Siogopi Lowassa kuwa rais bali naogopa genge lake!


UNDENIABLE

UNDENIABLE

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2013
Messages
2,305
Points
1,500
UNDENIABLE

UNDENIABLE

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2013
2,305 1,500
Heshima mbele!

Haya ni mawazo yangu binafsi naomba kutangulia kusema hivyo.

Natazama kwa ukaribu sana jinsi move ya urais ndani ya CCM inavyoendelea. Jana alikuwa Lowassa, leo ni Wassira na Nchemba. Move bado itaendelea!

Sijawahi kuamini kama nchi hii inaongozwa na rais kwa utashi wa urais baada tu ya kifo cha Hayati Mwalimu Nyerere. Japo Nyerere pia alipata tabu sana kukabiliana na hili genge, hata naamini ndio waliomstaafisha Nyerere (ni mawazo yangu). Hili genge lina nguvu za ajabu sana, you cant beat them!

Kumbuka urais wa Mwinyi baada ya kifo cha Nyerere. Mwinyi alishindwa kabisa kuhimili nguvu za hili kundi akakata tamaa na kuamua nchi ijiendee yenyewe. Angalia pia urais wa mkapa. Mkapa alitumia mkono wa chuma kuhakikisha kuwa habari nyingi za serikali yake hazipatikani kirahisi. Lengo kuu ni kuficha umafia wa hili genge.

Akaja kikwete. Kila mtu ni shahidi kwa yanayoendelea kila kukicha. Ni kama serikali imeparakanyika vipande vipande. Mapema kabisa alisalimu amri kwa genge hili ambalo ndilo lililomuingiza madarakani na ndilo linalotaka kumuingiza madarakani mh Lowassa. Ndipo naposema simuogopi Lowassa kuwa rais bali naogopa genge hili la mafia linalomuingiza madarakani.

Uongozi wa ki rais kwa sasa ni wa kinadharia tu kukidhi matakwa ya dunia na si vinginevyo. Hii nchi inaongozwa na genge la mafia ambapo wao sio viongozi wa kisiasa kwa namna yeyote ile. Sio rais kuwaona kwenye ulingo wa kisiasa. Watu hawa hata hawazidi kumi, naweza kusema hivyo.

Hili genge la mafia wana kazi moja tu nayo ni biashara zao. Ni wafanyabiashara haramu mfano madawa ya kulevya kwa kutaja biashara moja tu. Kwao wanasiasa ni daraja la kufanya mambo yao ya kibiashara, basi. Watapambana kwa kila namna wawezavyo kuwaweka viongozi wa kisiasa kwa nafasi za kisiasa kwa namna watakavyo wao.

Mwanasiasa yeyote aliepo mrengo wa kushoto na genge hili la mafia hastahili kuwa kiongozi. Kumbuka sakata la madawa ya kulevya la Mwakyembe na kuhamishiwa wizara ya afrika mashariki! Kumbuka sakata la bandari la sitta na mwakyembe, ni kama sitta alitumika kumchafua mwakyembe. Mwakyembe alishughulikiwa vilivyo. Hili genge ni invisibles kwa wananchi wa kawaida lakini ni genge hatari lenye nguvu kupita kiasi.

Tatizo kubwa la genge hili la mafia ni kuwa hawaangalii maslahi mapana ya taifa wao ni biashara zao tu. Na hapa ndipo ndipo kulipo na shida kubwa.

Angalia namna genge hili linavyofanya kazi.
Leo Wassira anatangaza nia, pia Mwigulu anatangaza nia. Nakuhakikishia hawa wote wanatumika na lile genge la mafia kumuingiza Lowassa madarakani. Usijisumbue kutafakari.

Simuogopi Lowassa kuwa rais bali naogopa genge linalomuingiza kwenye kiti cha urais!
 
tyc

tyc

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2014
Messages
323
Points
500
tyc

tyc

JF-Expert Member
Joined Feb 25, 2014
323 500
Mkuu Undeniable, naungana na wewe juu ya mashaka ya mfumo uliopo nyuma ya mh.EL, hawa wanaojiita friends of Lowassa ambao wanapigana kwa kila namna kuhakikisha jamaa anaingia Ikulu kwa GHARAMA yoyote. Juzi katika mahojiano baina ya EL na wahariri aliwasifia watu kama kina Rostam, Karamagi n.k ambao katika macho ya jamii hawa jamaa si waadilifu kutokana na kuhusishwa na kashfa mbalimbali za ufisadi.

Pia hawa key players wanaomkampenia EL kusaka urais ndio waliotumika kuuingiza SERIKALI DHAIFU YA JK MADARAKANI.

So if we think and behave in the same way we SHOULDNT expect a different result!!!

SUMU YA HII NCHI NI WANANCHI WENYEWE,,,MAANA WENGI WANA ULEMAVU MKUBWA WA KIFIKRA!!!
 
Root

Root

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2012
Messages
29,917
Points
2,000
Root

Root

JF-Expert Member
Joined Jan 23, 2012
29,917 2,000
Kila serikali duniani huingizwa na watu hapo walipo
 
M

masagati

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2012
Messages
415
Points
250
M

masagati

JF-Expert Member
Joined Oct 16, 2012
415 250
Inatia huruma kuwa na wananchi wanao toa maamuzi kwa ushabiki na si ktk kujua uhalisia wa mtu mwenyewe
 
Daudi Mchambuzi

Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Messages
38,878
Points
2,000
Daudi Mchambuzi

Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined Nov 25, 2010
38,878 2,000
Eti first eleven inayoaminiwa na Lowasa ni Chenge, Rostam, karamagi, tibaijuka nk
 
Mzito Kabwela

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2009
Messages
17,820
Points
2,000
Age
36
Mzito Kabwela

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Joined Nov 28, 2009
17,820 2,000
Urais kwa sasani tunda jema linalosubiriwa na Ukawa
 
Chibolo

Chibolo

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Messages
3,520
Points
2,000
Age
38
Chibolo

Chibolo

JF-Expert Member
Joined Oct 13, 2012
3,520 2,000
Nakubaliana uchambuzi hata mi nimeshaliona hilo na EL atapita ndani ya chama ila wananchi wakimchagua kuwa rais tujiandae kula nyasi.
 
W

wakimataifa

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2014
Messages
942
Points
0
W

wakimataifa

JF-Expert Member
Joined Nov 16, 2014
942 0
halafu cha kushangaza kila alieengulia kwa tuhuma katika serikali hii yupo kwa lowasa mfano tibaijuka
 
Nakapanya

Nakapanya

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2012
Messages
1,966
Points
1,250
Age
39
Nakapanya

Nakapanya

JF-Expert Member
Joined May 22, 2012
1,966 1,250
Kama sijakuelewa vile,"Urais wa Mwinyi baada ya kifo cha Nyerere"?......ina maana Nyerere alikufa wakati Mwinyi yupo madarakani?
 
G

Getstart

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Messages
6,269
Points
2,000
G

Getstart

JF-Expert Member
Joined Oct 13, 2012
6,269 2,000
"...Kumbuka urais wa Mwinyi baada ya kifo cha Nyerere. Mwinyi alishindwa kabisa kuhimili nguvu za hili kundi akakata tamaa na kuamua nchi ijiendee yenyewe. Angalia pia urais wa mkapa. Mkapa alitumia mkono wa chuma kuhakikisha kuwa habari nyingi za serikali yake hazipatikani kirahisi. Lengo kuu ni kuficha umafia wa hili genge..."

Nafikiri hii statement ni uongo. Nyerere alifariki baada ya Mwinyi kukamilisha vipindi vyake viwili vya utawala.
 
Elungata

Elungata

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Messages
30,896
Points
2,000
Elungata

Elungata

JF-Expert Member
Joined Jan 28, 2011
30,896 2,000
zinaitwa special interest groups...
duniani pote zipo labda kasoro mbinguni tu
 
Elungata

Elungata

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Messages
30,896
Points
2,000
Elungata

Elungata

JF-Expert Member
Joined Jan 28, 2011
30,896 2,000
Kama sijakuelewa vile,"Urais wa Mwinyi baada ya kifo cha Nyerere"?......ina maana Nyerere alikufa wakati Mwinyi yupo madarakani?
chezea ma analyst wa bavicha wewe?,wako so dedicated.
 
jingalao

jingalao

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Messages
29,070
Points
2,000
jingalao

jingalao

JF-Expert Member
Joined Oct 12, 2011
29,070 2,000
Genge la kina serukamba ,Msukuma,tibaijuka,kingunge na lugola....ndio wanakupa hofu
 
Marire

Marire

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2012
Messages
11,833
Points
2,000
Marire

Marire

JF-Expert Member
Joined May 1, 2012
11,833 2,000
Mleta mada umenisaidia sana mkuu

Maana jana nilizusha ubishi sehemu flani kuwa lowasa akisema anampa chenge uwaziri mkuu na rostam waziri wa fedha kuna mtu atalalamika?
_Wakasema hawezi na blabla kibao kwani si matakwa ya rais kumchagua amfaaye?
 
Marire

Marire

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2012
Messages
11,833
Points
2,000
Marire

Marire

JF-Expert Member
Joined May 1, 2012
11,833 2,000
Jingine linaloniumiza kichwa kama lowasa,chenge,rostam walitaka kufutwa uanachama na nape akatutangaiza amewapa siku tisini za kujivua gamba kwa tuhuma za ufisadi
Je ccm hao hao watakuja wamnadi lowasa kuwa ni msafi na tumpe kura?

Mi nasubiria tu hii movie
 
UNDENIABLE

UNDENIABLE

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2013
Messages
2,305
Points
1,500
UNDENIABLE

UNDENIABLE

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2013
2,305 1,500
Kama sijakuelewa vile,"Urais wa Mwinyi baada ya kifo cha Nyerere"?......ina maana Nyerere alikufa wakati Mwinyi yupo madarakani?
"...Kumbuka urais wa Mwinyi baada ya kifo cha Nyerere. Mwinyi alishindwa kabisa kuhimili nguvu za hili kundi akakata tamaa na kuamua nchi ijiendee yenyewe. Angalia pia urais wa mkapa. Mkapa alitumia mkono wa chuma kuhakikisha kuwa habari nyingi za serikali yake hazipatikani kirahisi. Lengo kuu ni kuficha umafia wa hili genge..."

Nafikiri hii statement ni uongo. Nyerere alifariki baada ya Mwinyi kukamilisha vipindi vyake viwili vya utawala.
Let us try to push beyond the limits. Hivi, of all the words hizi ndo zimekuwa concern kubwa kwenu?!
 
KIM KARDASH

KIM KARDASH

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Messages
5,099
Points
1,250
KIM KARDASH

KIM KARDASH

JF-Expert Member
Joined Sep 21, 2011
5,099 1,250
Pia marafiki wa lowassa,jamaa ana marafiki wengi sana kwa kiwango cha mkuu wa nchi,hawa watakua mzigo kwa mlipa kodi tu hakuna namna nyingine ya kuwaridhisha
 
MOTOCHINI

MOTOCHINI

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2014
Messages
24,751
Points
2,000
MOTOCHINI

MOTOCHINI

JF-Expert Member
Joined Jan 20, 2014
24,751 2,000
"...Kumbuka urais wa Mwinyi baada ya kifo cha Nyerere. Mwinyi alishindwa kabisa kuhimili nguvu za hili kundi akakata tamaa na kuamua nchi ijiendee yenyewe. Angalia pia urais wa mkapa. Mkapa alitumia mkono wa chuma kuhakikisha kuwa habari nyingi za serikali yake hazipatikani kirahisi. Lengo kuu ni kuficha umafia wa hili genge..."

Nafikiri hii statement ni uongo. Nyerere alifariki baada ya Mwinyi kukamilisha vipindi vyake viwili vya utawala.
Ebu muerimishe nduguyo
 

Forum statistics

Threads 1,283,912
Members 493,869
Posts 30,805,854
Top