Siri kuu 4 usizozijua wazitumiazo wafanyabiashara wakubwa kuwa juu zaidi ya wajasiriamali

Status
Not open for further replies.

Biashara2000

JF-Expert Member
Nov 9, 2013
636
540
Habari zenu. Kutokana na umuhimu wa topic yenyewe inavyowasumbua wajasiriamali wengi wadogo nchini, nimeona umuhimu wa kutoa nafasi hii kuwafahamisha siri kuu 4 usizozijua wazitumiazo wafanyabiashara wakubwa kuwa juu zaidi ya wajasiriamali.

Kabla sijaanza kufanya biashara zangu miaka kadhaa iliyopita nilihudhuria semina kadhaa za ujasiriamali zitolewazo hapa nchini. Gharama ya mafunzo yale ilikuwa sh. 255,000 kwa siku kadhaa. Nilipotoka pale nilijaribu kutumia mafunzo yale kuyaweka katika biashara yangu ila biashara ile ikafa. Baada ya biashara ile kufa, Mungu alisaidia nikapata nafasi ya kwenda kusoma katika chuo kikuu nchini Finland kiitwacho Rovaniemi UAS (sasa Lapland UAS). Kule nilipata mafunzo kinyume kabisa na jinsi nilivyofundishwa na wale walimu waliojiita walimu bora wa ujasiriamali Tanzania.

Nikagundua kuwa wakinamama na vijana wengi nchini wanaibiwa hela zao na watoa mafunzo mbalimbali ya ujasiriamali nchini wanaotoa mafunzo yasiyosaidia kabisa kufanya biashara za wajasiriamali nchini kukua, maana kama zingekuwa zinasaidia basi leo hii tungeona mabadiliko makubwa sana katika hali za maisha za wajasiriamali wetu nchini.

Nchini Finland tulifundishwa jinsi wafanyaiashara wakubwa wanavyofanya biashara tofauti kabisa na wajasiriamali wadogo. Na hii imewasaidia biashara zao walizozianzisha zikiwa ndogo, kuwa kubwa ndani ya muda mfupi na kupata faida kubwa. Nimeamua kuwasaidia wajasiria mali wadogo nchini nao wafahamu ujuzi huu kwani baada ya kurudi nchini na kuanzisha biashara yangu ya kutengeneza mkaa wa kisasa na kutumia ujuzi ule, nimeona mabadiliko makubwa ndani ya muda mfupi. Nawe waweza fanya vivyo hivyo kwa kupata ebook (softcopy) ninayoiuza kwa sh. 15,000/- tu.

Kitakufundisha kuacha kuwa mjasiriamali na kuwa mfanyabiashara kamili mwenye kuingiza faida na si kipato cha kula chakula kwa siku. Pia kitakuonyesha ni jinsi gani umekuwa ukidanganywa na kuliwa pesa zako bure miaka nenda rudi na biashara yako hailui. Kwa anayekihitaji tafadhali usisite kuni sms, PM au kunipigia 0758 308193.

Biashara sio ngumu kama unavyodhani wala si complicated kama wao wanavyotaka ufahamu. Siri wanayotumia ni kufanya biashara ionekane ngumu ili uone huwezi kufanya ili uendelee kufikiri unahitaji elimu zaidi na kuendelea kuhudhuria mafunzo yao na wao waendelee kukuibia. Biashara inahitaji vitu 4 tu ambavyo ni rahisi kufanya na hivi ndivyo wafanyabiashara wakubwa huvitumi na wajasiriamali wadogo hawavitumii. Walimu hawa wanakutisha kwamba changamoto za biashara ni ngumu na wewe huwezi pambana nazo eti mpaka upate mafunzo yao hayo expensive, wakati ni njia nne tu unatakiwa uzitumie na hizi challenges huwezi kumbana nazo. So chukua nafasi hii kujifunza real business na si watu hawa wanaokulisha theories ambazo wao wenye haajawahi zitumia. Chaguo ni lako wengine wanasema kazi kwako.

Asanteni
 
TWanaofundisha ujasiriamali hawana hata biashara ya njugu ndo tatizo.

Pia nakushauri badili kichwa cha habari kisomeke kuwa unauza kitabu, otherwise hutakuwa na tofauti walimu wenzio.

Kwa nini unatangaza biashara yako kwa kuponda za wengine, hizo njia kuu 4 mbona huzitaji, au ndo mbinu ulizojifunza Finland?
 
Wanaofundisha ujasiriamali hawana hata biashara ya njugu ndo tatizo.

Pia nakushauri badili kichwa cha habari kisomeke kuwa unauza kitabu, otherwise hutakuwa na tofauti walimu wenzio.

Of course mi niko tofauti nao kwa sababu 2. 1. Mimi sitoi mafunzo kwa ghali. 2. Mi sitoi theory bali ni uzoefu wangu kama mfanyabiashara. Baadhi ya wana JF washawahi tembelea biashara yangu Kibaha.
 
Asante kwa ufafanuzi, lakini headline yako imekaa vibaya kiongozi,
 
TWanaofundisha ujasiriamali hawana hata biashara ya njugu ndo tatizo.

Pia nakushauri badili kichwa cha habari kisomeke kuwa unauza kitabu, otherwise hutakuwa na tofauti walimu wenzio.

Kwa nini unatangaza biashara yako kwa kuponda za wengine, hizo njia kuu 4 mbona huzitaji, au ndo mbinu ulizojifunza Finland?

kila mtu anatangaza biashara yake. Huyu nae anataka apate hizo 15,000 wakati Robert Kiyosaki anatoa material kama vile Rich Dad poor Dad na mengineyo kwa njia mbalimbali bila gharama yoyote online. Ukitaka nitarusha pdf moja hivi. Ukiisoma na kuifanyia kazi hutakuwa yuleyule tena.
 
Tuelimishe nasi maana mimi nimehudhuria makumi ya hizi semina za ujasiriamali wao wakikazania ununue DVD zao. Kuna jamaa alikuwa anatufundisha ujasiriamali basi baada ya mafunzo akasema tununue DVD yake kwa sh. 35,000. Basi kununua na kwenda kuiangalia nikakuta ni DVD ya movi inaitwa Police story ya Jackie Chan. Siendi tena hizi semina. Nimeku sms mkuu unipe hicho kitabu.
 
Pdf za kiyosaki zinauzwa babu. We unafanya piracy. Nyie ndo mnaorudisha nyuma wasanii
 
kila mtu anatangaza biashara yake. Huyu nae anataka apate hizo 15,000 wakati Robert Kiyosaki anatoa material kama vile Rich Dad poor Dad na mengineyo kwa njia mbalimbali bila gharama yoyote online. Ukitaka nitarusha pdf moja hivi. Ukiisoma na kuifanyia kazi hutakuwa yuleyule tena.

Hakuna material yoyote ya kiyosaki anayotoa bure. Nyie ndo mnao download vitu illegally. Sio kwamba kwa kuwa unaweza download kitu basi kimewekwa for free. Watu wametoa jasho halafu wewe una download. Utajiskiaje wewe kaz zako watu wakizidownload?
 
Wewe mkuu mwenye hii mada mbona hauna utofauti na hao waalimu uliowaponda, wewe mwenyewe unaonekana kiliza namba moja kuliko hata hao walimu wengine, nina mashaka na wewe hata huko Finland hukwenda kusoma wala nini, jipange upya mkuu
 
Tuelimishe nasi maana mimi nimehudhuria makumi ya hizi semina za ujasiriamali wao wakikazania ununue DVD zao. Kuna jamaa alikuwa anatufundisha ujasiriamali basi baada ya mafunzo akasema tununue DVD yake kwa sh. 35,000. Basi kununua na kwenda kuiangalia nikakuta ni DVD ya movi inaitwa Police story ya Jackie Chan. Siendi tena hizi semina. Nimeku sms mkuu unipe hicho kitabu.

Hahahaah, pole sana. Nimekupata mheshimiwa
 
Wewe mkuu mwenye hii mada mbona hauna utofauti na hao waalimu uliowaponda, wewe mwenyewe unaonekana kiliza namba moja kuliko hata hao walimu wengine, nina mashaka na wewe hata huko Finland hukwenda kusoma wala nini, jipange upya mkuu

Nashukuru kwa maoni yako. Ila nadhani una judge bila kuwa na uhakika na nadhani mara nyingi hiyo ni hofu waliyonayo watu wengi ambayo ni hofu ya mafanikio ambayo unaogopa. Inakutisha. Usiogope.
 
Wewe mkuu mwenye hii mada mbona hauna utofauti na hao waalimu uliowaponda, wewe mwenyewe unaonekana kiliza namba moja kuliko hata hao walimu wengine, nina mashaka na wewe hata huko Finland hukwenda kusoma wala nini, jipange upya mkuu

Halafu mzee unajua tunaishi katika nchi huru, kama huna nia ya kufanya kitu flani usikikashifu au kukiponda. Una uhuru uliopewa na serikali wa kuchagua njia nyingine. We chagua njia byingine itakayokupa mafanikio wala usichague yangu kama inakufanya uwe uncomfortable
 
kila mtu anatangaza biashara yake. Huyu nae anataka apate hizo 15,000 wakati Robert Kiyosaki anatoa material kama vile Rich Dad poor Dad na mengineyo kwa njia mbalimbali bila gharama yoyote online. Ukitaka nitarusha pdf moja hivi. Ukiisoma na kuifanyia kazi hutakuwa yuleyule tena.

Nirushie hiyo pdf mkuu,ingekuwa inauzwa wasingeweka link ya ku download.
Makoga55@gmail.com
Thnx
 
Mi naona kama vile bei yako ni fare ukizingatia zile gharama kubwa kubwa zinazochajiwa na hawa walimu wetu wa ujasiriamali. Naweza tembelea nione mradi wako wa kutengeneza mkaa wa kisasa? maana hapo juu umesema unatengeneza mkaa
 
Waweza ni PM mawasiliano yako
 
kila mtu anatangaza biashara yake. Huyu nae anataka apate hizo 15,000 wakati Robert Kiyosaki anatoa material kama vile Rich Dad poor Dad na mengineyo kwa njia mbalimbali bila gharama yoyote online. Ukitaka nitarusha pdf moja hivi. Ukiisoma na kuifanyia kazi hutakuwa yuleyule tena.

Naomba Io pdf ndg yang though jisanja@yahoo.com
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom