Siri kashfa ya EPA hadharani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siri kashfa ya EPA hadharani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Apr 10, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Apr 10, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  • Mnyika amwandikia barua Spika kutaka ufafanuzi

  WAKATI utata wa sh bilioni 135 zilizoibwa katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kupitia Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), unaendelea kuligubika taifa, imebainika kuwa serikali imeamua kulibeba deni hilo na kuliingiza katika deni la taifa. Chini ya utaratibu huo, serikali italilipa deni hilo kwa riba na hadi deni hilo litakapo iva, serikali italazimika kulipa sh bilioni 230 badala ya sh bilioni 137.7 zilizoibwa na wajanja.

  Hali hiyo imebainishwa katika taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) katika ripoti yake ya fedha za Serikali Kuu kwa mwaka ulioishia Juni 30 2009, fungu 22 kuhusu deni la taifa na matumizi mengine ya taifa.

  Kwa mujibu wa ripoti hiyo, serikali imebadilisha deni katika Akaunti ya Malipo ya Nje (EPA) la sh bilioni 137.7 kuwa dhamana ya serikali zitakazolipwa kwa riba ya kiwango cha sh bilioni 11.50 katika kipindi cha miaka 20 kilichopitishwa . Kwa hali hiyo, deni lote ambalo linapaswa kulipwa na serikali kwa riba litafikia sh bilioni 230, hivyo kulifanya taifa kubeba deni la EPA.


  Hatua hiyo ambayo inazidisha mzigo wa madeni kwa serikali, imemfanya Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, kumwandikia barua Spika wa Bunge, Anne Makinda akitaka ufafanuzi juu ya wizi wa EPA, kupitia Kampuni ya Kagoda.

  "Mheshimiwa Spika, haya yanafanyika bila Bunge lako kushirikishwa kwa ukamilifu ikiwemo kutaarifiwa makampuni ambayo yamerejesha fedha za EPA, kiasi kilichorejeshwa kwa kila kampuni na orodha ya makampuni ambayo hayajarejesha pamoja na wamiliki wake, mojawapo ya makampuni hayo ikiwa ni Kagoda," alisema Mnyika.


  Kabla ya kufikia uamuzi wa kulibeba deni hilo, serikali iliunda tume ya watu watatu kuchunguza na kubaini wezi wa fedha hizo na kuzirejesha bila kufikishwa mahakamani. Hata hivyo taarifa ya tume hiyo iliyoongozwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Said Mwema, imebaki kuwa siri, kwani haijulikani watuhumiwa gani wamerejesha, kiasi cha pesa kilichopatika na kiasi cha fedha kilichobaki mikononi mwa watuhumiwa wengine.


  Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima kuhusiana na hatua hiyo ya serikali kuingiza fedha za wizi wa EPA katika deni la taifa, ndio uliosababisha Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, kuuliza swali bungeni.

  Mnyika akiuliza swali la nyongeza juzi, alitaka kujua uchunguzi wa wizi wa fedha za EPA kupitia Kampuni ya Kagoda, umefikia wapi. Lakini wakati akijibu swali hilo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Mathias Chikawe, alijibu kwa kifupi sana kwamba serikali bado inaendelea na uchunguzi wa tuhuma dhidi ya kampuni hiyo.


  Hata hivyo uchunguzi zaidi uliofanywa na gazeti hili, umebaini kuwa Mnyika amemwandikia barua Spika wa Bunge, Anne Makinda, akieleza kutoridhishwa kwake na majibu ya Waziri Chikawe kuhusu uchunguzi juu ya Kampuni ya Kagoda ilivyohusika na wizi wa fedha za EPA.

  "Utakumbuka kwamba katika mkutano wa tatu wa Bunge, kikao cha kwanza, Aprili 5 mwaka huu, niliuliza swali la nyongeza kutokana na swali la msingi namba nne kwa Ofisi ya Rais (Utawala Bora).

  "Katika swali hilo nilihoji serikali itoe kauli kuhusu hatua zilizochukuliwa kuhusiana na Kampuni ya Kagoda Agricultural Limited na kukumbusha kwamba serikali imekuwa ikitoa ahadi za mara kwa mara bungeni kuwa uchunguzi unaendelea kwa kushirikiana na vyombo vya kimataifa. Niliuliza ni lini uchunguzi huo utakamilika? "Katika majibu yake, waziri alitoa jibu fupi kwamba uchunguzi bado unaendelea, bila kutoa majibu ya ukamilifu kama Kanuni za Kudumu za Bunge (Toleo la 2007) kifungu 46 (1), kinavyohitaji," alisema.


  Mnyika alisema kwa ajili hiyo, anaomba kuwasilisha maelezo yafuatayo bungeni kwa mujibu wa kanuni ya 50 na ya 28 ili kuitaka serikali kutoa majibu ya ukamilifu kwa kuwa miaka takriban mitatu imepita toka uchunguzi husika uanze. Ikumbukwe kwamba Kagoda inatuhumiwa kuchota jumla ya dola za Marekani 30,732,658.82 (sh 40 bilioni) katika Akanuti ya Madeni ya Nje (EPA), ndani ya BoT. Fedha hizi na nyingine zipatazo sh bil. 73 zilichotwa katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005.


  Serikali imekuwa ikitoa kauli za kujichanganya kuhusu ufisadi wa Kagoda. Mathalani Septemba 15, 2006, Waziri wa Fedha wakati huo, Zakia Meghji, aliwaandikia wakaguzi wa hesabu wa Kampuni ya Deloitte & Touche ya Afrika Kusini akisema, fedha za Kagoda zilitumika kwa "kazi za usalama wa taifa." Nyaraka mbalimbali, zinaonyesha kuwa cheti cha usajili wa Kagoda Na. 54040 kilichotolewa na Ofisi ya Wakala wa Usajili wa Leseni za Biashara na Makampuni (BRELA), kinaonyesha Kagoda ilisajiliwa Septemba 29, 2005 na waliohusika kuisajili wanatajwa kwa majina. Hadi sasa siri za ufisadi wa kampuni hiyo na kampuni nyingine zilizohusika na wizi wa fedha za EPA zimebaki kwa Rais Jakaya Kikwete, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema, Mkurugezi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Edward Hoseah na Johnson Mwanyika, ambao walikuwa wajumbe wa Kamati Maalumu ya Rais ya kufuatilia walioiba benki.  Tanzania Daima
   
 2. k

  kakini Senior Member

  #2
  Apr 10, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 197
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  haya mambo haya muda si mrefu Bongo kutanuka tene sio kidogo kutanuka mpaka watu watashangaa

  Rais wa burundi aliwahi kusema Bongo haina amani bali watu hawajui na ndo wanaanza kujua yaani sipati picha
   
 3. raybse

  raybse Senior Member

  #3
  Apr 10, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Days are very numbered here.....!!!
   
 4. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #4
  Apr 10, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,652
  Trophy Points: 280
  WACHA KINUKEEEE!!!
  WACHA WASHAAAAAAAAeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!
   
 5. k

  kayumba JF-Expert Member

  #5
  Apr 10, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 654
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hawa mpaka siku tukiwa na Katiba mpya itakayoondoa madaraka ya Rais tutawakamata wote hawa!
   
 6. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #6
  Apr 10, 2011
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Unajua Spika naye inawezekana alipata Mgao wa hayo Mabilioni ,naye si amepandikizwa na CCM na Mafisadi kwa kiinimacho cha kuweka spika Mwanamke? Tutarajie kusikia Majibu yake ya Mkato,nyodo na Mbwembwe kama ambavyo huwa anamjibu Tundu Lisu hasa utasikia ''kanuni..namba...ya Bunge inanipa mamlaka kama spika kuamua serikali ijibu au isijibu"....nk Spika Naye Kibaraka tu wa Mafisadi
   
 7. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #7
  Apr 10, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,132
  Trophy Points: 280
  Bongo inatia kichefuchefu
   
 8. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #8
  Apr 10, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Hadi sasa siri za ufisadi wa kampuni hiyo na kampuni nyingine zilizohusika na wizi wa fedha za EPA zimebaki kwa Rais Jakaya Kikwete, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema, Mkurugezi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Edward Hoseah na Johnson Mwanyika, ambao walikuwa wajumbe wa Kamati Maalumu ya Rais ya kufuatilia walioiba benki.

  Kwa hiyo waliunda kamati ya kufuatilia wizi ili majibu wabaki nayo wao? kwa hiyo wamekula pesa za vikao na majibu hawatoi, na wanaendelea kuchunguza nini wakati wezi wanajulikana, dr slaa si alisha watajia, au wanapotezea ili mwishowe tusahau haya bwana. wanjanja wao
   
 9. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #9
  Apr 10, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Murha mbuya! Nu umutulutumbi oree ghose ni iyake??
   
 10. muhosni

  muhosni JF-Expert Member

  #10
  Apr 10, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Chadema ongeza kasi, shindilia zaidi. Naona kama Chadema wanawachapa ccm makonde kushoto na kulia wakisindikiza na mateke nyuma huku wananchi wakizomea

  Je ccm wanaweza kujinasua?
   
 11. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #11
  Apr 10, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  siku ya ukombozi inakuja..
   
 12. f

  findu fiki JF-Expert Member

  #12
  Apr 10, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 431
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Siku za mwizi ni arobaini
   
 13. King junior

  King junior Member

  #13
  Apr 10, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ccm wameshazoea wizi hao, CDM kazeni buti mpaka 2watiririshe, wanajifanya wanajivua gamba huko Dodoma, hawajui kama kansa inakaa kwenye damu...? Mwisho wenu utafika tu, mtajificha kama mwenzenu wa Ivory Coast, Pambaf nyie, pesa zetu mnafanya mitaji...!
   
 14. Elinasi

  Elinasi Member

  #14
  Apr 10, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 64
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  taratibu tu,tunakaribia kufika,tuangalie tusijikwae tu
   
 15. Elinasi

  Elinasi Member

  #15
  Apr 10, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 64
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  sasa kama kamati ilipewa fedha kufanya uchunguzi na mwisho igome kutoa report hadharani huu si ufisadi mwingine huu?kulikuwa na haja gani ya kutangazia umma kumeundwa kamati ya kufatilia huo wizi?au ndio janja ya kufanya watu watulie na kusahamu madudu ya serekali yao?mwisho wa huu usanii ni lini jamani?na huyo aliepelekewa hiyo report kwann asije hadharani na kusomea wananchi matokeo??na kama uchunguzi unaendelea kwann pia wasitoe sehemu ya matokeo yaliyo tayari????
   
 16. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #16
  Apr 12, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  CCM inafikiri matatizo haya yaliyosababishwa na serikali ya ccm mojawapo ikiwa ni kashfa ya EPA itasuluhishwa kwa kupata wajumbe wapya wa kamati kuu nk
   
 17. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #17
  Oct 25, 2013
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Naona hatufiki na tumepotea njia
   
 18. M

  Mzee Wa Liverpool Senior Member

  #18
  Oct 25, 2013
  Joined: Jul 18, 2013
  Messages: 198
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Takukuru + Serikali ya CCM = Pigo na ufisadi uliokithiri Tanzania
   
Loading...