Sioni ubaya kwa serikali kuelekeza baadhi ya fedha za maafa kwenye taasisi nyingine za kiserikali

Uzuri mjiletea laana wenyewe, huko mbele hata madawati sijui mwenge sijui nini hampati kamwe, tumeshawajua, tunachanga halafu mnagawia wabunge 10m kila mmoja, kweli?
Hujawai kuchanga hata senti tano lakini maneno mengii. Kama unabisha lete ushahidi.
 
Uzuri mjiletea laana wenyewe, huko mbele hata madawati sijui mwenge sijui nini hampati kamwe, tumeshawajua, tunachanga halafu mnagawia wabunge 10m kila mmoja, kweli?
Mkuu wangu mchango uliotolewa na wananchi wa kawaida haufiki 5%, kiasi kikubwa kilitolewa na nchi za nje na wafanyabiashara wakubwa na mataasisi makubwa...hawa wana mtazamo mpana zaidi ya kuwanunulia waathirika Maharage na Mchele. Iacheni serikali ilete maendeleo ya pamoja sio upendeleo wa kimaeneo.
 
Mkuu ulichokisema hapa ni sahihi kabsa....Hata mimi jana nilileta uzi humu ndani juu ya hili swala....nikawauliza Wenye ushaidi wa matumizi ya sivyo ndivyo juu ya hizi pesa walete ushaidi hapa nilikuwa na maana ya kwamba si kweli HIZI pesa zimetumika nje ya mkoa husika ama nje ya lengo husika...PESA ZOTE ZINAELEKEZWA HUKO KAGERA kwa ajili ya kuboresha miundo mbinu na huduma muhimu..na IKIWEZEKANA kuanzisha HUDUMA nyingne ambazo ni muhimu LAKINI SI kuwajengea WAHANGA nyumba...Hapa kinachotakiwa kuangalia kwa jicho la ziada ni MAKUNDI MAALUMU ndio yapewe kipaumbele juu ya MAKAZI yao LAKINI SI WAHANGA WOTE au jambo la muhimu kabsa ni kuiomba serikali kuondoa kodi kwenye VIFAA VYA UJENZI ili bei iwe nafuu kwa hawa WAHANGA.....sasa hawa WENZETU wa UPIMNZANI UCHWARA wao ndio wamepata PAKUTOKEA JUU YA HILI maana NI WATU WA MATUKIO KWELI SIKU HIZI......TUSISHANGAE KESHO WAKAHIMIZA MAANDAMANO NCHI NZIMA kupitia hili....
Mkuu serikali haikupaswa kutumia zole pesa hata senti mpaka wahakikishe wale wanaoishi kwenye mahema wamepata walau chumba kimoja cha kulala ili hata mvua ikinyesha wasitaabike sana,

Lakini bado watu wanalala kwenye mahema na serikali inaenda kujenga miundo binu mengine. Waliotoa hizo pesa hawakutoa kwa ajili ya matumizi ya serikali bali kwa ajili ya wananchi wasiojiweza kwa sababu jambo limetokea ghafla la kwenye utawala huu kujenga nyumba sio masihara mkuu.

Serikali ilishasema tetemeko hawakulileta wao kwa wanchi wananchi wasiilalamikie serikali ndio maana wale wenye huruma na watanzani wenzo ndio wakaamua kjitolea kile kidogo walichonacho ili kuwasitiri hawa wanyonge wasio na uwezo wa kujenga tena.Ndio maana hata kwenye nyuma za ibada tumepitishiwa hili bakuli la kuchangia hawa wahanga kwa huruma zetu tukajitolea.

Na serikali kama ilikuwa haina haina uwezo wa kuboresha miundo mbinu yake ambayo imepata hitilifu baada ya kukumbwa na lile tetemeko ilibidi na wao waombe wachangiwe kama watu wanavyotoa kwenye michango ya mbio za mwenge lakini sio kwa ubabe huu uliotumika ,

Siungi mkonyoo hoja hata kidogo.
 
Hivi tusingechanga ina maana serikali isingejenga hayo mamiundombinu yake?
Mkuu Takwimu zinaonyesha kuwa michango ya mtu mmoja mmoja si mikubwa kuliko ile ya wahisani, Taasisi na wafanyabiashara wakubwa...Hawa hawaamini katika kuwajaza mapesa waathirika bali kuboresha miundombinu na hudukwa kwa waathirika na jamii yote kwa ujumla...Tuache ubinafsi pesa ile haikuchangwa kwa waathirika wa tetemeko pekee bali kwenye mfuko wa maafa wa Taifa zima.
 
Mimi nakuunga mkono mtoa mada ya kwamba KAMA..... On a hilo neno "KAMA" lkn kinachofanyika nikuwa hakuna walichosaidiwa waathirika isipokua walipewa biskuit. Je mleta mada hiyo ni haki kweli? Watu walichanga kwa ajili ya matatizo ya watu binadsi si kwa ajili ya matatizo ya serikali! Kwa hiyo wangeshughulika na matatizo ya watu kwanza, na baadae waombe msaada kwa kwa ajili ya serikali kushughulikia miundobinu.
 
wakuu tusiwe watu wa kutwist mambo,hata mungu hapendi kabisa.
serikali ya uk kupitia kwa balozi wake hapa nchini ilitoa bilion sita,kwa ajili ya yale maafa.
wafanya biashara walipoitwa ikulu kuiunga mkono serikali katika swala hili ,wapo walio walio changia mifuko mingi tu ya sementi akiwemo mzee lowasa,wapo wafanya biashara waliojitolea kujenga zile shule zilizo bomoka nk.
msd wamepeleka tani za kutosha za madawa,kenya wametoa magodoro na mabasi si haba,mseveni ametupa hard cash in term of dollars .
nashangaa waratibu wa lile zoezi wanasema wanapeleka pesa kwenye miundombinu ya serikali,miundombinu ipi wakati kuna watu walijitolea kujenga hiyo miundombinu,wengine wakatoa na cement,au hizo pesa ndio garama za mafundi?
jamani tumuogope mungu,mungu hapendi kabisa mnyonge kunyayasika,watu walitoa baada ya kuwaona wale wazee wakilala nje,wakishinda njaa ndio .
 
Mkuu Takwimu zinaonyesha kuwa michango ya mtu mmoja mmoja si mikubwa kuliko ile ya wahisani, Taasisi na wafanyabiashara wakubwa...Hawa hawaamini katika kuwajaza mapesa waathirika bali kuboresha miundombinu na hudukwa kwa waathirika na jamii yote kwa ujumla...Tuache ubinafsi pesa ile haikuchangwa kwa waathirika wa tetemeko pekee bali kwenye mfuko wa maafa wa Taifa zima.


Huu utetezi wako ungekuwa wakili mahakamani walahi mteja wako ni kifungo tu kwa hakimu.
 
Kwani lengo lilikuwa ni kiasi gani?? Kwa hiyo mnatumia kiasi kilichozidi kwenye makusanyo au makusanyo yote?
 
Km lengo ni kujenga miundo mbinu. Kwann mlitumia picha za wahanga wa tetemeko? Mgetumia picha za miundo mbinu basi. Huu ni wizi uliotukuka.
FISADI HAACHI ASILI YAKE, mbona TRA wanakusanya kodi kuvuka malengo, hizo pesa zinaenda wapi?
 
Nianze tu kwa kuwapa pole wahanga wa tetemeko la KAGERA, mpate nguvu za kusimama na kuendelea na shughuli nyingine za ujenzi wa Taifa.

Nije kwenye mada, Kumekuwepo na wachangiaji wengi kwenye mitandao ya kijamii, na vyombo vingine wakiponda msimamo wa serikali kuelekeza pesa za Maafa ya kagera kwenye shughuli nyengine za kiserikali, binafsi kwa maoni yangu ni kuwa sioni ubaya kwa serikali kuelekeza pesa kwenye shughuli nyingine za maendeleo kwa sababu zifuatazo.

Kwanza watu watambue kwamba lengo kuu la pesa zile ni kuyarejesha maisha ya waathirika katika hali zao za kawaida kama ilivyokuwa kabla ya kukumbwa na shida ile, Mfano yule aliyebomokea na nyumba kuijenga, aliyeharibilkiwa mazao shambani kumuwezesha kama mbegu na pembejeo, aliye patwa na msiba ni kumliwaza kwa kuwa nae na michango midogo midogo, si lengo la michango ile kuwatajirisha wahanga au kuwajaza mapesa ...HAPANA. Si lengo la michango ile kuifanya kagera kuwa DUBAI...HAPANA.

Kwa Mtazamo wangu, ikiwa lengo hili limekamilika, pesa inaweza kuelekezwa sehemu nyingine yoyote ikiwemo kuboresha maeneo mengine yenye hatari ya kukumbwa na jaga kama lile, au eneo lolote lenye manufaa ya ujumla kwa jamii.

Kwa muktadha huu basi, ikiwa pesa zilizochangwa zimevuka lengo kuu la awali la kurejesha maisha ya waathirika katika hali yao ya kawaida sioni ubaya kwa ziada ya pesa zile kuelekezwa kuboresha miundombinu mingine ya serikali ambayo itakuwa ni kwa faida ya jamii yote kwa ujumla wakiwemo waathirika wa tetemeko.

Kitendo chochote cha kutaka kutafunwa pesa zote na wana kagera nakichukulia kama ni kitendo cha ubinafsi na ukosefu wa uzalendo.

Tusijenge tabia ya kupinga kila kitu jamani.

Nitoe lawama zangu kwa wasaidizi wa JPM kwa kuacha upotoshaji huu kunawiri.

Kwa hili nipo pamoja na JPM.

Asante

Tume ya katiba
(Mtaalamu wa mifumo ya komputer na Mtakwimu anayeishi UHAMISHONI.)
mwizi ni mwizi tu,

Hao CCM kuanzia Mwenyekiti wao , Katibu mkuu na wengineo wote ni majambazi tu
 
Ondoa upuuzi hapa,ile pesa ni haki yao,hawajapewa na serikali bali wamechangiwa na watu,sasa haipaswi kuwapangia matumizi.hata kama ni kuwatajirisha haina shida kwa sababu ni pesa iliyochangwa kwa sababu yao na wala haijatolewa na serikali,
 
Au ni kweli serikali haina kitu
 

Attachments

  • 1479117498560.jpg
    1479117498560.jpg
    41.9 KB · Views: 25
Ondoa upuuzi hapa,ile pesa ni haki yao,hawajapewa na serikali bali wamechangiwa na watu,sasa haipaswi kuwapangia matumizi.hata kama ni kuwatajirisha haina shida kwa sababu ni pesa iliyochangwa kwa sababu yao na wala haijatolewa na serikali,
Pesa imechangwa kwenye KAPU KUU LA MAAFA LA TAIFA....Kwa nini mmekuwa wagumu kuelewa?
 
Pesa imechangwa kwenye KAPU KUU LA MAAFA LA TAIFA....Kwa nini mmekuwa wagumu kuelewa?
Kwa hiyo kabla ya hapo hilo kapu likikuwa empty? Maana kusubiri michango ndio usaidie wahanga ina maana hilo kapu halikuwa na kitu kabla.sasa ikitokea tatizo jingine serikali itasubiri tena michango? Maana sasa zinazosalia mnapeleka kwenye taasisi za umma,na je kwani hizo taasisi hazina wizara husika? Bajeti ya wizara zake inafanya nini kama mambo yenyewe ndio haya ya kutumia pesa za pole?usijitoe ufahamu mkuu,kwa hili serikali imechemka sana
 
Kwanza watu watambue kwamba lengo kuu la pesa zile ni kuyarejesha maisha ya waathirika katika hali zao za kawaida kama ilivyokuwa kabla ya kukumbwa na shida ile....

Kwa Mtazamo wangu, ikiwa lengo hili limekamilika...

Ewe Mtanzania mwenzangu, kabla hujatoa utetezi kwa Mh. Raisi na serikali yake ungesema wazi hapa "kwa mtazamo wako" lengo limekamilika au lah ndio tujadili utetezi.
 
Hii issue imekuwa handled vibaya na serikali toka mwanzo. Zinahitajika busara ili wananchi waelewe vyema lengo la serikali kwao. Ukitaka utawale bila pressure kubwa ya umma ni kuwaelewesha wananchi vizuri na kwa lugha nyepesi malengo ya serikali. Nyerere alipata fursa ya kupambana na external pressure sababu aliweza kuwafanya wananchi wamuelewe kila hatua anayopanga kufanya ndio maana makaburu, wareno n.k walimshindwa. Si vyema ku assume kila mtu anapaswa kujua na kuelewa.
Yaani ni kama unatamani kutetea ila unaona aibu flan hivi:D:D:D
 
Back
Top Bottom