platozoom
JF-Expert Member
- Jan 24, 2012
- 9,405
- 11,284
JAYANTILAL Keshavji Chandelier (Sir Andy Chande), amefariki dunia wiki iliyopita. Kwa vyovyote vile, na kwa sababu yoyote, huu ni msiba mkubwa kitaifa.
Huyu ni mtu ambaye alikubali kulitumikia taifa hata baada ya mali za familia yake kuwa zimetaifishwa na serikali. Huyu ni mtu ambaye alisaidia katika ujenzi wa mashirika yote makubwa ya umma yaliyopo nchini hivi sasa.
Iwe Shirika la Reli, Mamlaka ya Bandari, Shirika la Umeme na karibu kila taasisi muhimu ya kiuchumi hapa kwetu. Kuna wakati, alikuwa mjumbe katika bodi takribani 20 za mashirika mbalimbali ya umma.
Sir Andy Chande tayari alikuwa mfanyabiashara mkubwa katika wakati ambapo nchi yetu haikuwa na watu wa kutosha wa kada hiyo. Kwa vyovyote vile, ana mchango mkubwa kuliko hata wale ambao tunadhani wana mchango mkubwa zaidi.
Lakini mzalendo huyu amefariki dunia wiki iliyopita na jambo la kushtua ni kwamba ni watu wawili tu mashuhuri; Benjamin Mkapa na Zitto Kabwe, ndiyo ambao wametoa hadharani salamu zao za rambirambi kwa familia yake.
Nimeelewa kuhusu rambirambi alizotuma Mkapa kwa sababu yeye alikuwa ni rafiki binafsi. Hata angekuwa hajawahi kuwa Rais mstaafu, bado angetafuta namna ya kuwasilisha salama zake hizo.
Lakini nimeshtushwa na ukimya wa serikali. Hadi wakati naandika makala hii, Jumatatu, saa saba mchana, hakuna salamu zozote za rambirambi kutoka Ofisi ya Rais, Makamu au Waziri Mkuu kuhusu msiba huu mkubwa kwa taifa letu.
Ni serikali hiihii ambayo imekuwa ikitoa taarifa kwa umma kuhusu misiba yote iliyotokea katika siku za karibuni. Walipokufa wanasiasa wa zamani, wanamuziki, watumishi waandamizi wa serikali na watu wengine maarufu, serikali ilitoa salamu zake za pole hadharani kupitia vyombo vya habari.
Hata kama leo akifa Mkuu wa Mkoa au Mkuu wa Wilaya, sina shaka kwamba Ikulu itatoa salamu za pole kwa familia ya marehemu siku hiyohiyo ambayo tukio limetokea.
Lakini, haikuwa hivyo kwa Sir Andy Chande ambaye inaelezwa msiba wake utahudhuriwa na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi yetu.
Hali hii inanirudisha katika mada ambayo nimeizungumza mara nyingi katika safu yangu hii; kwamba wakati mwingine kwa makusudi au bahati mbaya, tunashindwa kuenzi mchango wa watu wenye rangi tofauti na wengi wetu.
Nina imani kwamba kama Chande angekuwa mweusi kama mimi, huenda taarifa ingetoka mapema maana hakuna namna nyingine ya kuelezea upungufu. Nadhani kuna ile hali ya kusema “huyu si mwenzetu”.
Mkasa wa mzee Chande unanikumbusha ule wa mzee mwenzake, Ameenullah Kashmir, ambaye aliondolewa jeshini yeye na aliyekuwa Mkuu wa Majeshi, Mirisho Sarakikya, kwenda kutumika serikalini.
Miaka 30 baadaye, Sarakikya akastaafishwa rasmi jeshini kwa kupewa cheo cha Jenerali anachostahili. Kashmiri, mwenye asili ya Kihindi, ambaye alikuwa wa pili kwa cheo baada ya Sarakikya, anasota hadi leo kupewa heshima hiyo.
Kustaafishwa rasmi kwa Sarakikya kunamaanisha kwamba atapata stahiki zake zote kama mstaafu mwenye hadhi ya Jenerali. Ni haki ambayo Kashmiri pia anatakiwa kuipata.
Tofauti pekee ni kwamba, Kashmiri wala hahitaji chochote. Anachohitaji, kama askari, ni kustaafishwa na kuagwa rasmi na jeshi ambalo ameshiriki kulitengeneza. Nimeambiwa kwamba ameandika barua kadhaa kuomba hilo na baadhi ya barua hazijajibiwa hadi leo. Narudia, hata kujibiwa barua ni shida!
Tunaweza kudhani kwamba haya ni mambo madogo lakini si madogo namna hiyo. Kuna watu wanayatazama na bila shaka wanajenga mtazamo kuhusu taifa letu.
Vitendo kama hivi, vinatoa picha kwamba taifa letu linazingwa na aina fulani ya ubaguzi ambao hauonekani kwa macho ya kawaida. Ni ubaguzi ambao taratibu unamea pasi na wengi kuona.
Kwa mfano, badala ya Chande kujulikana kwa mema yake, hivi sasa anafahamika zaidi kwa wadhifa wake katika jamii ya Free Masons. Ukweli mchungu ni kwamba, zaidi ya nusu ya Watanzania wana mawazo tofauti kuhusu jamii hiyo. Hakuna heshima yoyotem kwa hapa nchini, wakati mtu anapofahamika kama mwanachama au kiongozi wa Free Masons.
Hakuna anayekumbuka mchango wa Sir Andy kwenye ujenzi wa Shule ya Viziwi ya Buguruni wala Sekondari ya Shaaban Robert. Hakuna anayetaka kusema ni wawekezaji wangapi au biashara ngapi zimefanikishwa kwa sababu ya ushawishi wake.
Lakini watajuaje umahiri wa Sir Andy Chande wakati hata serikali haisemi jambo lolote la kheri kumhusu?
Source: Raia Mwema.