Paparazi Muwazi
JF-Expert Member
- Dec 23, 2007
- 310
- 79
Huu ndio wakati wetu wanahabari na wachambuzi kuanika siri zote tunazozifahamu wajumbe wateule wa tume ya katiba kwa sababu ikulu imesema Rais atawaapisha ijumaa.
Siri hizi zitawezesha usalama wa taifa kumshauri Rais kuacha kuwaapisha wajumbe wenye mashaka, pia makundi ambayo Rais amedai kuwa yameridhika na mapendekezo yataweza kuweka pingamizi pale ambapo mteule hajatokana na ridhaa yao.
Tusiangalie dini wala makabila ya watu walioteuliwa, tuangalie namna walivyoteuliwa iwapo walitokana na makubaliano ya makundi kweli ya wanaowakilisha na tuangalie pia kama kweli wana uwezo na msimamo wa kuhakikisha maoni ya wananchi ndiyo yanayowekwa badala ya mawazo ya watawala.
Kulipaswa kuwe na waliopendekezwa na vyama vya siasa, waliopendekezwa na vyama vya wafanyakazi, asasi za kiraia, taasisi za dini, vyama vya wanataaluma, sekta binafsi na makundi mengine muhimu katika taifa letu.
Weka jina la mjumbe unayemjua katika orodha na siri unazozifahamu kuhusu mjumbe huo. Haya tuanze sasa?
Mimi naanza na Mwenyekiti, ana sifa zote za kuwa mjumbe wa tume lakini sio mwenyekiti kwa kuwa alishawahi kuwa Mwenyekiti wa Tume ya rushwa lakini akakubali ripoti yake isitekelezwe na pia katika siku za karibuni amekuwa akitoa kauli za kikada kama mwanaCCM, Mwenyekiti wa tume hii alipaswa kuwa mtu neutral ingawa Mzee Warioba ana sifa za kuwa mjumbe.
PM