JacksonMichael
JF-Expert Member
- Mar 22, 2012
- 339
- 61
Ndugu wadau,
Ukweli kuwa CCM ndio chama kikomavu na cha kidemokrasia umedhihirika baaba ya kushindwa ARUMERU.
Mgombea wa ccm ameahidi kutoa ushirikiano na amempongeza nasary kwa ushindi mdogo alioupata, pia ameelezea atatumia taaluma yake ya sheria katika kuwaletea maendeleo wana arumeru.
Ingekuwa CDM wameshindwa unafikili tungesikia matamko kama haya? huu yet ni ushahidi mwingine wa uwezo mkubwa wa CCM, nakiri laiti isingekuwa mipangilio mibovu ya CCM "Washindwe tuheshimiane" na kuchagua "mbumbumbu" kusimamia kampeni matokeo yasingekuwa yale.
Taarifa kamili na NIPASHE:
Aliyekuwa mgombea ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mdogo Jimbo la Arumeru Mashariki mkoani Arusha, Sioi Sumari, amesema atapima upepo wa kisiasa ulivyo kabla ya kuamua kugombea tena ubunge katika jimbo hilo katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
Sioi alitoa kauli hiyo baada ya kuulizwa na NIPASHE kama atagombea tena ubunge katika jimbo hilo, baada ya kushindwa na mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joshua Nassari, katika uchaguzi uliofanyika Jumapili iliyopita.
Uchaguzi huo ulifanyika kujaza nafasi ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, marehemu Jeremiah Sumari, aliyefariki dunia mapema mwaka huu.
Alipoulizwa kama ana mpango wa kuingia kwenye kinyanganyiro cha ubunge kwa mara nyingine katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, alisema bado hajafikiria suala hilo na kwamba wakati ukifika ataangalia upepo ulivyo kwanza.
Kuhusu hatma yake kisiasa baada ya kushindwa, Sioi alisema fani yake ni sheria na ni wakili wa Mahakama Kuu na siyo mwanasiasa, hivyo ataendelea na kazi yake ya uanasheria.
Wakati huo huo, Sioi ameahidi kutoa ushirikiano kwa mbunge mteule wa jimbo hilo, Joshua Nassari, kwa lengo la kuharakisha kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo hilo.
Sioi alisema amekubaliana na matokeo yaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) ambayo yamempa ushindi mgombea wa Chadema na kwamba atahakikisha anashirikiana naye katika kuhakikisha wananchi wa Arumeru wanapata maendeleo.
Nimeyapokea vizuri kwa moyo wote matokeo, maana asiyekubali kushindwa si mshindani, nataka kuamini kuwa wana-Arumeru ndio waliofanya uamuzi na kamwe siwezi kuwa na pingamizi lolote katika uchaguzi huo, alisema Sioi.
Aliongeza kuwa pamoja na kwamba kulikuwa na mapungufu ya hapa na pale wakati wa uchaguzi huo, lakini hawezi kuchukua hatua ya kukataa matokeo hayo kwani wananchi wa Arumeru wametumia demokrasia yao kumchagua mtu wanayemuona atawaletea maendeleo.
Ni hayo tu
Shina la wakereketwa wa CCM
Nje ya nchi