Siri: Lipumba aja na agendas mfukoni

Siri: Lipumba aja na agendas mfukoni

GHIBUU

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2011
Posts
4,432
Reaction score
3,016
Kila mtu anayechukia ukoloni wa CCM, anafahamu fika kwamba Lipumba ana ‘issue’ kibindoni tayari alizopangiwa na CCM, anakujanazo ndani ya CUF kwa kuzitekeleza.

(l) Kutaka kuzima au kubabaisha mataifa katika madai yaliyopo juu ya meza ya wazanzibari kuhusiana na matokeo ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, 2015.

(ll) Atataka kuitambua au niseme atajaribu kusema kwamba uchaguzi wa marudio wa Machi 20 ulistahili kisheria na kikatiba kufanywa, hivyo ulikuwa halali. Atasema, baada ya kutafakari vya kutosha CUF, imebadilisha uamuzi wake na sasa inaitambua serikali ya Dk Shein.

(lll) Pia, ana mkakati mzito aliyopangiwa na CCM, kufumfukuza Maalim Seif na viongozi wengine (kundi lake) ndani ya CUF (this is very serious issue), kwa sababu ya kutaka kuwachanganya kimawazo au kuwababaisha wazanzibari, wanachama na wafuwasi wa CUF, juu ya mwelekeo wa Zanzibar.

Itakumbukwa mkutano wa Kiembe Samaki wa CCM, Balozi Seif Ali Iddi (Nduli) alisema nini kuhusu CUF kuwa, mwaka huu ndiyo mwisho wake. Uchambuzi wa kitaalamu wa kauli ile ndiyo haya matokeo ya sasa.

Kuna mambo mengi ya ubaya dhidi ya wazanzibari waliyoikataa CCM, Lipumba anakuja nayo kapewa kuyatekeleza. Ndiyo sababu ‘speed’ au niseme kasi ya kumrejesha imekuwa kubwa.

CCM, wanahofu na hatua zinazochukuliwa na CUF chini ya Maalim Seif kuhusu Zanzibar na Tanzania, ambayo nayo inaathirika zaidi.
Ingawa kwa sasa tunaweza tukasema kwamba, kwa hatua iliyofikiwa kuhusu masuala ya Zanzibar, CCM wananafasi finyu na ndogo mno kunusurika na mkono wa dunia. Ndiyo maana wanajaripu kupapatua kwa njia za kijasusi, kupitia uhuni wa Lipumba na gengi lake.
Inafaa tujiulize, tena tujiulize sana tangu CUF kuasisiwa, sasa ni miaka 24 kwa hesabu, lini imetokea Mwenyekiti wake, kuanzia Mapalala kupelekwa ofisini kwa vikosi vya polisi, geti la ofisi kuvunjwa, walinzi kupigwa mabomu na uhalifu mwingine kama kweli kuna nia njema huko mbele.

Kwa Wazanzibari, haya si mageni labda kwa wenzetu upande wa bara ambao wao kwao yanaweza kuwa mageni, hawaifahamu CCM hulka yake kwa undani. Ingawa sasa kidogo kidogo wameanza kupata picha. Wazanzibari chini ya CUF, wamewazoea CCM wala hawawababaishi tena.

CCM, wanaamini kuwa dunia yote ni kama vile serikali yao ilivyo, viongozi kutembea kwa ving’ora na misururu ya gari za ulinzi kuelekea katika mikutano ya kinafiki ya hadhara na kurudi majumbani, wakisubiri siku inayofuta kwenda mashamba Unguja na Pemba, kudanganya watu.

Dunia haiku hivyo tena sasa, imebadilika. Sindano ikianguka mto-pepo, dakika hiyo hiyo wanaisikia waliyoko Toronto.
Umoja wa ulaya (EU) imesema kuhusu uchaguzi wa Zanzibar, Jumuiya ya Madola (Commonwealth), Marekani na Uingereza na kadhalika wote wamesema na kutokuitambua Serikali ya Zanzibar, Lipumba anarejeshwa CUF kwa mabavu na ajenda ya kigaidi. Nani atamkubali kumpokea gaidi mkuu wa wazanzibari?.

Mwaka wa kwanza Julius Nyerere, kufanya ziara Pemba, ilikuwa mwaka 1965 hapa ilikuwa ni mwaka mmoja tangu kuunda Muungano wa Zanzibar na Tanganyika. Mzee mmoja mwenye asili ya Tanganyika, Ibrahim Mkumba alitunga na kughani utenzi kwa ajili ya Nyerere.

“Kila ajaye kwa shari – Aijuwa yake siri – Ivunde yake dhamiri – Asiweze kusimama.”
Maneno hayo ya ushairi yalikuwamo ndani ya utenzi uliyokuwa na zaidi ya beti 110 uliyoghaniwa na Mzee Ibrahim Mkumba aliyekuwa akiishi Chanjamjawiri, pale kwenye njia inayoelekea Skuli ya Kidongo (sasa Skuli ya Chanjamjawiri).

Kwa fumbo la kishairi la Mzee Mkumba, hatunashaka kwamba, dhamira aliyonayo ndani ya nafsi yake Ibrahim Lipumba, itamsuta na hataweza kusimama. Mwenyezi Mungu Jala Jalal, hatasimama naye, hatampa nguvu za kuweza kuwafanyia ugaidi wanzanzibari. – amin.
Wazanzibari, mjini na mashamba, Pemba na Unguja ni waelewa wa mambo yote kuhusu nchi yao. Miaka zaidi ya 50 ya Muungano ‘uchwara’ wamekumbana na mengi na sasa wamechoka kuishi katika hali ngumu ya umasikini na ufukara, hawatatetereka tena na mbinu ovu za CCM. Wazanzibari wako makni sana.
 
Yani mgombane wenyewe,then ccm ihusishwe?
Wacha kuihusisha ccm na mambo ya kipumbavu.
 
Bora CCM kuliko unafiki wa MAREKANI... Wameifanya dunia mzima inanuka damu.. Alafu Leo viongozi uchwara wanaenda kuishitaki Tanzania kwa wanao watuma.. Eti wazungu mnawaona wenzenu.. Mnajisumbua bure tu
 
Hutuambii kitu tukakusikiliza Sisi Tupo na professor wetu ambaye tumepigwa wote mabomu na virungu Sio Yule Katibu mkuu anatangaza Nchi haitatawalika kisha anaenda Omani Hajawahi pigwa wala kuvunjwa Hata mkono... Chama kimerudi kwenye misingi Kwa maana mwanzilishi wa ukawa bungeni ndio kimerudi kwake
 
Kwa Zanzibar Lipumba ataishia Unguja tu
 
Mbona ata Chadema kwenye kampeni zao walisema CCM ndio mwisho wao nao walkuwa wametumwa?
 
time will continue to tell
"muda utaendelea kusema"
 
Ubarikiwe mleta mada.

Ninachoona hapa ni kwamba Lipumba atakijuruhi kwa kiasi flani CUF kwa upande mmoja (Tanganyika) Ila kwa upande wa Zanziba ni kama harakati au niseme ukombozi kama sio Mapinduzi kuzaliwa upya.

Wazanzibar kwa kiasi kikubwa wanajitambua na wanajua nini cha kufanya. Na hapa naona kama Leo Lipumba kaanza na wakurugenzi kesho sitashangaa akamgusa Maalimu Seifu, na hapo ndipo kosa kubwa la karne litakuwa limefanywa na wale wote waliopo nyuma ya Lipumba. Kwani Wazanzibar hawatakuwa na chakupoteza tena.

Wait and see
 
Kila mtu anayechukia ukoloni wa CCM, anafahamu fika kwamba Lipumba ana ‘issue’ kibindoni tayari alizopangiwa na CCM, anakujanazo ndani ya CUF kwa kuzitekeleza.

(l) Kutaka kuzima au kubabaisha mataifa katika madai yaliyopo juu ya meza ya wazanzibari kuhusiana na matokeo ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, 2015.

(ll) Atataka kuitambua au niseme atajaribu kusema kwamba uchaguzi wa marudio wa Machi 20 ulistahili kisheria na kikatiba kufanywa, hivyo ulikuwa halali. Atasema, baada ya kutafakari vya kutosha CUF, imebadilisha uamuzi wake na sasa inaitambua serikali ya Dk Shein.

(lll) Pia, ana mkakati mzito aliyopangiwa na CCM, kufumfukuza Maalim Seif na viongozi wengine (kundi lake) ndani ya CUF (this is very serious issue), kwa sababu ya kutaka kuwachanganya kimawazo au kuwababaisha wazanzibari, wanachama na wafuwasi wa CUF, juu ya mwelekeo wa Zanzibar.

Itakumbukwa mkutano wa Kiembe Samaki wa CCM, Balozi Seif Ali Iddi (Nduli) alisema nini kuhusu CUF kuwa, mwaka huu ndiyo mwisho wake. Uchambuzi wa kitaalamu wa kauli ile ndiyo haya matokeo ya sasa.

Kuna mambo mengi ya ubaya dhidi ya wazanzibari waliyoikataa CCM, Lipumba anakuja nayo kapewa kuyatekeleza. Ndiyo sababu ‘speed’ au niseme kasi ya kumrejesha imekuwa kubwa.

CCM, wanahofu na hatua zinazochukuliwa na CUF chini ya Maalim Seif kuhusu Zanzibar na Tanzania, ambayo nayo inaathirika zaidi.
Ingawa kwa sasa tunaweza tukasema kwamba, kwa hatua iliyofikiwa kuhusu masuala ya Zanzibar, CCM wananafasi finyu na ndogo mno kunusurika na mkono wa dunia. Ndiyo maana wanajaripu kupapatua kwa njia za kijasusi, kupitia uhuni wa Lipumba na gengi lake.
Inafaa tujiulize, tena tujiulize sana tangu CUF kuasisiwa, sasa ni miaka 24 kwa hesabu, lini imetokea Mwenyekiti wake, kuanzia Mapalala kupelekwa ofisini kwa vikosi vya polisi, geti la ofisi kuvunjwa, walinzi kupigwa mabomu na uhalifu mwingine kama kweli kuna nia njema huko mbele.

Kwa Wazanzibari, haya si mageni labda kwa wenzetu upande wa bara ambao wao kwao yanaweza kuwa mageni, hawaifahamu CCM hulka yake kwa undani. Ingawa sasa kidogo kidogo wameanza kupata picha. Wazanzibari chini ya CUF, wamewazoea CCM wala hawawababaishi tena.

CCM, wanaamini kuwa dunia yote ni kama vile serikali yao ilivyo, viongozi kutembea kwa ving’ora na misururu ya gari za ulinzi kuelekea katika mikutano ya kinafiki ya hadhara na kurudi majumbani, wakisubiri siku inayofuta kwenda mashamba Unguja na Pemba, kudanganya watu.

Dunia haiku hivyo tena sasa, imebadilika. Sindano ikianguka mto-pepo, dakika hiyo hiyo wanaisikia waliyoko Toronto.
Umoja wa ulaya (EU) imesema kuhusu uchaguzi wa Zanzibar, Jumuiya ya Madola (Commonwealth), Marekani na Uingereza na kadhalika wote wamesema na kutokuitambua Serikali ya Zanzibar, Lipumba anarejeshwa CUF kwa mabavu na ajenda ya kigaidi. Nani atamkubali kumpokea gaidi mkuu wa wazanzibari?.

Mwaka wa kwanza Julius Nyerere, kufanya ziara Pemba, ilikuwa mwaka 1965 hapa ilikuwa ni mwaka mmoja tangu kuunda Muungano wa Zanzibar na Tanganyika. Mzee mmoja mwenye asili ya Tanganyika, Ibrahim Mkumba alitunga na kughani utenzi kwa ajili ya Nyerere.

“Kila ajaye kwa shari – Aijuwa yake siri – Ivunde yake dhamiri – Asiweze kusimama.”
Maneno hayo ya ushairi yalikuwamo ndani ya utenzi uliyokuwa na zaidi ya beti 110 uliyoghaniwa na Mzee Ibrahim Mkumba aliyekuwa akiishi Chanjamjawiri, pale kwenye njia inayoelekea Skuli ya Kidongo (sasa Skuli ya Chanjamjawiri).

Kwa fumbo la kishairi la Mzee Mkumba, hatunashaka kwamba, dhamira aliyonayo ndani ya nafsi yake Ibrahim Lipumba, itamsuta na hataweza kusimama. Mwenyezi Mungu Jala Jalal, hatasimama naye, hatampa nguvu za kuweza kuwafanyia ugaidi wanzanzibari. – amin.
Wazanzibari, mjini na mashamba, Pemba na Unguja ni waelewa wa mambo yote kuhusu nchi yao. Miaka zaidi ya 50 ya Muungano ‘uchwara’ wamekumbana na mengi na sasa wamechoka kuishi katika hali ngumu ya umasikini na ufukara, hawatatetereka tena na mbinu ovu za CCM. Wazanzibari wako makni sana.
Hahahaha fisadi Lowasa na Dikteta MBOWE ukawa kwaheri! Mmelikoroga wenyewe mlinywe
 
Hizi fikira potofu ya kuzani Amerika, Uingereza na nchi zingine za ulaya ni sovereign zaidi ya nchi za Africa zitatutoka lini? Fikira za kuzani bado tunatawaliwa na wazungu. Mkigombana hata kidogo tu fikira zenu ni kwenda kushitakiana kwa mzungu. Kweli bado kuna waafrika wenye mgando wa akili namna hii? Mbona nchi za Asia na mabara mengine hayana watu wa fikira mgando kama hizi. Tanzania is a sovereign country like the USA, UK or any other European country. Our poverty does not make us less sovereign. In fact we are not poor in all aspects and even them are not rich in all aspects.

Mvurugano wa CUF kausababisha Maalimu Seif kwa kujifanya kuwa yeye ana madaraka makubwa kuliko Mwenyekiti wa chama chake. Yaani Mwenyekiti yuko chini yake. Hii ulishaiona kwenye chama kipi? Yaani Mbowe awe chini ya Mashilingi au Magufuli awe chini ya Kinana? Only in CUF it has existed and the Registra has ordered to stop such an unconstitutional affair. You free to appeal to our High court or you may again go to the wazungu to appeal.

Yaani Seif anamtimua kwenye chama mwenyekiti wake. Na hii si mara yake ya kwanza. Alimtimua Mapalala sasa kwa Lipumba amekwaa kisiki na atatimuliwa yeye hivi karibuni. Yaani just imagine Mashilingi amtimue Mbowe halafu ikubalike? Mrema alipokuwa mwenyekiti wa NCCR alitimuliwa na wakina Mabere, halikukubalika na Mrema aliwageuzia kibao akawatimua wakina Mabere. Huu mfano wa Mrema si sawa kabisa na huu wa Lipumba. Kaeni mkao wa kula.
 
Bora CCM kuliko unafiki wa MAREKANI... Wameifanya dunia mzima inanuka damu.. Alafu Leo viongozi uchwara wanaenda kuishitaki Tanzania kwa wanao watuma.. Eti wazungu mnawaona wenzenu.. Mnajisumbua bure tu
ulitaka tuwaone ni wenzetu wakati wa kuchangia bajeti yetu tu? mdomo huo huo unawakashifu wazungu,mdomo huo huo unabugia misaada yao. mwe!
 
Hizi fikira potofu ya kuzani Amerika, Uingereza na nchi zingine za ulaya ni sovereign zaidi ya nchi za Africa zitatutoka lini? Fikira za kuzani bado tunatawaliwa na wazungu. Mkigombana hata kidogo tu fikira zenu ni kwenda kushitakiana kwa mzungu. Kweli bado kuna waafrika wenye mgando wa akili namna hii? Mbona nchi za Asia na mabara mengine hayana watu wa fikira mgando kama hizi. Tanzania is a sovereign country like the USA.

Mvurugano wa CUF kausababisha Maalimu Seif kwa kujifanya kuwa yeye ana madaraka makubwa kuliko Mwenyekiti wa chama chake. Yaani Mwenyekiti yuko chini yake. Hii ulishaiona kwenye chama kipi? Yaani Mbowe awe chini ya Mashilingi au Magufuli awe chini ya Kinana.

Yaani Seif anamtimua kwenye chama mwenyekiti wake. Na hii si mara yake ya kwanza. Alimtimua Mapalala sasa kwa Lipumba amekwaa kisiki na atatimuliwa yeye hivi karibuni.
We kipofu, Lipumba hakutimuliwa ameondoka kwa kujiuzulu nafasi yake kwa maandishi. Wake up
 
Hutuambii kitu tukakusikiliza Sisi Tupo na professor wetu ambaye tumepigwa wote mabomu na virungu Sio Yule Katibu mkuu anatangaza Nchi haitatawalika kisha anaenda Omani Hajawahi pigwa wala kuvunjwa Hata mkono... Chama kimerudi kwenye misingi Kwa maana mwanzilishi wa ukawa bungeni ndio kimerudi kwake
kwani wakati ule alipojiuzulu katikati ya kampeni ulienda nae Rwanda? wote nyie mlimuita msaliti.kinyume na matarajio yake ameona chama kimepata wabunge na madiwani wengi zaidi anajaribu kurudi kupitia dirishani (msajili) ili awanie ruzuku. una kadi namba ngapi ya ccm?
 
Lengo hapa sio kupambana na wabunge wa CUF,Target hapa ni Maalim Seif na misimamo yake.
 
Back
Top Bottom