Sio sawa kabisa dhifa za taifa kuonyeshwa kwenye tv | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sio sawa kabisa dhifa za taifa kuonyeshwa kwenye tv

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mama kubwa, Nov 8, 2011.

 1. m

  mama kubwa JF-Expert Member

  #1
  Nov 8, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 2,410
  Likes Received: 1,968
  Trophy Points: 280
  Jana niliona dhifa ya Taifa ,wakubwa wanakunywa michuzi na wine. Sio vibaya kumkirimu mgeni lakini kwa uelewa wangu mdogo ni dharau kwa wavuja jasho, watu wasio na uhakika wa mlo hata mmoja.

  Tv zimeenea nchi nzima hata vijijini kule igunga ambapo watu wanakunywa maji na ng'ombe , kule kwetu ambapo mtu akila mara moja anashukuru mungu, anaonyeshwa wanene wanavyofaidi nchi hii.

  Swali kwa wenzetu mnaoishi nje hivi rais wetu akifanyiwa dhifa huwa anaonyeshwa live? watanzania tumechoka na dharau hii hatukatai kuleni lakini msitukebehi tunao lala na njaa.
   
 2. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #2
  Nov 8, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,091
  Likes Received: 6,557
  Trophy Points: 280
  Mama kubwa nakukubali kwa mambo ya siasa,
  enzi za mwalimu walikuwa wanatangaza kwenye RTD, mama eda sanga aliifanya sana hiyo kazi,
  kwa kuonyesha kwenye tv ingekuwa safi waonyeshe yale mambo mengine mengine ambayo hayataleta chuki kwa watazamaji.
   
 3. m

  mama kubwa JF-Expert Member

  #3
  Nov 8, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 2,410
  Likes Received: 1,968
  Trophy Points: 280
  Kibaya zaidi wenyewe hawalioni hili.Hebu fikiri wale watu wanaokula majajalani kule Dodoma na picha hii ya wanene wakitanua hata hotuba zao hasa ya mgeni wa jana ni mtu aliekuja kuenjoy tu mie binafsi naona si sawa.
   
 4. feis buku

  feis buku JF-Expert Member

  #4
  Nov 8, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 2,371
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mmh!!!
   
 5. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #5
  Nov 8, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,328
  Likes Received: 22,172
  Trophy Points: 280
  Kwa hasira mtu unaweza kuirushia tv yako nyundo
   
 6. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #6
  Nov 8, 2011
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Haikuwa busara hata kidogo kuonesha kwenye tv zaidi ya shughuli za kawaida ambazo kila mwananchi atajua kuwa kuna suala la msingi na ambalo linaleta maendeleo kwao na si starehe hata kama huwa zinafanyika.
   
 7. mwaJ

  mwaJ Tanzanite Member

  #7
  Nov 8, 2011
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 4,076
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ngoja nisubiri wenye hekima zao wazungumze.
   
 8. F

  FJM JF-Expert Member

  #8
  Nov 8, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kumbe na wengine mmeona. Sikuelewa na bado sijaelewa mantiki ya kuonesha watu wanakula? Na kitu kilichonishangaza zaidi mtangazaji wa TBC alimua kuongea throughout kwa hiyo hatukusikia Rais Kikwete alisema nini? Ni pale tu Prince Charles alipokuwa anaongea ndio TBC waliondoa porojo zao na kuacha watu wasikie ujumbe wa mwana wa Malkia. Nimetumia porojo maana mtangazaji wa TBC hakuwa na point hata kidogo. She was just making noise!

  Hata hivyo kuna vitu vingine nimeona vya kushangaza. Kwa mfano, pamoja na kwamba hatukusikia Kikwete alisema nini hasa, mara baada ya kumaliza kuongea Salva aliongea (nadhani alishukuru)! This is wrong wrong wrong. Salva anaongea in the middle of toasting? Pamoja na kusafiri hawa watu hawajifunzi? Yeye Salva ni nani mpaka ashukuru? Na kwa nini aongee between token ya Rais Kikwete na Prince Charles?

  Pili, sina nia ya kudharau masoko yetu hata kidogo lakini dhifa gani ya kitaifa watu (wa-TZ) wana-move around kama wako sokono na wengine wanaongea kwenye simu zao? Dhifa ya kitaifa (State banquet) ina nidhamu yake.Tables manners hakuna kabisa! Kwa ujumla ilkuwa vurugu na sio state banquet.
   
 9. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #9
  Nov 8, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  JK alikuwa anaongeza CV kwa watanzania na kuwaonyesha kwamba si mchezo kuwa ikulu lazima kufanya kweli sasa lieni yeye kesha fanya kweli .Jamanij huyu ana PhD tena 2 za field tofauti ? Mnalia eti Mashoka toka UK asubuhi karibu nyumbani .Jioneeni wenyewe .
   
 10. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #10
  Nov 8, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Walikuwa wanawalingishia walianza na stata wakaja na mzigo sasa ule wa haja na miwine.
  Uliza bajeti ya ulo mlo wa jana kwa watu wale usishangae ukaambiwa Ikulu imetumia mil.240 kwa chakula cha usiku wa jana
   
 11. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #11
  Nov 8, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,229
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  Ndio maana mlimchagua jk. sasa mnalalamika nn? ukiwa rais lazima ujue kutumia fedha, haijalishi kama unajua kuitafuta...thats what jk is trying to show his voters....bravo jk...u are killing yor ccm and making a good path for cdm.
   
 12. m

  malimwengu Member

  #12
  Nov 8, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kudadaddadadeki mimi nilifurahia sana ile dhifa kuoneshwa katika tv, kilichonifurahisha ni kujua kuwa kumbe charles ni mtoto wa mfalme. Hongereni tbc kazeni uzi hapo hapo. Prince charles mwana wa mfalme. Hongera amina mollel ulifanya kazi nzuri sana mpaka ukaishiwa pumzi, wewe kweli uko fiti na unaijua kazi yako hureeeeeeeee tbc, hureeeeeeee amina mollel
   
 13. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #13
  Nov 8, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Craaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaap hakuna kitu hapa na sio dhifa ya kwanza kuonyeshwa kwenye tv, huu ni wivu wa kike !
   
 14. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #14
  Nov 8, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wivu wa kike cdm utawamaliza, kumbe maneno yako hayo yote ni kwa vile JK , ila angekuwa slaa poa tu, subirini na nyie 3025 mtafanya
   
 15. COMPLICATOR2011

  COMPLICATOR2011 JF-Expert Member

  #15
  Nov 8, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 255
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 33
  maana hasa ya kuonyesha ile ilikuwa nn?
   
 16. JS

  JS JF-Expert Member

  #16
  Nov 8, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kuna kitu inaitwa ETIQUETTE ambayo inapaswa itumike sana katika dhifa za kitaifa kama hii ya jana. lakini viongozi wetu wengi hawana hiyo kitu kabisa ni kuvurunda tu mpaka unaona aibu mwenyewe utadhani ulikuwepo kwenye eneo la tukio. so embarrassing. wawapeleke kozi ya masuala haya au wakupe hiyo nafasi mshkaji upunguze makali ya maisha uwafundishe mpaka waone aibu wenyewe. tunaanzia na bogus Salva
   
 17. The Stig

  The Stig JF-Expert Member

  #17
  Nov 8, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 80
  Unajua uko makini sana!

  1. Hilo la mtangazaji mbabaishaji lina-apply sana TBC/ Daily News etc. Jana kwenye Jahazi ya Clouds, Kayanda alikuwa anaongea na m-TBC mmoja alieenda London kwenye Miss World. Kwa kuanza Kayanda alijitahidi kuset background kuwa mrembo wetu alijitahidi sana lakini alianguka kutokana na upinzani mkubwa. Alikpopewa m-TBC fursa ya kuongea akaanza kumponda yule mrembo wetu utafikiri wamenyan'ganyana bwana!

  2. Kama ni kweli Salva aliongea katikati ya toast za wakubwa, basi amekosea sana.

  3. Hilo la kukosa discipline na watu kuzunguka zunguka utaliona kwenye kila tukio kubwa linalowahusu waswahili kama waratibu. Iwe ni uapisho wa waziri, kutoa kombe la mashindano, kote utaikuta hii kitu.
   
 18. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #18
  Nov 8, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  wasiishie hapo tu. Tunatakiwa tuende mbali zaidi mpaka kwenye cherekochereko kupitia TBC1 ambapo huonyesha watu wakila wakati sisi tuna njaa.
   
 19. m

  mama kubwa JF-Expert Member

  #19
  Nov 8, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 2,410
  Likes Received: 1,968
  Trophy Points: 280
  hata mie ndicho kilochonishangaza maana hata hotuba ya raisi haikusikika sasa cha muhimu ilikuwa ni ile michuzi waliokuwa wanajichana?
   
 20. Crucial Man

  Crucial Man JF-Expert Member

  #20
  Nov 8, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 3,277
  Likes Received: 470
  Trophy Points: 180
  mkuu umenena,yani pale palikuwa ni vurugu tupu,utazania graduation ceremony ya chekechea kulikuwa hakuna table manners kabisa.sijawai shuhudia state baquet yenye vurugu ka ile.it was shamefull.
   
Loading...