Siri na ugumu wa kutenda wema

Showio

JF-Expert Member
May 16, 2019
255
481
MTIHANI mmojawapo mkubwa kwenye maisha yetu ya kila siku ni kuendelee kuwa wema na kufanya mema kwa mtu/watu ambao wanaonekana hawana shukrani au pengine wanakurudIshia ubaya kabisa.

Mara nyingi kawaida ya moyo wa mwanadamu ni kutaka KUSHUKURIWA kwa kila jema analolitenda. Kama ni KIONGOZI akifanya kitu anataka asifiwe na kushukuriwa, kama ni MUME/MKE anataka ambiwe ahsante zaidi ya mara moja, kama mtu ametoa MSAADA wa Kijamii anataka kila mtu aseme neno la kumshukuru, kama mtu ametoa PESA za kusaidia mwingine anataka kusikia watu wakimshukuru n.k.

Kumbuka ARDHI huwa HAIMSHUKURU mkulima kwa KUPANDA MBEGU ila hilo halimkatishi tamaa mkulima kuendelea kupanda mbegu zake na kuzimwagilia ili aje kuvuna.

Ndio maana waswahili walisema: TENDA wema USINGOJE shukrani.Kumbuka ukitaka KULIPWA na KUSHUKURIWA na WANADAMU hautapata MALIPO ambayo MUNGU huwa ANAYATOA kwa WATENDA MEMA. USICHOKE wala USIZIMIE MOYO, ENDELEA KUTENDA MEMA!
 
Back
Top Bottom