Tume ya Katiba
JF-Expert Member
- Apr 6, 2012
- 4,896
- 1,862
Nianze tu kwa kuwapa pole wahanga wa tetemeko la KAGERA, mpate nguvu za kusimama na kuendelea na shughuli nyingine za ujenzi wa Taifa.
Nije kwenye mada, Kumekuwepo na wachangiaji wengi kwenye mitandao ya kijamii, na vyombo vingine wakiponda msimamo wa serikali kuelekeza pesa za Maafa ya kagera kwenye shughuli nyengine za kiserikali, binafsi kwa maoni yangu ni kuwa sioni ubaya kwa serikali kuelekeza pesa kwenye shughuli nyingine za maendeleo kwa sababu zifuatazo.
Kwanza watu watambue kwamba lengo kuu la pesa zile ni kuyarejesha maisha ya waathirika katika hali zao za kawaida kama ilivyokuwa kabla ya kukumbwa na shida ile, Mfano yule aliyebomokea na nyumba kuijenga, aliyeharibilkiwa mazao shambani kumuwezesha kama mbegu na pembejeo, aliye patwa na msiba ni kumliwaza kwa kuwa nae na michango midogo midogo, si lengo la michango ile kuwatajirisha wahanga au kuwajaza mapesa ...HAPANA. Si lengo la michango ile kuifanya kagera kuwa DUBAI...HAPANA.
Kwa Mtazamo wangu, ikiwa lengo hili limekamilika, pesa inaweza kuelekezwa sehemu nyingine yoyote ikiwemo kuboresha maeneo mengine yenye hatari ya kukumbwa na jaga kama lile, au eneo lolote lenye manufaa ya ujumla kwa jamii.
Kwa muktadha huu basi, ikiwa pesa zilizochangwa zimevuka lengo kuu la awali la kurejesha maisha ya waathirika katika hali yao ya kawaida sioni ubaya kwa ziada ya pesa zile kuelekezwa kuboresha miundombinu mingine ya serikali ambayo itakuwa ni kwa faida ya jamii yote kwa ujumla wakiwemo waathirika wa tetemeko.
Kitendo chochote cha kutaka kutafunwa pesa zote na wana kagera nakichukulia kama ni kitendo cha ubinafsi na ukosefu wa uzalendo.
Tusijenge tabia ya kupinga kila kitu jamani.
Nitoe lawama zangu kwa wasaidizi wa JPM kwa kuacha upotoshaji huu kunawiri.
Kwa hili nipo pamoja na JPM.
Asante
Tume ya katiba
(Mtaalamu wa mifumo ya komputer na Mtakwimu anayeishi UHAMISHONI.)