Sir Chande kaondoka, hata pole?

Sir Chande kaondoka, hata pole?

Hivi wewe unaishi sayari ya WAPI? Kifo cha Kanumba hukusikia hizi habari zikisemwa? Ulikuwa hujazaliwa? Swali gani unauliza hilo wakati mitaani kila mmoja anajua Freemason lazima utoe kafara TENA ndugu wa Karibu!! Sasa watu woote hao wawe waongo?
Kumbe ni story za mtaaani

Zitakuumiza kichwa achana nazo
 
Katengwa kwa sababu ya imani Yake ya Ufremasoni na si kwa sababu zingine. Viongozi hawawezi kushiriki hata hayo mazishi wala kutuma salami wanahofia kuwa watabatizwa na kuitwa ni wafuasi wa Freemason. UBAYA wa imani hii ya Freemason imejikita katika kutoa kafara watu. Sasa unapokwenda kushiriki hata kama sio imani YAKO HALAFU huku nyuma akafa ndugu YAKO wa karibu jamii itakuchukuliaje? Itaacha kuamini wewe ndo umemtoa kafara? TATIZO IMANI YENYEWE IMEJIKITA KATIKA KUTOA KAFARA. HAPO NDO KWENYE TATIZO. SASA KIONGOZI AKIJIWEKA KIMBELE MBELE RAIA WATAMSEMA KUWA NI MIONGONI MWA FREMASON NA RAIA WATAMUOGOPA ILI ASIJE WATOA WAO KAFARA!!MFANO wewe uwe na Rafiki ambae kaamua kuwa Freemason Hivi utaendelea kuwa na ukaribu nae huku ukijua IPO Simu atakutoa kafara?
Mkuu serikali haina dini na Freemason ni dini pia hata kama hawakwenda wangetoa official salamu za rambirambi kutoka eidha serikalini au ikulu moja kwa moja ili kuepuka watu kuielewa vibaya serikali yetu.
 
Mbona husemi alikuwa blood sucker? Unajua hizo mali ziligharimu mapipa mangapi ya damu za watu? Unawezaje kusema alisaidie mashirika bila kuangalia misaada hiyo ilimnufaishaje yeye? Je kama alikuwa akitoa kafara?

Mtu yeyote mchawi hapashwi kuishi na zaidi sana kusifiwa! PERIOD!
Siamini katika uzushi.
Unaweza kuweka mifano yenye uthibitisho juu u-blood sucker wake?
 
Kiukweli swala la kumlilia devil worshiper haliniingii akilini ukweli unauma hamna namna
 
JAYANTILAL Keshavji Chandelier (Sir Andy Chande), amefariki dunia wiki iliyopita. Kwa vyovyote vile, na kwa sababu yoyote, huu ni msiba mkubwa kitaifa.

Huyu ni mtu ambaye alikubali kulitumikia taifa hata baada ya mali za familia yake kuwa zimetaifishwa na serikali. Huyu ni mtu ambaye alisaidia katika ujenzi wa mashirika yote makubwa ya umma yaliyopo nchini hivi sasa.

Iwe Shirika la Reli, Mamlaka ya Bandari, Shirika la Umeme na karibu kila taasisi muhimu ya kiuchumi hapa kwetu. Kuna wakati, alikuwa mjumbe katika bodi takribani 20 za mashirika mbalimbali ya umma.

Sir Andy Chande tayari alikuwa mfanyabiashara mkubwa katika wakati ambapo nchi yetu haikuwa na watu wa kutosha wa kada hiyo. Kwa vyovyote vile, ana mchango mkubwa kuliko hata wale ambao tunadhani wana mchango mkubwa zaidi.

Lakini mzalendo huyu amefariki dunia wiki iliyopita na jambo la kushtua ni kwamba ni watu wawili tu mashuhuri; Benjamin Mkapa na Zitto Kabwe, ndiyo ambao wametoa hadharani salamu zao za rambirambi kwa familia yake.

Nimeelewa kuhusu rambirambi alizotuma Mkapa kwa sababu yeye alikuwa ni rafiki binafsi. Hata angekuwa hajawahi kuwa Rais mstaafu, bado angetafuta namna ya kuwasilisha salama zake hizo.

Lakini nimeshtushwa na ukimya wa serikali. Hadi wakati naandika makala hii, Jumatatu, saa saba mchana, hakuna salamu zozote za rambirambi kutoka Ofisi ya Rais, Makamu au Waziri Mkuu kuhusu msiba huu mkubwa kwa taifa letu.

Ni serikali hiihii ambayo imekuwa ikitoa taarifa kwa umma kuhusu misiba yote iliyotokea katika siku za karibuni. Walipokufa wanasiasa wa zamani, wanamuziki, watumishi waandamizi wa serikali na watu wengine maarufu, serikali ilitoa salamu zake za pole hadharani kupitia vyombo vya habari.

Hata kama leo akifa Mkuu wa Mkoa au Mkuu wa Wilaya, sina shaka kwamba Ikulu itatoa salamu za pole kwa familia ya marehemu siku hiyohiyo ambayo tukio limetokea.

Lakini, haikuwa hivyo kwa Sir Andy Chande ambaye inaelezwa msiba wake utahudhuriwa na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi yetu.

Hali hii inanirudisha katika mada ambayo nimeizungumza mara nyingi katika safu yangu hii; kwamba wakati mwingine kwa makusudi au bahati mbaya, tunashindwa kuenzi mchango wa watu wenye rangi tofauti na wengi wetu.

Nina imani kwamba kama Chande angekuwa mweusi kama mimi, huenda taarifa ingetoka mapema maana hakuna namna nyingine ya kuelezea upungufu. Nadhani kuna ile hali ya kusema “huyu si mwenzetu”.

Mkasa wa mzee Chande unanikumbusha ule wa mzee mwenzake, Ameenullah Kashmir, ambaye aliondolewa jeshini yeye na aliyekuwa Mkuu wa Majeshi, Mirisho Sarakikya, kwenda kutumika serikalini.

Miaka 30 baadaye, Sarakikya akastaafishwa rasmi jeshini kwa kupewa cheo cha Jenerali anachostahili. Kashmiri, mwenye asili ya Kihindi, ambaye alikuwa wa pili kwa cheo baada ya Sarakikya, anasota hadi leo kupewa heshima hiyo.

Kustaafishwa rasmi kwa Sarakikya kunamaanisha kwamba atapata stahiki zake zote kama mstaafu mwenye hadhi ya Jenerali. Ni haki ambayo Kashmiri pia anatakiwa kuipata.

Tofauti pekee ni kwamba, Kashmiri wala hahitaji chochote. Anachohitaji, kama askari, ni kustaafishwa na kuagwa rasmi na jeshi ambalo ameshiriki kulitengeneza. Nimeambiwa kwamba ameandika barua kadhaa kuomba hilo na baadhi ya barua hazijajibiwa hadi leo. Narudia, hata kujibiwa barua ni shida!

Tunaweza kudhani kwamba haya ni mambo madogo lakini si madogo namna hiyo. Kuna watu wanayatazama na bila shaka wanajenga mtazamo kuhusu taifa letu.

Vitendo kama hivi, vinatoa picha kwamba taifa letu linazingwa na aina fulani ya ubaguzi ambao hauonekani kwa macho ya kawaida. Ni ubaguzi ambao taratibu unamea pasi na wengi kuona.

Kwa mfano, badala ya Chande kujulikana kwa mema yake, hivi sasa anafahamika zaidi kwa wadhifa wake katika jamii ya Free Masons. Ukweli mchungu ni kwamba, zaidi ya nusu ya Watanzania wana mawazo tofauti kuhusu jamii hiyo. Hakuna heshima yoyotem kwa hapa nchini, wakati mtu anapofahamika kama mwanachama au kiongozi wa Free Masons.

Hakuna anayekumbuka mchango wa Sir Andy kwenye ujenzi wa Shule ya Viziwi ya Buguruni wala Sekondari ya Shaaban Robert. Hakuna anayetaka kusema ni wawekezaji wangapi au biashara ngapi zimefanikishwa kwa sababu ya ushawishi wake.

Lakini watajuaje umahiri wa Sir Andy Chande wakati hata serikali haisemi jambo lolote la kheri kumhusu?

Source: Raia Mwema.
Ahsante umeeleweka
 
Mbona husemi alikuwa blood sucker? Unajua hizo mali ziligharimu mapipa mangapi ya damu za watu? Unawezaje kusema alisaidie mashirika bila kuangalia misaada hiyo ilimnufaishaje yeye? Je kama alikuwa akitoa kafara?

Hayo mashirika uliyoyataja yamestabilize kwa kiwango gani kwa msaada wa freemason? Unaweza kuona namna kila siku yanazidi kuyumba na ukaona msaada wa kuyategemeza siyo huo uliokuwa unatolewa pengine kwa masharti ya free mason? Vitu vingine vinakuja kwa rangi za yeboyebo kuhadaa watu lakini in a real sense ndio mkono wa uharibifu kutoka kwa shetani. Usikimbilie kupokea na kufurhia kila uanchopewa. Vingine ni ndoana za mashetani.

Mtu yeyote mchawi hapashwi kuishi na zaidi sana kusifiwa! PERIOD!
Nani kakuambia Freemason ni uchawi ,unaweza kutoa uthibitisho au ndio nimesikia nimesikia ,speculations tu
 
Siamini katika uzushi.
Unaweza kuweka mifano yenye uthibitisho juu u-blood sucker wake?

Nenda kajiunge na freemason upate first hand experiences. Unauliza mauaji kwa osama? Unatafuta ubichi kwenye mvua? Utakwenda kanisa la katoliki ukose kupig magoti kwenye misalaba? Utakwenda kuswali misikitini useme hukusujudia hadi nchi? Namna gani wewe!
 
Nani kakuambia Freemason ni uchawi ,unaweza kutoa uthibitisho au ndio nimesikia nimesikia ,speculations tu

Ok. Narekebisha basi napaka rangi yake halisi. Ni USHETANI!. Nali alikuambia shetani ana karama njema?
 
Hivi wewe unaishi sayari ya WAPI? Kifo cha Kanumba hukusikia hizi habari zikisemwa? Ulikuwa hujazaliwa? Swali gani unauliza hilo wakati mitaani kila mmoja anajua Freemason lazima utoe kafara TENA ndugu wa Karibu!! Sasa watu woote hao wawe waongo?
Nimesikia nimesikia je uthibitisho upo ?

Mbona mitaani kuna stori za nguva ,popobawa ,je wapo

Sio kila stori mitaani bila uthibitisho mnayaweka kichwani ,uzushi nikiuweka leo mitaani utasambaa

Je uthibitisho upo
 
Tangu lini nchi yetu imesajili dini zinazotoa kafara za watu?!!!!
 
Nimesema jamii ya Watanzania wengi ndo wanaamini hivyo kuwa Fremasoni ni kafara, TENA wanaenda mbali zaidi kuwa lazima utoe ndugu YAKO wa Katibu TENA yule umpendaye, Wazazi,Kaka au Dada n.k pia wanasema hata ajali zinazotokea barabarani wanaamini ni kazi ya fremasoni, Pia wanaamini kuwa matajiri na viongozi wengi wa kisiasa na Dino ni wafuasi wa Freemason. Huo NDIYO mtazamo wa Watanzania walio wengi juu ya imani hiyo. Sasa kumtoa kwenye Mawazo ya kutoamini kuwa Fremasoni hawatoi kafara sio rahisi kiasi hicho. Tazama video ya kijana mmoja anamzungumzia Kanumba kuwa ALIKUWA Fremasoni. na yeye alifanikiwa kutoka.
 
Nenda kajiunge na freemason upate first hand experiences. Unauliza mauaji kwa osama? Unatafuta ubichi kwenye mvua? Utakwenda kanisa la katoliki ukose kupig magoti kwenye misalaba? Utakwenda kuswali misikitini useme hukusujudia hadi nchi? Namna gani wewe!
Ulishawahi kujiunga ukapata first hand experience?
 
Kiukweli swala la kumlilia devil worshiper haliniingii akilini ukweli unauma hamna namna
100% ya binadamu wa leo ni devil worshiper in one way or another, hakuna anayefanya vile MUNGU anataka kwa asilimia mia moja. "MCHENI MWENYEZI MUNGU UKWELI WA KUMCHA" tofauti na hapo unaabudu aliyekuwa anaabudiwa na bwana Chande
 
Ok. Narekebisha basi napaka rangi yake halisi. Ni USHETANI!. Nali alikuambia shetani ana karama njema?
Kafara zipi ziliwahi kushuhudiwa

Freemason wanasingiziwa mengi na wengi wamepokea udaku nimesikia nimesikia ,

Freemason ni mahsusi kumuweka mtu huru kifikra na kwa kila kitu

Mtu awe huru kwa nyanja zote ,kama kuna utoaji kafara basi malengo ya Freemason yanakosewa ..

Msipende kuchafua
 
Daah nmeskitishwa sana kwa hili..huyu jamaa n legend kibongo na hta nje lakn ukmya wa Tz kwny msba wake nomaa..wakat maelfu wanatumia miundombinj alyoihangaikia kuitengeneza..
Mambo km haya yanakatsha tamaa km ya uyo mjeda mwngn3
 
Mkuu tupo tunaokumbuka na kuthamini mchango wa marehemu, sir Andy alijitahidi sana kueleza kuhusu freemasonry na mpaka leo clips za interviews zake zipo YouTube ila watanzania wameamua kuamini uzushi na speculations, hawajiulizi imekuwaje mazishi yake yamefuata taratibu zote za imani ya kihindu?
 
huyu mzee ndiye aliyemfanya mkapa awatoe kafara watanzania kwenye mv bukoba na ajali ya treni dodoma pia ndiye aliyempa uanachama kikwete akawatoa kafara wazenji kwenye mv spice.

NB: Ukitaka kumuua paka mpe jina baya,nimemaliza
 
Kihere here tu, yeye kapumzika zake we unaanza uchonganishi hayakuhusu kwani kuhuzuria msiba au kutoa lambilambi ni lazima? Acheni uchonganishi
 
Mjibu mpumbavue sawa sawa na upumbaue wake ili ajidharau mwenyewe. Usimjibu mpumbavue sawa na upumbavue wake usije ukafanana naye. Pumbavue wewe usinipotezee muda. Kam ahata mifano nimekpa huwezi kutafuta kuelewa, sina muda wa kuajdil kitu na wewe. Sina muda katika upumbavue! Nenda kwa atu wa kiwango chako.
Umepanick hoja zimekimbia.
Swali moja umeandika mistari zaidi ya saba.

Makamo ya mjadala yanatofautiana
 
Umepanick hoja zimekimbia.
Swali moja umeandika mistari zaidi ya saba.

Makamo ya mjadala yanatofautiana

Usinilazimishe niwaze kama uanvowaza wewe. Wewe ni mpumbavue kwa sababu humji hata Mungu. Mimi namjua Mungu na nafahamu tofauti yake na shetani. Kwako wewe bora liende. Huna hadhi ya kujadili na mimi haya mambo. Please endelea na upumbavu wako.
 
Back
Top Bottom