Siri ya jiji la Mwanza kuendelea bila msaada wa Serikali

Mwasita Moja

JF-Expert Member
Dec 31, 2015
2,903
2,580
Tangu tupate uhuru mwaka 1961 , mikoa ya Tanzania imeendelea kukua hatua kwa hatua. Mkoa wa Dares salaam ulikuwa mkoa wa kwanza kufikia hadhi ya kuwa jiji. Lakini nyuma ya mkoa wa Dar kuna uwekezaji mkubwa ulifanywa na serikali, mfano ujenzi wa wizara mbali mbali, ujenzi wa barabara za lami, ujenzi wa vyuo mbali mbali, ujenzi wa hospital kubwa etc.

Hali ni hiyo hiyo kwa majiji mengine yamekuja kufikia hadhi ya kuwa jiji baada ya sapoti kubwa sana ya serikali, angalia mfano jiji la Arusha imejengewa barabara, mahoteli makubwa, na kumbi mbali mbali za kimataifa na serikali.

Mkoa wa mwanza ulifikia hadhi ya kuwa jiji mwaka 2000 na kutangazwa rasmi kuwa jiji na rais wa awamu ya tatu William Mkapa.
Mpaka Mwanza inafikia hadhi ya kuwa jiji hamna la maana lolote serikali ilikuwa imefanya kuusaidia mkoa, mfano hamna vyuo vikubwa vya serikali, hakuna kumbi za kimataifa za serikali ,pia ni nadra kuona viongozi wa serikali wakifanya ziara na kuhamasisha shughuli za maendeleo mkoa wa mwanza.

Je pamoja na kutengwa kote huku kwa nini mwanza ilikuwa ya pili kuwa jiji na kimaendeleo na kuicha mikoa mingine ambayo imekuwa ikipendelewa tangu enzi za ukoloni??

Siri ni wakazi wake kufanya kazi kwa bidii na pia ni wakarimu sana .
Wageni kutoka nchi zingine na mikoa mingine hupokelewa na kuishi kwa amani kabisa bila kubaguliwa.
Kuna baadhi ya mikoa wenyeji wake ni wachoyo na wabinafsi kiasi kwamba mgeni akifungua biashara wanamfanyia vigisu mpaka afunge biashara yake.
Hali ni tofauti kabisa katika aridhi ya usukumani.
Hongereni sana Wasukuma na Mungu awabariki Sana.
 
Kwahiyo hiyo ndio sababu rais anafanya ziara na teuzi hapo Mwanza tu au kuna jingine
 
Fishing industry miaka ya nyuma ilishamiri kuliko mahala popote tanzania, Kumbuka enzi madege makubwa yakiyokuwa yanachukua samaki kila wiki biashara iliyovutia industrialization na kustimulate employment.
Meli zilizoiunganisha mwanza na kenya na uganda hili halikuwepo mahala popote
Dhahabu za geita,Almasi mabuki,nakangwa misungwi zote zilikuwa kituo cha kuwekeza hizo pesa ni mwanza.
Kumbuka Magari kutoka Congo, etc waliokuwa wanafuata kayabo, dagaa mwaloni hilo lilikuwa halipo popote.
Watu wote waliokuwa wanahitaji kwenda kwao Mara/Musoma au Bukoba kituo kilikuwa ni mwanza maana hakukua na jinsi rahisi ya kwenda moja kwa moja kama sasa.

Hizi faida na nyingine nyingi ziliifanya mwanza lazima iendelee automatically.
 
Kumbe ni tatizo la historia,Mwanza ilikuwa ngangali enzi za mkoloni,lakini ilishuka wakati wa utawala wa mtu mweusi.Azia hapo.
 
Tangu tupate uhuru mwaka 1961 , mikoa ya Tanzania imeendelea kukua hatua kwa hatua. Mkoa wa Dares salaam ulikuwa mkoa wa kwanza kufikia hadhi ya kuwa jiji. Lakini nyuma ya mkoa wa Dar kuna uwekezaji mkubwa ulifanywa na serikali, mfano ujenzi wa wizara mbali mbali, ujenzi wa barabara za lami, ujenzi wa vyuo mbali mbali, ujenzi wa hospital kubwa etc.

Hali ni hiyo hiyo kwa majiji mengine yamekuja kufikia hadhi ya kuwa jiji baada ya sapoti kubwa sana ya serikali, angalia mfano jiji la Arusha imejengewa barabara, mahoteli makubwa, na kumbi mbali mbali za kimataifa na serikali.

Mkoa wa mwanza ulifikia hadhi ya kuwa jiji mwaka 2000 na kutangazwa rasmi kuwa jiji na rais wa awamu ya tatu William Mkapa.
Mpaka Mwanza inafikia hadhi ya kuwa jiji hamna la maana lolote serikali ilikuwa imefanya kuusaidia mkoa, mfano hamna vyuo vikubwa vya serikali, hakuna kumbi za kimataifa za serikali ,pia ni nadra kuona viongozi wa serikali wakifanya ziara na kuhamasisha shughuli za maendeleo mkoa wa mwanza.

Je pamoja na kutengwa kote huku kwa nini mwanza ilikuwa ya pili kuwa jiji na kimaendeleo na kuicha mikoa mingine ambayo imekuwa ikipendelewa tangu enzi za ukoloni??

Siri ni wakazi wake kufanya kazi kwa bidii na pia ni wakarimu sana .
Wageni kutoka nchi zingine na mikoa mingine hupokelewa na kuishi kwa amani kabisa bila kubaguliwa.
Kuna baadhi ya mikoa wenyeji wake ni wachoyo na wabinafsi kiasi kwamba mgeni akifungua biashara wanamfanyia vigisu mpaka afunge biashara yake.
Hali ni tofauti kabisa katika aridhi ya usukumani.
Hongereni sana Wasukuma na Mungu awabariki Sana.

Kweli umenena kuchapa kazi ndo suluhisho .
 
Back
Top Bottom