Mangi Mlay
JF-Expert Member
- Dec 18, 2016
- 5,743
- 7,106
Wahindi wametuibia, na wanatuibia bado sasa mtu anataka tuwape heshima
HahahhHivi wewe unaishi sayari ya WAPI? Kifo cha Kanumba hukusikia hizi habari zikisemwa? Ulikuwa hujazaliwa? Swali gani unauliza hilo wakati mitaani kila mmoja anajua Freemason lazima utoe kafara TENA ndugu wa Karibu!! Sasa watu woote hao wawe waongo?
Wewe acha upumbavue wa kutetea masuala ya kishetani hapa!. Pumbaveu sana!
Akili za kiTanzania hizi haswahuyu mzee ndiye aliyemfanya mkapa awatoe kafara watanzania kwenye mv bukoba na ajali ya treni dodoma pia ndiye aliyempa uanachama kikwete akawatoa kafara wazenji kwenye mv spice.
NB: Ukitaka kumuua paka mpe jina baya,nimemaliza
![]()
Nakushauri tafuta kitabu hiki soma ,acha kashfa na usipende kusoma udaku ukiambiwa thibitisha ushetani huo utatoa ,kwanza nini maana ya ushetaji
...
![]()
Ideology ya Freemason ni kukuweka huru kifikra na kuthink big ,na their motto ni integrity ,generocity ,humility and kindness ,kama ushetani ni kindness basi sawa
Na Freemason unaingia ukiwa na dini either Christianity or Islam ,kwahyo usichanganye joh
Hapa ndipo umepotea mkuu. Free mason is a faith. Christianity is a faith that shall never be bound with any other faith. Huwezi kuwa na Imani ya Kristo halafu ukawa na imani ya freemason au islam, halafu ukabaki kuwa Mkristo.
Utakuwa kwenye dimbwi kubwa la confusion.
In order to become a Freemason, it is necessary to meet these requirements:
Hapa ndipo umepotea mkuu. Free mason is a faith. Christianity is a faith that shall never be bound with any other faith. Huwezi kuwa na Imani ya Kristo halafu ukawa na imani ya freemason au islam, halafu ukabaki kuwa Mkristo.
Utakuwa kwenye dimbwi kubwa la confusion.
ahaaa aiseee malaika subiri kushuka naomba usizime jfhuyu mzee ndiye aliyemfanya mkapa awatoe kafara watanzania kwenye mv bukoba na ajali ya treni dodoma pia ndiye aliyempa uanachama kikwete akawatoa kafara wazenji kwenye mv spice.
NB: Ukitaka kumuua paka mpe jina baya,nimemaliza
Hivi shetani yupoje? Anafananaje?Freemason ni dini ya kishetani ukweli utabaki hivyo tu tusipindishe pindishe maneno wandugu kila MTU atavuna alichopandaaa yangu ni hayo tu
Duh..!huyu mzee ndiye aliyemfanya mkapa awatoe kafara watanzania kwenye mv bukoba na ajali ya treni dodoma pia ndiye aliyempa uanachama kikwete akawatoa kafara wazenji kwenye mv spice.
NB: Ukitaka kumuua paka mpe jina baya,nimemaliza
Naomba uniambie sababu kubwa ya kuwachukia hawa jamaa kiasi hichi? Lakini tambua hata animal ana haki ya kuishi jamani!Duh.....
Na hapo unajiona unajua sana kuhusu hiyo freemason,eti kisa watu walisema, seriously unajikuta mjuaji kisa tu mtu alisema? Kukaa kimya napo ni busara sio kujikuta wajua kila kitu.Hivi wewe unaishi sayari ya WAPI? Kifo cha Kanumba hukusikia hizi habari zikisemwa? Ulikuwa hujazaliwa? Swali gani unauliza hilo wakati mitaani kila mmoja anajua Freemason lazima utoe kafara TENA ndugu wa Karibu!! Sasa watu woote hao wawe waongo?
Kwa niaba ya mafreemason wewe toa pole, sisi wengine tunasema Mungu na ampe hukumu inayomstahiri huyo marehemu. Na mwisho, tunaomba Mungu awape adhabu wanaofanya maasi kama hawa mafreemasonsJAYANTILAL Keshavji Chandelier (Sir Andy Chande), amefariki dunia wiki iliyopita. Kwa vyovyote vile, na kwa sababu yoyote, huu ni msiba mkubwa kitaifa.
Huyu ni mtu ambaye alikubali kulitumikia taifa hata baada ya mali za familia yake kuwa zimetaifishwa na serikali. Huyu ni mtu ambaye alisaidia katika ujenzi wa mashirika yote makubwa ya umma yaliyopo nchini hivi sasa.
Iwe Shirika la Reli, Mamlaka ya Bandari, Shirika la Umeme na karibu kila taasisi muhimu ya kiuchumi hapa kwetu. Kuna wakati, alikuwa mjumbe katika bodi takribani 20 za mashirika mbalimbali ya umma.
Sir Andy Chande tayari alikuwa mfanyabiashara mkubwa katika wakati ambapo nchi yetu haikuwa na watu wa kutosha wa kada hiyo. Kwa vyovyote vile, ana mchango mkubwa kuliko hata wale ambao tunadhani wana mchango mkubwa zaidi.
Lakini mzalendo huyu amefariki dunia wiki iliyopita na jambo la kushtua ni kwamba ni watu wawili tu mashuhuri; Benjamin Mkapa na Zitto Kabwe, ndiyo ambao wametoa hadharani salamu zao za rambirambi kwa familia yake.
Nimeelewa kuhusu rambirambi alizotuma Mkapa kwa sababu yeye alikuwa ni rafiki binafsi. Hata angekuwa hajawahi kuwa Rais mstaafu, bado angetafuta namna ya kuwasilisha salama zake hizo.
Lakini nimeshtushwa na ukimya wa serikali. Hadi wakati naandika makala hii, Jumatatu, saa saba mchana, hakuna salamu zozote za rambirambi kutoka Ofisi ya Rais, Makamu au Waziri Mkuu kuhusu msiba huu mkubwa kwa taifa letu.
Ni serikali hiihii ambayo imekuwa ikitoa taarifa kwa umma kuhusu misiba yote iliyotokea katika siku za karibuni. Walipokufa wanasiasa wa zamani, wanamuziki, watumishi waandamizi wa serikali na watu wengine maarufu, serikali ilitoa salamu zake za pole hadharani kupitia vyombo vya habari.
Hata kama leo akifa Mkuu wa Mkoa au Mkuu wa Wilaya, sina shaka kwamba Ikulu itatoa salamu za pole kwa familia ya marehemu siku hiyohiyo ambayo tukio limetokea.
Lakini, haikuwa hivyo kwa Sir Andy Chande ambaye inaelezwa msiba wake utahudhuriwa na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi yetu.
Hali hii inanirudisha katika mada ambayo nimeizungumza mara nyingi katika safu yangu hii; kwamba wakati mwingine kwa makusudi au bahati mbaya, tunashindwa kuenzi mchango wa watu wenye rangi tofauti na wengi wetu.
Nina imani kwamba kama Chande angekuwa mweusi kama mimi, huenda taarifa ingetoka mapema maana hakuna namna nyingine ya kuelezea upungufu. Nadhani kuna ile hali ya kusema “huyu si mwenzetu”.
Mkasa wa mzee Chande unanikumbusha ule wa mzee mwenzake, Ameenullah Kashmir, ambaye aliondolewa jeshini yeye na aliyekuwa Mkuu wa Majeshi, Mirisho Sarakikya, kwenda kutumika serikalini.
Miaka 30 baadaye, Sarakikya akastaafishwa rasmi jeshini kwa kupewa cheo cha Jenerali anachostahili. Kashmiri, mwenye asili ya Kihindi, ambaye alikuwa wa pili kwa cheo baada ya Sarakikya, anasota hadi leo kupewa heshima hiyo.
Kustaafishwa rasmi kwa Sarakikya kunamaanisha kwamba atapata stahiki zake zote kama mstaafu mwenye hadhi ya Jenerali. Ni haki ambayo Kashmiri pia anatakiwa kuipata.
Tofauti pekee ni kwamba, Kashmiri wala hahitaji chochote. Anachohitaji, kama askari, ni kustaafishwa na kuagwa rasmi na jeshi ambalo ameshiriki kulitengeneza. Nimeambiwa kwamba ameandika barua kadhaa kuomba hilo na baadhi ya barua hazijajibiwa hadi leo. Narudia, hata kujibiwa barua ni shida!
Tunaweza kudhani kwamba haya ni mambo madogo lakini si madogo namna hiyo. Kuna watu wanayatazama na bila shaka wanajenga mtazamo kuhusu taifa letu.
Vitendo kama hivi, vinatoa picha kwamba taifa letu linazingwa na aina fulani ya ubaguzi ambao hauonekani kwa macho ya kawaida. Ni ubaguzi ambao taratibu unamea pasi na wengi kuona.
Kwa mfano, badala ya Chande kujulikana kwa mema yake, hivi sasa anafahamika zaidi kwa wadhifa wake katika jamii ya Free Masons. Ukweli mchungu ni kwamba, zaidi ya nusu ya Watanzania wana mawazo tofauti kuhusu jamii hiyo. Hakuna heshima yoyotem kwa hapa nchini, wakati mtu anapofahamika kama mwanachama au kiongozi wa Free Masons.
Hakuna anayekumbuka mchango wa Sir Andy kwenye ujenzi wa Shule ya Viziwi ya Buguruni wala Sekondari ya Shaaban Robert. Hakuna anayetaka kusema ni wawekezaji wangapi au biashara ngapi zimefanikishwa kwa sababu ya ushawishi wake.
Lakini watajuaje umahiri wa Sir Andy Chande wakati hata serikali haisemi jambo lolote la kheri kumhusu?
Source: Raia Mwema.