Sioni referee toka tanzania can-angola

Freetown

JF-Expert Member
Apr 6, 2008
883
73
Timu zetu hazifanyi vizuri, hivi tunashindwa hata kuwa na referees wanaotuwakilisha kwenye mashindano kama CAN-Angola??
je kuna uhusiano kukua kwa mpira na kuwa na mareferee wazuri??
Sioni Mtanzania hata msaidizi kwenye hii orodha
Naomba maoni yenu

Referees
1. Martins de Carvalho Helder -Angola
2. Maillet Eddy - Seychelles
3. Coulibaly Koman - Mali
4. Damon Jerome - South Africa
5. Benouza Mohamed - Algeria
6. Codjia Koffi - Benin
7. Essam AbdelFatah - Egypt
8. Badara Diatta- Senegal
9. Djaoupe Kokou – Togo
10. Seechurn Rajindraparsad- Mauritius
11. Bennaceur Kacem – Tunisia
12. Ssegonga Muhmed- Uganda
13. Bennett Daniel – South Africa
14. Abdel Rahman Khalid – Sudan
15. Doue Normandiez Desire – Côte d’Ivoire
16. Alghamdi Khalil Ibrahim - Saudi Arabia

Assistant Referees
1. Manuel Candido Inancio- Angola
2. Ntagungira Celestin - Rwanda
3. Menkouande Evarist - Cameroun
4. Molefe Enock - South AfricA
5. Abdel Naby Nasser - Egypt
6. Achik Redouane - Morocco
7. Ogbamariam Angessom - Eritrea
8. Hassani Bechir - Tunisia
9. Chichenga Kenneth - Zambia
10. Gahungu Desire - Burundi
11. Haruna Ayuba -Ghana
12. Champiti Moffat - Malawi
13. Edibe Peter - Nigeria
14. El Maghrabi Fooad- Libya
15. Al Ghamdi Mohammed H.S -Saudi Arabia
16. Hassan Kamranifar - IR Iran
 
hili ni tatizo kweli maanake kama tunakosa refa kwenye mashindano haya basi ni ngumu pia kuwa naye WC
 
Enzi za ma referee legendary watanzania kama kina Gwaza Mapunda (R.I.P) zimepita.
 
Enzi za ma referee legendary watanzania kama kina Gwaza Mapunda (R.I.P) zimepita.
Lakini hii hana maana ndio tukose wengine wapya kinachohitajika ni kuwa committed na kuacha mambo yasiyokuwa ya kimpira
 
Enzi za ma referee legendary watanzania kama kina Gwaza Mapunda (R.I.P) zimepita.

Chama cha mpira kinafanya juhudi gani kuinua kiwango cha mareferee? au wao wanajisikiaje wanapoona hali kama hii??. hao akina Gwaza Mapunda nafikiri zilikuwa juhudi zao binafsi
 
Chama cha mpira kinafanya juhudi gani kuinua kiwango cha mareferee? au wao wanajisikiaje wanapoona hali kama hii??. hao akina Gwaza Mapunda nafikiri zilikuwa juhudi zao binafsi
wao wanafikiria sisi washabiki tuende uwanjani tu wakusanye mapato na kulumbana kila siku ila kuwa na ubunifu wanashindwa kabisa. Wanshindwa kuelewa kuwa marefarii pia ni muhimu sana katika kutangaza ubora wa taifa kisoka. Sasa hivi wanakazana kulumbana nani amrithi Marcimo, mambo ya ajabu sana haya
 
  1. Na sitaona ajabu kocha anachaguliwa yule ambaye yupo tayari kutoa 10% ya mapato yake ndo maana hata ukileta kocha toka Brazil mambo ni yale yale,
  2. Ni ubovu wa chama cha mpira kutokuwa na program ya kuwa na timu za vijana chini ya miaka 15
  3. Hawashikiani na wizara ya elimu kuibua vipaji na kuviendeleza huko mashuleni, mfano huko nyuma Makongo secondary ilijaribu kufanya hivyo.
  4. Yale mashindano ya taifa cup yalisaidia sana enzi hizo kuwapata wachezaji ambao hawapo kwenye timu zinazoshiriki ligi kuu.
  5. Hivi wizara husika ina mchango gani, yaani budget ya kuendeleza michezo ipo? na kama ipo inatumikaje?
 
Soka ya bongo ubabaishaji tu.,kwa aina ya referees tulionao sasa tusitegemee kusikia hata mmoja kaitwa ku-officiate kwenye international tournaments zaidi labda ya mashindano ya CECAFA.
 
Soka ya bongo ubabaishaji tu.,kwa aina ya referees tulionao sasa tusitegemee kusikia hata mmoja kaitwa ku-officiate kwenye international tournaments zaidi labda ya mashindano ya CECAFA.
Ni kweli but we need to change for sure
 
Soka ya bongo ubabaishaji tu.,kwa aina ya referees tulionao sasa tusitegemee kusikia hata mmoja kaitwa ku-officiate kwenye international tournaments zaidi labda ya mashindano ya CECAFA.

Naomba kutofautiana kidogo na kutoa vigezo vinavyotumika na CAF na FIFA kuteua marefa. CAF/FIFA wanaangalia points alizopata mwamuzi, na hizi points huhesabiwa katika kila mechi za kimataifa alizochezesha mwamuzi, mwenye point nyingi ndio huwa considered na kufanyiwa mchujo kwa kuangalia vigezo vingine. Tatizo la bongo hakuna refa ambaye atapewa mechi mfululizo za kimataifa ikiwemo friend matches ili ajikusanyie points nyingi. Mambo ya bongo leo kachezesha huyu, kesho atapewa yule ili nae apate kodi ya nyumba kesho kutwa atapewa mwingine apate ada ya mtoto ya shule. Mwisho wa siku utakuta katika labda mechi 6-8 za kirafiki kwa kipindi cha mwaka na nusu wamechezesha waamuzi 8 tofauti, hivyo inakuwa vigumu kupata points za kutosha kuwa considered. Enzi za kina Hafidh Ally walikuwa wanapewa mechi nyingi za kimataifa kuchezesha!
 
Back
Top Bottom