Sipati picha, naomba Wachumi mniaaidie

ong'wafaza

JF-Expert Member
Apr 30, 2012
243
100
Hivi huwa najiuliza;inawezekana ikafika mahala watu wote wakawa sawa kiuchumi?

Maana yangu ni kwamba, je kuna uwezekano wa wananchi wote kuwa Matajiri (bila kuwepo maskni wa kipato) na maisha yakaendelea?
Lakini vilevile je, kuna uwezekano kwa wananchi wote kuwa maskini wa kipato (bila kuwepo na matajiri) na maisha pia yakaendelea?

Tuchukue mifano michache ya kuona ni nini kitatokea kiuchumi endapo wananchi wote watakuwa maskini wa kipato.
Hali ikiwa hivyo dereva wa bodaboda ataendesha nini ilihali wote hawana uwezo wa kumiliki bodaboda?

Mpiga debe stand atapiga debe gani ilihali hakuna mwenye uwezo wa kununua gari,achilia mbali uwezo wa kulipanda.

Lakini pia, kama wote tungekuwa matajiri, ni nani angepanda hayo mabasi na bodaboda ilihali kila mtu ana usafiri wake?

Ni nani angepanga nyumba ya mtu ilihali kila mmoja ana nyumba yake?
Ni nani angeenda kufanya kazi shambani au ofisini kwa mtu ilihali kila mtu anajimudu kiuchumi?

Kifupi mimi nadhani makundi haya mawili ni mhimu kuwepo katika jamii kwa kuwa yanategemeana kwa namna moja au nyingine.

Au Wachumi mnasemaje?
 
Hayo makundi mawili ya utajiri na umasikini yanamantiki katika nchi za africa lakini kwa nchi za wenzetu wakiwa matajili wote kazi ngumu na za hovyo zinafanyaga mashine au wanaagiza mabeki tatu na mashamba boy kutoja nchi za giza
 
Back
Top Bottom