Siri iliyojificha muda ambao mtu anakaribia kufa na kuona mizimu, wachawi au inginevyo.

Secret Star

JF-Expert Member
Jul 1, 2011
1,568
2,000
Kwa kawaida Binadamu ana Mambo Mengi sana ndani yake, kiasi kwamba hadi sasa tunavyovijua ni vichache mno kuliko tusivyovijua.

Leo Nitawaleteeni Funzo fulani kuhusu saa za mwisho mtu anakaribia kufa. Kwa Mara nyingi Watu wengi wanapokaribia kufa huwa na hali tofauti na ya nyuma, kama vile Ucheshi kuongezeka

Kutabiri mambo, uwezo wa kuaga wenzao, kulalama kwamba wanaona jitu, watu, shetani, mizimu kuwa wanakuja kuwachukua na nyinginezo. Mara nyingi mambo haya huwatokea watu siku au masaa ya mwisho wanapokuwa wanakaribia kuuacha mwili (Kufa).

Siri iliyojificha nyuma ya mambo haya yote ni ''Jicho Latu'' au kwa jina jingine naweza nikakwambia kuwa ni ''jicho La Roho''
Kwa kawaida Kila mtu ana jicho la tatu ila ni binadamu wachache sana ambao huweza kulicontrol jicho hilo kwenye maisha yao ya kila siku.

Walio Wengi huishi kwa Macho haya haya mawili tunayoyajua ambayo kwenye ulimwengu wa Roho macho haya ni sawa na upofu tu.

Binadamu katika shughuli zake za kila siku hutawaliwa na Mwili, Roho ikiwa ndani yake, Hivyo siku au miezi kadhaa kabla ya mtu hajafa Roho huwa inaanza kuutawala Mwili Taratibu. Moja ya matokeo ya Roho kuutawala Mwili ni kufunguka kwa jicho la tatu bila Mtu mwenyewe kujua, Baadae ndipo kizaazaa huanza.

Mtu huyo hubadilika katika mambo kadhaa, huwa mchangamfu kuliko kawaida yake, Huweza hata kuaga wenzie bila yeye mwenyewe kujitambua. Ila Masaa machache mtu anapokaribia kufa hali ndiyo huwa mbaya zaidi kwani Roho huwa na nguvu kali zaidi kuushinda mwili kitu ambacho husababisha jicho lake la tatu kufunguka kwa kiasi kikubwa na hapo ndipo mtu huyo huanza kuona mambo mengi, huona maisha yake tangu anazaliwa hadi hapo alipo, huona maisha ya anaowaacha (Future) na baadhi ndo huutumia muda huo kutoa Wosia kwa ndugu anaowaacha maana huona live yanayokuja

Hizo ni faida lakini hasara ni mtu huyo kuona mapichapicha (Ndoto) hasa kama hakuwa imara katika Ulimwengu wa kiroho, kwenye Maisha yake. Jicho la tatu huwasumbua sana watu ambao walikuwa Hawana mazoezi ya ulimwengu wa roho katika maisha yao maana muda wa mwisho huona mauzauza mengi, lakini kiuhalisia ni sawa na ndoto tu.

Na hilo hutokea pale mtu anapokuwa anahangaika kuicontrol Pumzi, maana dakika za mwisho Pumzi hutoka kama inavutwa Na kitu. hivyo wakati anahangaika kuivuta pumzi irudi Ndani huanza kujenga dhana kuwa yawezekana kuna kitu kipo pale kinavuta pumzi yake, Na Jicho latu huitikia dhana hiyo na kuleta taswira halisi kinachowazwa na mtu huyo.

Jicho la tatu huwa na tabia ya kuonyesha mambo yaliyojificha pia, hivyo kama mtu huyo atakuwa karogwa Jicho la tatu huweza kumuonyesha mtu huyo taswira ya yule mbaya wake mbele yake, hapo kwa mtu huyo huhisi kuvutwa pumzi na pumzi yake hupungua taratibu hadi mtu huyo anaposhindwa kabisa kumudu kuendelea kuvuta pumzi na hatimaye kufa.
 

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 31, 2016
8,592
2,000
Ukiwa katika process ya mwili kushut down huwa hivii.
Kama una madhambi mengi basi utakuwa ukijutia hivyo kufanya roho kwenda mbio mbio na ndipo hata maumivu ya kifo yataongezeka
Ila ukiwa unakufa na huku una moyo mwepesi hutapata taabu utakwenda ukiwa ume relax kwenye state nyingine
 

Loftins

JF-Expert Member
Oct 1, 2017
8,322
2,000
have you ever died?? if no then where is this experience coming from?? or you have just decided to write down your illusions.
Nimelifikiri hili pia, nadhani huyu jamaa kapata uwezo wa kuandika haya kutokana na story mbalimbali anazozisikia kwa wafiwa kuwa alianza kuwa hivi mara vile
 

mulwanaka

JF-Expert Member
Feb 19, 2017
4,179
2,000
I was about to ask the guy such a question.
What i know is a dead man tells no tell.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna kitu kinaitwa 'near to death exprience' niwale walio kalibia kufa ila hawakufa walipoteza fahamu ila baadaye zinarudi....ila tatizo kubwa kwao nikwamba ubongo hauwezi kufanya kazi vizuri kwasababu mtu akifa ubongo ndo unaanza kuoza kwanza, wakirudi duniani hawawezi kuishi sanaa au kusimulia yote walio exprience, mie personally na Imani kwamba ata Yesu alipata 'near to death exprience' ndomaana hakuweza kuishi tena zaidi sana Mtu akifa hawezi kurudi kama binaadamu, ata kwa Yesu ni Imani tu, to keep us with hope ila hawezi kurudi wala tarehe ya kurudi hawaitaji kwasabb wata umbuka bure

Sent using Jamii Forums mobile app
 

logframe

JF-Expert Member
Aug 19, 2014
3,784
2,000
Kuna kitu kinaitwa 'near to death exprience' niwale walio kalibia kufa ila hawakufa walipoteza fahamu ila baadaye zinarudi....ila tatizo kubwa kwao nikwamba ubongo hauwezi kufanya kazi vizuri kwasababu mtu akifa ubongo ndo unaanza kuuza kwanza, wakirudi duniani hawawezi kuishi sanaa au kusimulia yote walio exprience, mie personally na Imani kwamba are Yesu alipatikana na 'near to death exprience' ndomaana hakuweza kuishi tena zaidi sana Mtu akifa hawezi kurudi kama binaadamu, ata kurudi kwa Yesu ni Imani to keep us with hope ila hawezi kurudi wala tarehe ya kurudi hawaitaji kwasabb wata umbuka bure

Sent using Jamii Forums mobile app
Ulianza vizuri, ila umekosea kuingiza masuala ya Imani.


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom