Siri saba (7) ambazo ni lazima umfahamishe mwenza wako

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,597
215,346
Uaminifu ni msingi wa mapenzi, wako wanaodhani mapenzi yanaweza kushinda kila jaribu lakini ukweli ni kwamba bila uaminifu mapenzi hayana afya njema

1. Usimfiche mwenza wako hali yako ya kifedha. Kama una madeni, kipato kimepungua, unaweka pesa kwa aajili ya kitu fulani. Yawekeni wazi.

2. Mahusiano ya pembeni, ikiwa hakuwa muaminifu ni kheri useme mapema na kuomba radhi, usenet na sababu ya kuvunja uaminifu. Ikipelekea uhusiano kuvunjika kutokana na ukweli wako ni kheri kuliko she agunduebaadae mfanyiane visa.

3. Kama ulishawahi kuwa mhalifu na ukafungwa jela au una rekodi polisi. Nikheri uyaweke wazi. Haya mambo hayafichiki.

4. Hali yako ya kiafya, kama ulishapata matatizo ya afya ya akili, Ukoo una magonjwa ya kurithi (genetic issues), HIV nk ni kheri uyaweke wazi.

5. Kama uliwahi kubakwa ukiwa mtoto, mara nyingi huathiri afya ya akili ukubwani kama tatizo halikukabiliwa kitaalamu. Watoto wa kiume hii huaathiri sana ukubwani.
 
Ni vyema pia ukapata kumfahamu vyema (kwa undani) mwenza uliyenaye kabla ya kumkabidhi baadhi ya hizo [siri].

La sivyo, kesho yake unaweza kuikuta 'siri yako' ikiranda randa mitaani!
Ninadhani hatua muhimu katika dating ni kupima uwezo wa mwenzako kutunza siri. Ukishajua si mtu za Siri lakini moyo umempenda ya kwako yahifadhi.
 
labda Kama mmekutana toka utotoni huko vijijini unaweza fanya hivyo,
Ila ki mjini mjini huwa kinachowekwa wazi ni hiyo namba moja tena kwa asilimia 60% kushuka chini.
Fikiria unatika kazini unakuta nguo zako zote zimekula mkasi. Unaona hii si hali ya kawaida. Mnaenda hospitali mnapewa referral Mirembe. Kumbe kule mwenzako anajulikana na file lake wanalipa.
 
Fikiria unatika kazini unakuta nguo zako zote zimekula mkasi. Unaona hii si hali ya kawaida. Mnaenda hospitali mnapewa referral Mirembe. Kumbe kule mwenzako anajulikana na file lake wanalipa.
hao huwa wanakuwa na uwendawazimu wa mapenzi tu na ukijitia nawe kichaa ukakomaa naye mpaka ndoa,
Hawakawii kukuvizia wakala nanilii ukiwa umelela.
 
Kwenye Kikao Chetu cha mwisho wanaume tulishalimaliza hilo mimi kama Katibu acha niwakumbushe
hakuna kutoa siri zetu kirahisi ivyo tutafanya hivyo panapotokea ulazima tu
kwenye swala la kipato tunatakiwa kuwajuza wapenzi ambao tunamalengo nao au wake zetu kwa 60% kushuka chini
hautakiwi kumpa mwanamke historia Yako Chafu vingine tunamezea biblia imeandika wanawake tuishi nao kwa akili
 
Yaani we manka sikuelewi nimekuoa una 25 yrs na haukuwa na bikira unaniambia John alikuwa ananipanua, halafu eti tukaachana na John anakuwa jirani yetu. Unadhani ni salama sana?
Ee ni rahisi hivyo? Mbulaaaa
 
Yaani we manka sikuelewi nimekuoa una 25 yrs na haukuwa na bikira unaniambia John alikuwa ananipanua, halafu eti tukaachana na John anakuwa jirani yetu. Unadhani ni salama sana?
Ee ni rahisi hivyo? Mbulaaaa
Mhh hapa unaeleza ulivyoteleza ukiwa kwenye ndoa.
 
Back
Top Bottom