Sipati Picha Uhuru Kenyatta amfunge Raila Odinga then Afanye ziara Kisumu

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Mar 11, 2020
2,704
6,499
Sipati Picha Mfano Uhuru Kenyatta wa Kenya amfunge Jela Raila Odinga then Uhuru afanye Ziara kule Kisumu au eneo la Nyanza.

Kenya wana utamaduni ambao uko nchi nyingi isipokuwa Tanzania, Utamaduni wa Kila eneo kulianda kiongozi wao.

Tuwe wakweli hata Marekani kwenye Demokrasia ya kubwa Huwa yale maeneo waliko zaliwa wagombe Uraisi hasa wa vyama vya Democratic na Republican huwa wanaungwa mkono kwa asilimia 100

Kenya Mfano kule Eldoreti kwao William Ruto kule ni No go zone kwa viongozi wengine, Kisumu kule Raila Odinga ni sehemu ambayo wanaweza kumriwaza.

Mfano Raila Odinga afungwe Jela then kiongozi afanye Ziara kule Kisumu huo moto unaweza zimwa na vikosi vya UN.

Huku Tanzania tunashindwa kabisa ku pay lasr respect kwa Watoto wetu, Mfano Zitto anapaswa kupewa Heshimu kule Kigoma kwa sababu ni Mtoto wao. Au Makamu Wa Raisi anapaswa kupewa heshima kubwa kule kwao Kigoma pia.

Mbowe anapaswa kupewa heshima kubwa kule Kilimanjaro kwa sababu ni mtoto wao. Waziri Mkuu Majariwa anapaswa kupewa heshima ya kipekee kule Lindi kwao.

Eneo au ukanda anako tokea Kiongozi huwa ni eneo la mwisho la kumpa matumaini, au kumlinda na kadhalika.

Tanzania unashangaa Lipumba ana dhihakiwa kule kijijini kwao, au Mrema ana dhihakiwa Kijijini kwao au Zitto ana dhihakiwa kijijini kwao au Mbowe au kiongozi yoyote yule.

Ifike wakati Maeneo wanako toka viongozi yawe ni maeneo ya mwisho ya kuwapa viongozi hao matumaini haijalishi ni kiongozi kutoka Upinzani au tawala.

Moshi kule wanapaswa kuwa ndio sehemu ya Mwisho ya kumliwaza Mbowe.

Sehemu nyingi za Dunia hata nchi zenye Democrasia ya kutisha huwa wale viongozi wana kwao na kule kwao ndio huwa sehemu ya kumliwaza.
 
Haya mambo ya kwao na kwetu siyaelewi..., Hata kama yapo dunia nzima na Tanzania hayapo basi wao inabidi watuige kwa kuendelea....

Mimi kama Mtanzania kwetu ni Tanzania wala sihitaji passport kwenda popote na ninaweza kuhamia popote pale (Na hili la Umoja wa Kitaifa ndio lililobaki ninalojivunia kama Mtanzania) Tafadhali na hili msilinyakue
 
Hatari yake ni kwamba itafika mahali uwezi kumove on kwenda sehemu nyingine ikiwa jamii yako au kabila lako limewahi kumshambuliaa mtu wao huu Ni ukabila mbaya sana sana.

Na ndicho kinawateza Kenya ukabila mkuu futa uzi wako kwa amani

Mimi mwaka Jana nilikuwa Morogoro Tena mjini pale nilienda kucheki gari yangu iliyo haribika wakati natafuta fundi nikampata mluguru walivyo jua mimi Ni mmasai walichukia sana kisa Ni kwamba wanasema wamasai wana roho mbaya sna na wakatili.

Niliwashangaa sana. Nikawambiwa Hawa wamasai siyo wa Arusha Ni wakitanga hawakunielewa waliniona mtu mkatili. Hakika hadi leo gari haijapona sijui mimi ila ukabila Ni mbaya sana ndugu zangu
 
Nimekaa Kenya na Kushiriki Chaguzi zao Mbili Live front line Hicho kitu HAKIWEZEKANI braza, yaani hata RAO aka Baba hata kuwekwa rumande Kenya au mahabusu haiwezekani na hakuna kituo cha polisi au mahakama inaweza accomodate kesi ya Odinga Kenya.
sasa kweli unaweza mlinganisha RAO na huyu muhuni wa siasa aliye gerezani?!!
 
Mhalifu anapewaje heshima?!
tuache kuingilia kazi ya mahakama.

mhalifu hastahili heshima ndio maana analala gerezani sio nyumbani, maana sehemu sahihi kwa mhalifu yeyote yule ni gerezani.
Mbona wewe umesha ingilia kazi ya mahakama?
 
Mhalifu anapewaje heshima?!
tuache kuingilia kazi ya mahakama.

mhalifu hastahili heshima ndio maana analala gerezani sio nyumbani, maana sehemu sahihi kwa mhalifu yeyote yule ni gerezani.
Mahakama haijawahi kumshitaki Mbowe. Acheni kujificha nyuma ya mahakama.
 
Sipati Picha Mfano Uhuru Kenyata wa Kenya amfunge Jera Raila Odinga then Uhuru afanye Ziara kule Kisumu au eneo la Nyanza.

Kenya wana utamaduni ambao uko nchi nyingi isipo kuwa Tanzania, Utamaduni wa Kila eneo kulianda kiongozi wao...
Huo ndio unaoitwa ukabila na ukanda ambao kwa Tanzania upo kwenye mioyo ya watanzania ila kwa nje ni kama haupo hata hivya faida zake ni chache kuliko hasara.
 
Tamasha halijaandaliwa na wachaga tumeshaambiwa. Ni kikundi cha CCM kimejikusanya kikajiita wachaga for the interest best known to them. Na bila shaka kulikuwa na pecuniary handouts kwa waliojumuika ili ionekane ni shughuli ya wachaga kweli kumbe fake. CCM mlikofika mtakuja kuchinja wanenu kwa drama zenu za ajabu.
 
Umeanza vzr lakkn ulipofika mbele ukaharibu andiko lako, kwa Mtu mwenye kufikiri weweee ndy umeonekana ni mjinga zaidi kuliko mleta mada ".Nimeelewa neno moja tu."Fairlier ".
Roho ya kihalifu tangu lini ikajitambua zaidi ya kuwaza uhalifu.

Chadema siku zote rafiki yenu ni yule anayewaza kama nyinyi.

Na hiyo huwa ni hulka ya ki nyumbu.

Mmoja akirukia mtoni basi wengine wooote hapo hapo.
Bila hata kujihakikishia usalama wao.
Matokeo ni baadhi kusombwa na kasi ya maji mtoni.
Na wengine huishia vinywani mwa mamba.

Piteni na uovu wenu.
 
Sipati Picha Mfano Uhuru Kenyata wa Kenya amfunge Jera Raila Odinga then Uhuru afanye Ziara kule Kisumu au eneo la Nyanza.

Kenya wana utamaduni ambao uko nchi nyingi isipo kuwa Tanzania, Utamaduni wa Kila eneo kulianda kiongozi wao...
Kenya si wanakatiba bora kabsia kuwahi kutungwa Africa sasa kenyatta atamfungaji udinga ili hali kuna separation of power

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom