Sirari: Wananchi wakusanyika kituo cha Polisi baada ya Polisi kudaiwa kumuua mdogo wake John Heche, Suguta Chacha

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,896
Wananchi wa Kata ya Sirari Jimbo la Tarime vijijini amekusanyika katika kituo cha polisi cha Sirari, Baada ya Jeshi la polisi kudaiwa Kumuua Mdogo wa Mbunge wa Tarime vijijini Mhe. John Heche akiwa chini ya ulinzi, anaejulikana kwa jina la Suguta Chacha.



heche1.jpg
heche2.jpg
heche4.jpg

---

UPDATES..

Mbunge John Heche ameithibitishia JamiiForums kutokea kwa tukio hili..

Ameeleza kuwa;

1. Tukio ni la kweli

2. Kijana Suguta Chacha ameuawa kwa kuchomwa kisu na Polisi waliomkamata jana usiku akiwa Bar.

3. Polisi walijaribu kumtupa baada ya kumuua lakini eneo hilo kulikuwa na mlinzi ambaye aliwafukuza hivyo ikashindikana na kuwalazimu kumpeleka Mochwari.

-------------- Jeshi la Polisi lathibitisha askari wake kuhusika----------------​

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Polisi Tarime Rorya Henry Mwaibambe amethibitisha kuuawa kwa Bwana Chacha Heche Suguta ambaye ni mdogo wa Mbunge wa Tarime Vijijini John Heche, kwa kuchomwa kisu na Polisi.

“Tukio ni la kweli limetokea na huyo askari tunamshikilia, huyo kijana alikamatwa usiku sasa wakati wapo kwenye gari wakielekea kituo cha polisi, ukatokea mzozo kati ya huyu askari na huyu marehemu, mzozo kama wanataka kupigana, mwenzake akaingilia kuamua, lakini ni kweli askari amemjeruhi huyu mgongoni, mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi leo saa 6 mbele ya ndugu zake, kweli umekutwa na jeraha la hicho kisu mgongoni na mtuhumiwa alikuwa hajavalishwa pingu, ila hatujui nini waliambiana mpaka kufikia hivyo”, amesema Kamanda Mwaibambe.

Pia Kamanda Mwaibambe amewataka watu kutochukulia tukio hilo kisiasa, isipokuwa ni kama tukio lingine la mauaji, ingawa sio jambo zuri kwa mtu yeyote.
 
Haya ndio matukiio AMBAYO CHADEMA MTAANZA KUTENGENEZA KAMA PLAN C ya kupambana na SERIKALI baada ya maandamano kushindikana kwa mara ya pili....
Huyu mleta habari anajaribu kutengeneza STORI kuwa kubwa kumhusisha HECHE kwenye hili.....ETI MDOGO WAKE HECHE...kwa hiyo akiwa mdogo wake ndio inakuwaaaje???
KAMA KAINGIA KWENYE KUMI NA 18 za polisi kijinga kijinga acha APATE HAKI YAKE....
Afu sijui kwanini unapenda kuleta HABARI ZA UPANDE MMOJA TU.....
CHADEMA NYIE HAMTAKI KABSA KUONA NCHI HII IKITAWALIKA NA KUWA NA AMANI
 
Waliamshe bhana kabla hawajakusanyika police wengi wakane marehemu hakufia kituoni alikufa akiwa njiani kupelekwa hospital
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom