Siri 5 ambazo wanazijua matajiri tu, masikini hawazijui

Royal Warrior

JF-Expert Member
Nov 19, 2015
1,166
2,143
Habari zenu ladies & gentlemen,

Leo nimekutana na article moja nzuri sana kutoka kwa billionea mmoja kutoka huko majuu na ningependa nishee (share) na nyie maskini wenzangu huenda ikatusaidia kutufumbua macho na kupiga hatua mbele walau na sie tupate usingizi wa amani, maana unalala huku kichwa bado kipo ON kinapiga mahesabu + stress za madeni.

Ok ngoja nisiwachoshe, namwaga mtama, mutanishukuru baadae mukishatajirika.

1. Kwanza kabisa usichukue mikopo ovyo.

2. Tengeneza vyanzo mbalimbali vya kujiingiza mapato. Kamwe usitegemee chanzo kimoja cha mapato hata kama kinakutosheleza mahitaji yako.

3. Tumia kiasi kidogo kuliko kile unachao ingiza, na kinachobaki wekeza. (Spend less than you make, and invest the rest)

4. Fikiria namna ya kuwekeza kile ulichosevu na sio kufikiria namna ya kukitumia.

Na mwisho kabisa ni kwamba
5. Huhitaji kuwa na utajiri mkubwa sana ku enjoy maisha, tafuta utajiri utao kutosheleza kukupa financial freedom baada ya hapo wekeza pesa zako zikufanyie kazi.

A rich man makes money with his hands, a richer man has his employees make money for him, and the richest has his money make money for him.
 
karibu, kila la kheri.
Unapokuwa na vyanzo vingi hii mimi naiona kuwa sio nzuri! utashindwa kusimamia kwa ufanisi hivyo vyanzo! nafikiri unapokuwa na chanzo kimoja. ukatuliza akili! ukafanya kwa ufanisi! mambo yatabadarika. ni mtazamo wangu.
 
Back
Top Bottom