Sio wanawake tu, hata wanaume hupenda kusifiwa

Ben-adam

JF-Expert Member
Jun 2, 2023
765
1,669
Kila mtu anapenda sifa (kusifiwa), si wanawake pekee wanaopenda kusifiwa isipokuwa tofauti yao na sisi ni reaction baada ya kusifiwa au kutosifiwa.

Mfano, Mwanaume ukimsifia kwakitu fulani utasikia"ah kawaida tu mbona hahh" yaani haipi uzito sana kwa wakati huo lakini amependezwa!

Mwanamke yeye ukimsifia utaona kabisa body language yake; atafurahi ma asante juu huku akilamba lamba lips 🥰

Awe mtoto, Mwanaume au mwanamke, wote wasifiwe pale wanapofanya vizuri.

Si kufanya vizuri tu, hata pale anapokosea Muonye/mkosoe, lakini pia angalia neno zuri la kumwambia.

Sifa huwa na Nguvu ya pekee ndani ya mtu. Utasikia; "Ben hanaga shukrani yaani hashukuru kabisa huyo jamaa" kumbe shukran anayoimaanisha ni "sifa"! maana yake ni Ben-adam hana tabia ya kusifia!🤭

Fundi akimaliza kukujengea nyumba ukamsifia/ukasifia kazi yake, anaweza kukujengea na banda la kuku bure!

Wale watu wanaoitwa machawa kazi yao kubwa ni kumsifia boss.

Sifa ni nzuri, zina Energy, zitumie vizuri.. Usizidishe maana utaonekana mnafiki.

Pia usiache kusifia panapostahili.

Ukitaka wafanyakazi wako afanye kazi nzuri zaidi dawa sio kuwapa usimamizi mkali wewe wasifie tu!

Mtoto hafanyi vizuri shuleni, achana na mikong'oto, msifie kwa kile kizuri anachofanya, muelekeze, anapofanya vizuri "msifie". kwishaa!!

NB: Sifa huambatana na zawadi, mara moja moja uwe unatoa vizawadi (offer)
 
Nimeipenda, hasa hapo mwisho umemalizia vizuri.

Kwa mfano ukamsifia mdada mkali, kisha ukamtwanga na vipesa kidogo, kifuatacho..!!😁
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom