Sioni haja ya kwenda chuo

Unabaki na pesa, huna elimu, na hiyo pesa, unaipata wapi ya, kufanya biashara,!? Wazazi, wako,wanakupatia? Just like that, yaani mtoto wa miaka, 22,wazazi, wakupatie milioni 10,ufsnye biashara ufanye biashara baadala ya, kukulipia Ada ya chuo?!
Nadharia, tupu! Kwanza, hiyo ten M, hqipatikani, kwa mkupuo! Inqpqtikana inapohitqjika! Ukute tuition fee ni milioni, moja! Muhura, wa, kwanza wakupe 500K, ufanye biashara mwaka wa kwanza, then baaadae wakupe tena 500k, mpaka miaka 4 ipite kila mwaka unakuza biashara kwa milioni moja!
 
Kwanini asijaribu kufanya uhasibu?
 
Sio haina haja tu, kwa wengine kama sisi haina manufaa. Hasa katika nyakati hizi.
Mkuu de gunner.Chuo unalijilipa Ada mwenyewe au unaomba mkopo serikalini? Kama unajilipia mwenyewe iyo pesa ya ada bac fanyia biashara tafuta mentor kwenye biashara ambayo unataka kuifanya akutrain vizuriiyo elimu uliyonayo inakutosha.ILA kama ni pesa ya serikali basi nakushauri omba mkopo nenda chuo kadome degree usikate tamaa kwa kuangalia watu wangapi wapo mtaani wamesoma hawana kazi.kila mtu na rizki yake la muhimu mtangulize mungu fanya ibada kuwa na nidhamu fanya na jitihada.
 
Nimekuelewa sana mkuu na hoja yako ya garama,
Ila bado sijashawishika na dhana ya kusema et usipoenda chuo unakosa elimu, labda kama unampango wa kuajiriwa kupitia vyeti, ambako nako kuna competition kubwa.
 
Nashukuru kwa ushauri , ila nimeshapita chuo na nimeleta hii mada kuonesha watu na jamii, kuwa chuo ni path amabayo wengi wanachukua na kuja kuregret baadae vijana wengi wamepoteza mda kwenda vyouni na kujikuta wanafanya vitu tofauti na walivyosomea simply because hakuna ajira...
 
Nilihitimu kidato cha SITA 2014, Tukaenda mujibu.. Mm na wanangu 6 tulipata “Zali” la kubaki na Option ya kuajiliwa baadae.. Nikalikacha kwa kuhadahika kwa bata za chuo na degree, wanangu wakabaki Jeshini, 2016 wakaajiliwa na wakala nyota! Mi nikahitimu 2017 mpk leo ni mjobless na wanangu wana maisha. Nishaomba nafasi Jeshini mpk “Nimebloo” Degree nayo haijanipa ajira wala ujila.
 
Pole sana mkuu, kuna inshu wengi hawaijui kuhusu elimu hasa nyakati hizi. Mimi naona ni kama biashara tu, update vyeti then hio ndo iwe kadi yako ya kupata ajira. Hao washakaji walisoma mchezo wakajua tu hiyo sijui mikopo na baba za chuo ni za mda tu, ila uhakika wa kupata ajira ni mdogo sana. Na sasa wanakula maisha hawata jutia ingawa walipitia msoto jeshini.
 
hata ningeajiliwa mshahara hauvuki 600k. Usomi wa nchi hii ni huzuni
 
Riziki yako inakuja mkuu
 
Umenifanya nipige hesabu ya ada na matumizi nimepata zaidi ya 12M😂

Acha ujinga degree itakulipa siku moja, hata ukichelewa ila Itakulipa tu punguza papara..!
Kupata elimu ya degree ni vizuri na ina umuhimu wake, ila usimjaze kwamba eti itakuja kumlipa siku moja......asije kukulaumu atakapofika uzeeni na malipo hayo hajayapata.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…