Sio wanawake tu, hata wanaume hupenda kusifiwa

Ben-adam

JF-Expert Member
Jun 2, 2023
765
1,669
Kila mtu anapenda sifa (kusifiwa), si wanawake pekee wanaopenda kusifiwa isipokuwa tofauti yao na sisi ni reaction baada ya kusifiwa au kutosifiwa;

Mfano, Mwanaume ukimsifia kwakitu fulani utasikia"ah kawaida tu mbona hahh" yaani haipi uzito sana kwa wakati huo lakini amependezwa!

Mwanamke yeye ukimsifia utaona kabisa body language yake; atafurahi ma asante juu huku akilamba lamba lips 🥰

Awe mtoto, Mwanaume au mwanamke, wote wasifiwe pale wanapofanya vizuri!

Si kufanya vizuri tu; hata pale anapokosea Muonye/mkosoe, lakini pia angalia neno zuri la kumwambia

Sifa huwa na Nguvu ya pekee ndani ya mtu

Utasikia; "Ben hanaga shukrani yaani hashukuru kabisa huyo jamaa" kumbe shukran anayoimaanisha ni "sifa"! maana yake ni Ben-adam hana tabia ya kusifia!🤭

Fundi akimaliza kukujengea nyumba ukamsifia/ukasifia kazi yake, anaweza kukujengea na banda la kuku bure!

Wale watu wanaoitwa machawa kazi yao kubwa ni kumsifia boss !

Sifa ni nzuri, zina Energy, zitumie vizuri.. Usizidishe maana utaonekana mnafiki.

Pia usiache kusifia panapostahili.

Ukitaka wafanyakazi wako afanye kazi nzuri zaidi dawa sio kuwapa usimamizi mkali wewe wasifie tu!

Mtoto hafanyi vizuri shuleni, achana na mikong'oto, msifie kwa kile kizuri anachofanya, muelekeze, anapofanya vizuri "msifie". kwishaa!!

NB: Sifa huambatana na zawadi, mara moja moja uwe unatoa vizawadi (offer)
 
Kuna uyo x-girlfriend wangu, toto la ki-marangu limenona mnoo udhaifu wake mkubwa ni ukimsifia, yaani nimeachana nae muda sana na tumebaki kama marafiki tu ila najua udhaifu wake ulipo ili akanipe tunda ni kumsifia, so mfano amepost picha yake status, niweka coment ya kumsifia tu kuanzia nywele zake mpaka nguo, posibility ya kwenda kumla ni 99.9%, wanawake wanapenda kusifiwa kuliko mwanaume.
 
Sura ninayoweka mwanaume mwenzangu akinisifia
IMG_20231116_080355_013.jpg
 
Kuna mwanamke alinisifia nina sauti ya base tukiwa tunaongea kwenye simu miezi kama 6 iliyopita.

Sijasahau mpaka leo sijui kwanini😂

Kwangu mimi naona ni kweli, wanawake kutoa sifa za kumaanisha bila utani utani ni ngumu sana. Au wanaogopa tutaomba papuchi?

Kusifiwa na me mwenzako kuna protokali zake.
 
Kuna uyo x-girlfriend wangu, toto la ki-marangu limenona mnoo udhaifu wake mkubwa ni ukimsifia, yaani nimeachana nae muda sana na tumebaki kama marafiki tu ila najua udhaifu wake ulipo ili akanipe tunda ni kumsifia, so mfano amepost picha yake status, niweka coment ya kumsifia tu kuanzia nywele zake mpaka nguo, posibility ya kwenda kumla ni 99.9%, wanawake wanapenda kusifiwa kuliko mwanaume.
Sifa zinapenya ubongoni😅
 
Kuna mwanamke alinisifia nina sauti ya base tukiwa tunaongea kwenye simu miezi kama 6 iliyopita.

Sijasahau mpaka leo sijui kwanini😂

Kwangu mimi naona ni kweli, wanawake kutoa sifa za kumaanisha bila utani utani ni ngumu sana. Au wanaogopa tutaomba papuchi?
Unaweza ukaanza kujirekodi ili uhakikishe 😅
Na hutafanya mara moja..

Mimi nilimsifia binti fulani hivi mdogo alikuwa anapenda sana kuvaa suruali Ila bahati mbaya miguu yake haikuwa inasapoti zile suruali zake, basi siku moja akapigilia gauni, nikamsifia sana... Hakurudia tena kuvaa suruali nikiwepo!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom