.Sheria za Ubakaji si zipo Mkuu?
Mbona watu mnafanya jambo hili kuwa gumu wakati ni uji. Nakupa andiko kuhusu wabakaji
Kumbukumbu la torati 22
25 Lakini yule mtu mume kama akimkuta kondeni kijana aliyeposwa, naye mume akamtenza nguvu, akalala naye; yule mtu mume aliyelala naye na afe pekee;
26 lakini yule kijana usimfanye neno; hana dhambi yule kijana ipasayo kuuawa, kwa kuwa ni mfano wa mtu kumwondokea mwenzake akamwua, ni vivyo lilivyo jambo hili;
27 kwani alimkuta kondeni; yule kijana aliyeposwa akalia, pasiwe na mtu wa kumwokoa.
Sheria Tanzania ni kufungwa miaka 30. Hivyo hapo hakuna ndoa.
Duh aisee, hata mimi hili jibu limeniacha na bumbuwazi.Yaani mapenzi yanakuwa hot inatokea hadi kufa mnaweza msipishane hata mwaka.
Mwanamke uliyemtoa bikra ukimjali hata kama huna hela za magorofa na magari si rahisi kuchepuka. Lakini upande wa pili ni kucheza na shilingi chooni.
Embu sikia hii stori ya kweli kumhusu Dada yangu ambayo bila shaka anasadifu wanawake wengi duniani.
Ilikuwa ni harusi ya Dada yangu, Miaka mitano iliyopita. Dada alikuwa amerembwa akarembeka. Kila mmoja home alifurahi nikiwamo mimi. Yalikuwa ni mafanikio ya familia yetu kuona dada yetu akiingia katika ulimwengu wa ndoa. Siku ya Harusi iliwadia. nderemo na shamra shamra zilitawala. Wenye madera walikuwepo, suti haya, magauni ya gharama nao hawakuwa nyuma basi ilimradi harusi ifaane. Matarumbeta na ngoma ziliwafanya waalikwa kuiona siku ile hakuna nyingine ingefuata kumbe ni hisia tuu za furaha.
Tulikuwa ukumbini, maputo na vitu kama unyoya unyoya vilikuwa vikiranda randa mule ukumbini mwa kanisa. Dada yangu alikuwa kapendeza sana. Alivalishwa gauni jeupe kubwa ungedhani asingeweza kuliburuza. Muda mwingi alikuwa kajificha kwa aibu ndani ya shela. Wengi walitaka afunuliwe ili wamuone vizuri lakini wakumfunua alikuwa ni mmoja naam ndiye huyo shemeji yangu aliyekuwa anamuoa.
Muda wa kula viapo uliwadia, sikuamini nilichokiona. Nilimuona Dada akilia kwa hisia kali sana hali iliyompa tabu mshenga wake kumfuta kila mara machozi yake. Moyoni nilijiuliza badala dada afurahi anaolewa yeye analia, ni furaha gani kupitiliza hiyo.
Hatimaye ndoa ilifungwa na historia ikaandikwa.
Baada miezi kadhaa kupita nilienda kumtembelea Dada yangu. Nilipofika tulipiga soga za hapa na pale. Nyingi zilikuwa ni kukumbuka baadhi ya matukio ya harusi yake. Alinionyesha baadhi ya picha na mwisho aliweka CD ya harusi yake. Ndipo nikakumbuka kumuuliza kwa nini alilia siku ile kwa hisia kiasi kile. Hii ni Baada ya kuona kipande kikimuonyesha akilia kwa kwikwi.
Sio Mimi tuu hata wewe usingeamini jibu alilonipa. lilikuwa jibu lililopasua mishipa ya moyo wangu na kufanya mwili kufa ganzi. Aliniambia kuwa alilia kwa sababu hakuamini kama kweli Allen hatamuoa. Binafsi sikumjua huyo Allen zaidi ya Shemeji aliyefunga naye ndoa siku ile. Aliongeza kusema; kilichoniliza si furaha ya kuolewa bali hakuamini ni kweli Alleni mwanaume aliyempenda kwa dhati kuwa hatamuoa tena.
Binafsi nilishikwa na kigugumizi.
mkuu stori hii inahusu wadada wengi wanaoolewa. Wewe wakati unadhani mwanamke unayemuoa analia kwa furaha siku ukiwa kanisani. Kumbe mwenzako analia kutokuamini kuwa hivi ni kweli hatakuwa tena na Ex wake.