Sio siri ninaumia

Nyakwaratony;
Pole sana kwa yanayokusibu na ubaya/uzuri ni kwamba umeanza kuonja machungu hata kabla ya ndoa. Kwani, wengi ni kawaida kufurahi sana kipindi cha bf na gf kuliko baada ya kuingia kwenye ndoa. Sasa kwako, kama hata kwasasa haupati neno Dear/Honey/Sweetie/Jaber/Jarinda/Mpenzi/Mpenzi/mrembo n.k; basi napata shida kuamini kama utaweza kusikia haya maneno maishani tena kutoka kwa huyo na hasa utakapoolewa. Kwani, kwa uzoefu maisha ya kudeka sana kwenye mapenzi kwa walio wengi ni kipindi cha uchumba (bf/gf); kwani baada ya kuingia kwenye ndoa kuna changamoto nyingi sana za maisha.

Jaber, usione ndoa nyingi watu wanatoka kwenye Jumba kubwa na magari ya maana na ni hakika wamefanikiwa sana ktk maisha haya lkn huko ndani ya nyumba wengi sana hawasikii hayo maneno kama hayo unayotaka kusikia kutoka kwa huyo jamaa yako. Lkn, hawa wote ambao kwasasa hawana maelewano, wengi wao huko nyuma hasa kipindi cha urafiki wao waliitana majina yote hayo mazuri. Lkn, baada ya kuingia kwenye ndoa mambo yamebadilika. Hivyo, ni juu yako wewe kujaribu kupima mwelekeo wa moyo wako na jinsi hali ilivyo kati yenu na ujaribu kuona kama kuna upendo. Wasiwasi wangu ni kwamba ukilazimisha kuingia kwenye ndoa wakt toka mwanzo umeanza kuona hakuna upendo; then jiandae huko mbeleni.

Nyathiwa; nataka nikushauri ya kwamba kamwe usilazimishe kuwa pale ambapo unaona hakuna upendo, kwani itakugharimu sana baadaye. Ni bora uwe huru kwasasa ukimwomba Mungu naye atakupa mtu mzuri atakayekupenda na kujali familia yenu. Naomba unielewe kwamba, wewe binafsi angalia hali ilivyo, jaribu kupiga picha future yenu (japo siku zote si sahihi), angalia jinsi unavyompenda na kuona kama na yeye anakujali/anakupenda? tusidanganyane, hakuna mtu asiyeweza kupata muda wa kumfikiria Mpenzi wake hata kama yuko busy kiasi gani. Kwani kazi gani isiyotambua nafasi ya familia pia ktk jamii zetu? Kwanini yeye asionyesha kama anakuthamini? ANGALIA USIJE UKAJIKUTA UNAONDOKA NA AYAKI, KWANI AYAKI haina cha HODI na ni jukumu lako ku take care ya afya yako. Kama haonyeshi kama anakujali kwa kisingizio kwamba yuko busy kwani wewe pia si unafanya kazi?
Nyathiwa inyalo pm ya mondo wamed miyore paro, nekech adieri iduaro paro.
Oriti Jaber.
 
Mapenzi bila mawasiliano ni sawa na chai bila sukari au kuku amechomwa/kaangwa/pikwa vizuri na ananukia vizuri lakini hana chumvi. Mi nadhani mawasiliano yanaleta radha kwenye mapenzi, yanaboresha mapenzi.
 
Da afadhari. Kumbe tuko wengi, nilidhani peke yangu. mimi wife alishasema mpaka akachoka ikabidi awe mpole
 
Hali zenyu bhana! Hope hamjambo wanajamii wenzangu. mimi ni ke nina b/f wangu yupo mkoani. To be honestly ninampenda jamani. Tatizo ni kwamba yeye haoneshi kama ananipenda. Naweza m-call hata cku tatu mfululizo yeye wala hata hastuki akacall back, najikaza ili aanze lakini najikuta tu mi ndo naanza kumpigia ili tu roho yangu iridhike, nashindwa kujicontrol.. sms ndo kwanza mpaka nimuulize umepata sms yangu ndo anakujibu, TENA jibu lenye la kawaida sana kama anamjibi man mwenzie. NATAMANI KUSIKIA I LOVE, NATAMANI KUSIKIA I MISS U, NATAMANI MANENO MATAMU YA KIMAPENZI TOKA KWA MTU NINAYEMPENDA. lakini siyapati naumia natamani kuachana naye ila roho yangu bado inampenda kwa kweli. Me binafsi napenda sana kuchat, kuongea hasa nyakati za ucku ukizingatia tupo mbali walau tupeane pole, tuambiane maneno matamu matamu ila yeye mkavu sana katika maongezi cjui hani-feel??? Tena ndio huwa wa kwanza kuaga utadhani kapiga yeye. Nashindwa kupata jibu yuko upande gani, nikijaribu kuumuuliza anasema yuko sawa. Mara nyingi hana story jamani nifanyeje........ naumia kwa kweli........
Usiwaze mimi ni me nina g/f wa hivyo ni bora tukafarijiana katika kipindi hiki kigumu...
 
Nahisi kuchukua uamuzi bila ya kumhusisha huyo jamaa utakuwa hujamtendea haki,jaribu kumhoji kulikoni isije ikawa nawe ni tatizo!
 
Pole!halafu umenichekesho kwelo pale uliposema "Halafu ndio huwa wa kwanza kuaga utadhani kapiga yeye"kwekwekwekwekwe teh teh teh teh teh...!
 
Kwanza nikusifu umependeza,unatabasamu eeh............mwambie binti mwenzio avunje ukimya amwambie ukweli kwamba hapendi anavyofanyiwa (awe na kifua hasa) halafu aone reaction yake.Kama ataonyesha kuelewa basi ajue ni swaga zake tu, wakati mwingine wanaume tunapenda deko fulani hivi hasa kama tunapendwa hatutaki kuonyesha sana eti tumekufa (hiyo siri usimwambie mtu).

Halafu kingine muulize huyo binti (me naogopa kumuuliza moja kwa moja ni dada yangu) kama huyo B/F ni wa kutoka maeneo ya kwao,kama ndivyo ohoooooooooooooo.........jasiri haachi asili!!!
Asante mkuu,hapo anaongelea miaka miwili ni mda ambao unatosha watu kufahamiana,na anasema kila akiongea naye mwenzie anaona ni kitu cha kawaida tu means hajali,na katika mapenzi sidhani swala la makabila au eneo analotoka linaweza kumfanya mtu asiwe tayari kuwasiliana na mwenzie.

 
hapo sawa ntajitahidi may be nikipata likizo make yupo mkoani!

Hapo ndo utajua mbivu na mbichi..... yaani usimwambie wewe tia timu mwambie niko stand hapa, uone atakavyo ingia mitini... au muulize akuelekeze kabisa anapoishi ili akitoka kazini akukute uko mlangoni uone kama hakumwaga vumbi... miguno, visingizio vingi , kuzima simu na kesho kukusindikiza stand uondoke.. :lol:
 
Pole!halafu umenichekesho kwelo pale uliposema "Halafu ndio huwa wa kwanza kuaga utadhani kapiga yeye"kwekwekwekwekwe teh teh teh teh teh...!

Mzee hapo ndo haswa alipotakiwa kupaelewa huyu bibie, manake ni kwamba anamboa jamaa... anataka kuwahi.. ndo maana anakata yeye simu..... akichelewa hapo utasikia anajidai... halooo ...... halooooo.. kama vile hamsikilizani... mara anakata simu na kuizima kabisa......:lol::lol:
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom