Unajua uko makini sana!
1. Hilo la mtangazaji mbabaishaji lina-apply sana TBC/ Daily News etc. Jana kwenye Jahazi ya Clouds, Kayanda alikuwa anaongea na m-TBC mmoja alieenda London kwenye Miss World. Kwa kuanza Kayanda alijitahidi kuset background kuwa mrembo wetu alijitahidi sana lakini alianguka kutokana na upinzani mkubwa. Alikpopewa m-TBC fursa ya kuongea akaanza kumponda yule mrembo wetu utafikiri wamenyan'ganyana bwana!
2. Kama ni kweli Salva aliongea katikati ya toast za wakubwa, basi amekosea sana.
3. Hilo la kukosa discipline na watu kuzunguka zunguka utaliona kwenye kila tukio kubwa linalowahusu waswahili kama waratibu. Iwe ni uapisho wa waziri, kutoa kombe la mashindano, kote utaikuta hii kitu.