Sipendi unavyoongea na mimi

Sipendi unavyoongea na mimi

hesbone

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2014
Posts
239
Reaction score
568
SIPENDI NAMNA UNAVYOONGEA NA MIMI...
"Una matatzo gani wewe? Sikukwambia mimi ufue shati langu la blue? Yaani kila siku wewe ni kusahau tu" akamkoromea mkewe.
Mke akatazama pembeni.
"Samahani, nilisahau kabisa kama kuna shati la kufua". Mke akaongea huku akimpa mumewe tai nyekundu.
Mume akapokea kwa kuikwapua huku akionekana dhahiri kukasirika.
"Sipendi namna unavyoongea na mimi" mke akamwambia mumewe.
"Unamaamisha nini? Zungumza ueleweke wewe mwanamke. Sina muda hapa, nachelewa ofisini kwangu". Mume akafoka.
Mke akakaa kitandani na kusema, "nenda tu kazini mume wangu".
Mume akashusha pumzi na kukaa kitandani karibu na mkewe.
"Nini kinakusumbua mke wangu?" Mume akamuuliza kwa upole kidogo.
"Hivi mim ni mke wako kweli?" Mke akauliza.
"Unawezaje kuniuliza hivyo? Umeanza lini upumbavu?" Mume akafoka tena.
Mke akamtazama tu mumewe huku akiwa kimya.
"Hiyo ndio sababu. Hebu angalia namna unavyoongea na mimi" mke akaongea zaidi.
"Kimsingi hauongei na mimi bali unaniamrisha. Unanikaripia, unanipa oda utafikiri meja wa jeshi kwa kuruta. Tokea lini wewe umekua bosi wangu? Wewe ni mume wangu na wala sio mkuu wangu...
...Nakusikia ukiyatumia maneno kama vile 'samahani', 'tafadhali' na 'pole' kwa wafanyakazi wenzako; lakini kwangu sikumbuki ni lini uliyatamka hayo maneno. Je kuwa mke wako ndio inamaanisha mimi ni mtumwa na nastahili kuhudumiwa hovyo hovyo na mume wangu?"
Mke akatazama chini na kuendelea..
"Unaniabisha mbele za watoto na majirani, unaninyanyasa na kunipa amri utafikiri mtoto wa sekondari. Mimi ni mwanamke wako, mke wako, nijali basi kama msaidizi wako. Ona hua huniangalii hata machoni unapoongea na mimi. Je natia kinyaa hata sistahili kuangaliwa usoni?
...Unao muda na marafiki zako kila siku lakini kwangu huna muda, muda ulio nao kwangu ni pale unapotaka tendo la ndoa tu..na hapo ukimaliza hujali kama mimi nimeridhika ama laa unageuka upande wa pili..hakuna maongezi, hakuna mapenzi..najichukia kwa kweli!
Mke akamtazama vizuri mumewe...Na kuendelea..
"Unapotaka kunipa kitu hunipi mkononi, unanitupia kama mbwa. Ukiangusha kitu mimi ndio wa kukiokota huku wewe ukiwa umekaa umeweka miguu juu ya meza...
...Tukiwa tunaenda mahala hautaki kutembea karibu na mimi, natembea nyuma yako, je sina thamani ya kutembea na wewe? Umejaza rekodi na kumbukumbu ya mapungufu yangu na kila siku unayakumbushia, kwaio mimi sina zuri hata moja?
...Yuko wapi mwanaume aliekua ananijali, ananisikiliza na kunipenda? Je amefariki baada tu ya kuingia kwenye ndoa? Bado nahitaji huduma yako nzuri mume wangu, haswa wakati huu tukiwa na watoto. Onesha kunihitaji nami nitakupa mambo matamu tutakayoyafurahia sote kwa pamoja hata kwenye tendo la ndoa.
...Niite majina matamu kama zamani, usiniite 'mwanamke' sijali sana kuhusu kukuhudumia ila nahitaji heshima. Nahitaji unifanye nijisikie ni mpenzi wako. Nikubali, kuwa mpole kwangu, ukali wako unaniogopesha kuliko hata nilivyokua namuogopa baba yangu. Mimi sio housegirl. Ni mke wako ndani ya nyumba hii.
Mke akashusha pumzi na akamtazama mumewe baada ya kuongea yote ya moyoni mwake...mume hakuongea kitu.
Mume akachukua simu yake na kupiga baadhi ya namba.
Pamoja na kumueleza yote hayo lakini bado amempotezea na kuchukua simu yake..Mke akajisikia vibaya sana.
Mke akasimama ili aondoke huku machozi yakimtoka, lakini mume akamshika mkono na kumrudisha kitandani huku akisikiliza simu aliyopiga.
Mume akaanza kuongea, "Hallo, tafadhali ahirisha kikao tufanye kesho, nimepata dharuka kidogo. Kuna jambo la kifamilia nashughurika nalo". Akakata simu.
Mume akamuona mkewe akitabasamu. Akamkumbatia mkewe na kumbusu mdomoni.
"Nisamehe mpenzi wangu, sikua nafahamu kama nakuumiza. Je nikupe offer ya kukutoa lunch leo? Kuanzia leo na kuendelea, nitakuhudumua vizuri kama vile unavyotamani. Mumeo nimerudi sasa !!!
Mwanamke jifunze kuongea kwa upole endapo kuna jambo haulifurahii na linakuumiza juu ya mwenzako, ni nadra sana kwa mwanaume kuwa mgumu kwa mwanamke anaenyenyekea.
My wisdom, "Happy is the man who finds a true friend, and far happier is he who finds that true friend in his wife"
 
Mwanamke anaijenga nyumban yake kwa mikono yake Bali mpumbavu huibomoa/!!!
 
Ingawa ya kutunga but it makes sense kuliko wale kila siku wanaleta stori za vibamia.... punyeto ....
 
Hongera zake huyo mama kwa kujiamulia kufunguka ambapo mwisho wa siku mume kabadika pasi kutarajia.

Funzo zuri sana kwa wanaume. Hebu tupendeni jamaani na inatakiwa mjue sisi ndio mapambo yenu na walezi wenu pia.
 
Hali imebadilika kila kitu ni vururu vururu, tutajitahidi na asante
 
Hongera zake huyo mama kwa kujiamulia kufunguka ambapo mwisho wa siku mume kabadika pasi kutarajia.

Funzo zuri sana kwa wanaume. Hebu tupendeni jamaani na inatakiwa mjue sisi ndio mapambo yenu na walezi wenu pia.

umeongea kwa hisia hadi nimeogopa
 
umeongea kwa hisia hadi nimeogopa
Usiogope mkuu inatakiwa mtupende wanawake ili na sisi tujisikie kwamba uwepo wetu una faida katika maisha yenu.

Na ukiangalia huyo mama amevumilia mengi hadi kuamua kufunguka si kazi ndogo mkuu.
 
  • Thanks
Reactions: 30P
Sasa unakutana na kimbembe yan ukimuuzi jiandae kumziba mdomo mana mpk memory ijae ndo atanyamaza
 
Back
Top Bottom