Siri nzito yafichuka kuhusu waraka wa Kanisa Katoliki

Siri nzito yafichuka kuhusu waraka wa Kanisa Katoliki

chupa ya maji

Member
Joined
Oct 31, 2017
Posts
58
Reaction score
68
*SIRI IMEFICHUKA!!!!!!*

• Maaskofu waukana Ujumbe wa Pasaka.
• Maaskofu 4 wa TEC waliouandika wajulikana
• Majina yao haya hapa, kwa taarifa za uhakika.

Nimeshtushwa sana na taarifa niliyoipata juu ya Ujumbe wa Kwaresima uliotolewa na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) ulioelekezwa kwa waumini wakati huu wa toba ya Kwaresima iliyoanza Februari 14, 2018 hadi Pasaka siku ya kusherehekea ufufuko wa Bwana Yesu Kristo (Pasaka).

Mimi ni Mkatoliki wa Jimbo la Dodoma na Askofu wangu ni Mhashamu Askofu Mkuu Beatus Kinyaiya.

Nikiri nilianza kupata mashaka tangu mapema ujumbe huu ulipotoka, nilijiuliza sana na hivyo nikaamua kufanya juhudi za kujua kama kweli Kanisa langu Katoliki limefikia hatua hii? Naujua utaratibu na utamaduni wa kanisa langu ndio maana nilipatwa na mashaka haya.

Kwa ambao hawajausoma ujumbe huu, ulikuwa na sura nne lakini iliyoleta tafrani ni sura ya tatu yenye ujumbe kuhusu “Dalili za nyakati zetu Tanzania” hususani katika kipengele cha siasa. Imeleta tafrani kwa sababu katika eneo hili ujumbe huu umeenda kwenye masuala ambayo siku zote yamesababisha kuwepo malumbano kuwa viongozi wa dini wanaingia mambo ya kisiasa ama wanachanganya dini na siasa.

Kwa ufupi kabisa ujumbe huu umetoa shutuma na bila shaka dhidi ya Serikali inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli kuwa shughuli za siasa kama vile uenezi, mikutano ya hadhara, maandamano, makongamano, mijadala na mikutano ya ndani zinazuiwa kwa kutumia vyombo vya dola.

Ujumbe unaendelea kushutumu kuwa vyombo vya habari vimefungiwa au kusimamishwa kwa muda, uhuru wa Mahakama na Bunge unaminywa na kwamba katika mazingira haya ni rahisi kwa jamii kufarakana na hata kujenga chuki kiasi cha kuhatarisha amani, usalama na hadhi ya uhai wa binadamu.

Ujumbe umeongeza shutuma nyingine kuwa chaguzi zinaharibiwa kwa vurugu na hivyo kuacha nyuma uchungu, hasira, tamaa ya kulipa kisasi na hata kususia chaguzi nyingine na kwamba hali hiyo ni hatari kwa mustakabali wa Taifa letu, ikiachwa izoeleke tusishangae huko mbele kujikuta katika mifarakano mikubwa zaidi itakayobomoa misingi ya amani na umoja wa kitaifa.

NIMEPATA TAARIFA ZA UHAKIKA KABISA kuwa ujumbe huu haukuandikwa na Maaskofu 35 wa Kanisa Katoliki kama ilivyotolewa na Baraza la Maaskofu (TEC).

Katika shauku yangu hii ya kutaka kujua kwa nini viongozi wangu wa Kanisa lenye heshima hapa nchini wamefikia hatua hii nimepata taarifa za uhakika kuwa Maaskofu walioshiriki kuandika ujumbe huu ni wanne (nitawataja huko mbele) na Maaskofu wengine walikataa kushiriki kikao kilichofanya kazi ya kuandika ujumbe huu.

Mniwie radhi sana nimepata mashaka makubwa sana niliposoma majina ya Maaskofu waliofanya kazi ya kuandika ujumbe huu na historia zao za mahubiri yenye uchochezi mkubwa na hata mara kadhaa wametuhumiwa kwa ukabila na uchochezi na ushahidi upo.

Maaskofu walioandika ujumbe huu ni Mhashamu Askofu Mkuu Beatus Kinyaiya wa Jimbo Kuu la Dodoma, Mhashamu Askofu Mkuu Yuda Thaddaeus Ruwa’ichi wa Jimbo Kuu la Mwanza, Mhashamu Askofu Augustino Shao wa Jimbo la Zanzibar na Mhashamu Askofu Severine Niwemugizi wa Jimbo la Rulenge-Ngara.

Maaskofu wengine hawakushiriki kuandika ujumbe huu na kwa kuwa wanatambua dosari iliyokuwa inafanyika wakatoa udhuru mbalimbali na kwa hivyo hao Maaskofu wanne wakaifanya kazi hiyo wakishirikiana na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania Padre Raymond Saba na wakamchukua Dk. Kasala kama mshauri wa uandishi wa ujumbe huo.

Kwa kuangalia safu hiyo utaona ujumbe huu umeandikwa pasi kuwepo Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania Mhashamu Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa wala Mwadhama Polyacarp Kardinali Pengo wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam.

Nimepata taarifa kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Songea Mhashamu Damian Dallu aliondoka mkutanoni na kuomba udhuru baada ya kubaini mwelekeo wa ujumbe huu.

Hapo ni kujiuliza kwa nini? Na kama kuna yeyote hayaamini haya basi na awaulize viongozi hawa kama walishiriki kuandika ujumbe huo, naamini hata wao wamekwazika na kwa namna yeyote hawawezi kukubaliana na yaliyomo katika ujumbe huu hata kama wat
 
Katika shauku yangu hii ya kutaka kujua kwa nini viongozi wangu wa Kanisa lenye heshima hapa nchini wamefikia hatua hii nimepata taarifa za uhakika kuwa Maaskofu walioshiriki kuandika ujumbe huu ni wanne (nitawataja huko mbele) na Maaskofu wengine walikataa kushiriki kikao kilichofanya kazi ya kuandika ujumbe huu.

Kwani ili maamuzi na kikao/ mkutano kiwe/ uwe halali wanatakiwa maaskofu wangapi kwa kiwango cha chini (quorum)? Je, mahudhurio yalichukuliwa mwanzo wa kikao?

Maaskofu walioandika ujumbe huu ni Mhashamu Askofu Mkuu Beatus Kinyaiya wa Jimbo Kuu la Dodoma, Mhashamu Askofu Mkuu Yuda Thaddaeus Ruwa’ichi wa Jimbo Kuu la Mwanza, Mhashamu Askofu Augustino Shao wa Jimbo la Zanzibar na Mhashamu Askofu Severine Niwemugizi wa Jimbo la Rulenge-Ngara.

Je, sio ndio waliounda kamati ndogo ili kufanya kazi hiyo kwa baraka za baraza?

Maaskofu wengine hawakushiriki kuandika ujumbe huu na kwa kuwa wanatambua dosari iliyokuwa inafanyika wakatoa udhuru mbalimbali na kwa hivyo hao Maaskofu wanne wakaifanya kazi hiyo wakishirikiana na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania Padre Raymond Saba na wakamchukua Dk. Kasala kama mshauri wa uandishi wa ujumbe huo.

Hivi idadi ya chini (quorum) ya mkutano uzingatiwa mkutano unapoanza au unapoisha? Zaidi ya hilo, je ni idadi gani ya wajumbe inatakiwa ili kupitisha maamuzi? Kama unapoanza na wengi wakatoa hudhuru katikati na kuendea mwishoni, na maamuzi ya mwisho yakawa hao wanne waandike yaliyojadiliwa kufuatia idadi ya waamuzi kwa mujibu wa taratibu zao za kikao, tatizo lipo wapi? Wahudhuriaji wa kikao ni wale walioandika majina yao mwanzo wa kikao hata kama waliondoka baadae, na ndio maana orodha ile ni ndefu kiasi hicho. Na yawezekana walibariki maamuzi ambayo yalifuata.

Nimepata taarifa kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Songea Mhashamu Damian Dallu aliondoka mkutanoni na kuomba udhuru baada ya kubaini mwelekeo wa ujumbe huu.

Kuondoka kwa huyo askofu hakufanyi mkutano huo kutokuwa halali kwa mujibu wa taratibu za mikutano. Na kama aliomba hudhuru wakati mwanzo aliandika jina lake kwenye mahudhurio basi bila shaka alihudhuria.

Hapo ni kujiuliza kwa nini? Na kama kuna yeyote hayaamini haya basi na awaulize viongozi hawa kama walishiriki kuandika ujumbe huo, naamini hata wao wamekwazika na kwa namna yeyote hawawezi kukubaliana na yaliyomo katika ujumbe huu hata kama wat

Mimi siwaulizi wala nini? Ila naomba tupewe orodha original ya mahudhurio ya mkutano huo. Kama vitabu vya yule kasisi wa KKKT, Fred Njama, vinakusanywa (Vitabu vya mchungaji KKKT vyakusanywa), basi huu ni mpango wa kuvikusanya na hivi vya Katoliki kwa makubaliano fulani. Pathetic.

Mimi nilikwisha nunua nakala yangu kutoka kwenye meza ya visakramenti Parokiani kwetu. Na huo waraka ni moja ya visakramenti. Ninakitunza sana kwa ajili ya kuchangia kwenye historia ya taifa letu kwa vizazi vijavyo.
 
Mniwie radhi sana nimepata mashaka makubwa sana niliposoma majina ya Maaskofu waliofanya kazi ya kuandika ujumbe huu na historia zao za mahubiri yenye uchochezi mkubwa na hata mara kadhaa wametuhumiwa kwa ukabila na uchochezi na ushahidi upo.
Kwanza unaitwa mchochezi
Kisha utaitwa msaliti
Kinachofuata hapo Mungu Epushia mbali.
Niyie ccm mnalaana nyie!! mpaka viongozi wadini mnawaita majina mabaya.
Kweli ukitaka kumuua mbwa mpe jina baya
 
Huo ushahidi unaoongelea uko wapi?au tuamin tuu hayo maneno yako kuwa una ushahidi...kwanza unalipwa sh ngapi kutetea hili jambo ...kikubwa tuangalie content haijalishi askofu yupi hakushiriki

Mpaka waraka ufike kwenye meza ya vitabu vya dini vya Parokia nafikiri zote, lazima utakuwa na baraka za TEC.
 
Back
Top Bottom