Angalia unakosea wapi na ujipange upya, cheki CV yako kama ipo ki Professional, Cover letter jaribu kufanya research, watu wanachukuliwa wengi tu na hawana ndugu, sisemi kama upendeleo hamna, hilo wanalijua wenyewe, nacho maanisha wengi wanapenda kulalamika wakati ukiangalia kwa undani ukifatilia unaona kua mlalamikiaji ndo mwenye makosa, Ajira ni kama upo vitani, kuna ushindani, lazima ujiweke vizuri, we unajifundisha kushika bastola tu wakati watu wanashika bastola, bunduki, mtu anategua mabomu sifa zote hizo anaendesha tenki lile la vita, utashindana nae? Jipange.
Kama unauhakika upo vizuri kote kote basi angalia kwingine hauwezi jua Mungu anakuepushia kitu gani, hatujui ya mbeleni, waweza kupata ajira miezi 6 ikatokea shoti section yako ukabambikiziwa kesi ukawekwa ndani, unajuaje? sasa ni kumshukuru Mungu ukikosa jambo lolote yeye ndo mwenye kufahamu zaidi, usichoke kumuomba, kitu km ni rizki yako ni yako tu.
Kila la heri