Sio Sahihi: Waasia na Wamatumbi Wote Kuitwa Watanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sio Sahihi: Waasia na Wamatumbi Wote Kuitwa Watanzania?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by DSN, Aug 7, 2011.

 1. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #1
  Aug 7, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Kuna kitu ambacho Mwalimu alikijenga kwa Watanzania ambacho kwa zama na nyakati za kizazi cha sasa uwa napenda kusimama pembeni dhidi ya misimamo yake hiyo Baba wa Taifa.Nakubali kwa nyakati zake hayo mambo yalikuwa sawa,na kweli kuna waasia [Waarabu na Wahindi] haswa wahindi walimsaidia Mwalimu katika ujenzi wa Taifa hili,kupitia chama cha ukomozi cha TANU.

  Uwanapata shida sana najiuliza maswali ambayo sina majibu lakini na hakika yana majibu.Katika watu huwa navutiwa nao katika historia na masimulizi ni Mzee Karume,yasemakana bahada ya kupata uhuru Zanzibar Karume alishiriki katika jambo ambalo kama ni kweli hakika Mzee huyu alikuwa Jasiri na Mzarendo wa Kweli juu ya Uafrika wake [Braveness].Alifika wakati kwa mujibu wa masimulizi kuwa kulikuwa na waasia na waarabu ambao mabinti zao waliwapend waafrika lakini kwa itikadi ya ubaguzi walio nao hawa ambao wanajiita ndugu zetu waligoma kuwaoza watoto wao kwa Wazanzibar wenye asili ya kiamatumbi [yaani weusi].Inasikika kuwa Karume chini ya usimamizi wake alihakikisha kuwa kama unamchumba na mmekubalina basi kama huna maali ya kulipa serikali itakulipia.Kuna muusia mmoja kusikia hilo akapandisha maali kubwa hili serikali ishindwe kulipa lakini ilipofika kwa Karume akasema mlipeni na Mzee akalipwa pesa hizo mmatumbi akavuta mtoto wa kiasia.Hakika kama hili lilikuwepo Mungu amlaze pema peponi kamanda huyu alitimiza kazi yake kuona kama sote tu wanajamii tunastahiki kuishi pamaoja kwa kuoleana na kuzaliana kwa uwiano.Sio mwingine akawa bingwa wa kuolea wakati mwingine yeye kwenye kuolewa aka hataki kusikia.

  Kwa Tanzania bara Mwalimu aliwaheshimu sana hawa marafiki zake wahindi,lakini kama kiongozi hakutengeneza miongozo ya kujua kuwa kwa kuwajumlisha hawa ambao ni [wachache] minority kama kundi kubwa sawa alivyowaona Watanaznia wabantu [Makabila tofauti tofauti] kuwa kitu kimoja kulifanyika makosa.Japo sio zama za kuhesabu makosa ila ni kipimo cha kuona tatizo lilianzia wapi.

  Wahindi na waarabu kwa sababu ya uchache wao ambao kihaiba na tamaduni ni tofauti sana na Watanzania wabantu,lakini Mwalimu akawaweka ndani ya mizani moja kama Watanzania,akasahau kuwa hawa wana jadi zao na tamaduni zao,pasipo nguvu ya dola na misimamo ya kitaifa hawa watu wataibuka na mataifa yao ndani ya Taifa moja.

  Alichokifanya karume kama kweli ni kweli,basi ukienda Zanzibar uanweza ukaona hata jinsi hawa watu Waasi na Wahindi wanavyoishi na Wazanzibar.

  Mwalimu aliwapenda akafikia na yeye wanampenda,lakini kihalisia hakuna lisowezekana la kuunda TAIFA moja ambako watu wanaishi kama kama ndugu.Ni nani asiyejua kuwa zunguka Nchi nzima miji mingi mikubwa na midogo ukiingia kwenye mitaa ushangai kusikia UHINDINI.Kwanini kulikuwa na mitaa kama hiyo na Serikali kuhalalisha matumizi ya majina hayo ambayo yaliendeleza kuunda UBAGUZI na hivyo kuendelea kujenga viota vya kuhalalisha mataifa Matatu ndani ya Taifa moja, Uhindini wanaishi Wahindi na Waarabu.

  Kwa kuishi kwao pamoja waliendeleza tamaduni zao wao kama wao binafsi badala ya kuunda ushirika na watanzania wengine hivyo kuunda jamii inayozaliana kwa kuoleana. Japo sio lahisi kwa mtu wa kawaida kujua madhara ya watu hawa kuishi daima sehemu moja wao wote wakiwa wamejikusanya ndani ya eneo moja kwa miaka nenda rudi toka wengine wetu atujazaliwa mpaka tumezaliwa wameendlea kuishi huko vizazi na viziazi,.

  Hivyo wamezidi kuishi kiasia zaidi na sio kitanzania ndio maana nikasema mataifa mattu ndani ya Taifa moja.Kiuishi kitanzania ndio huku leo mtu yoyote ruksa kuoa mchaga,mpare,mngoni,mkurya,msukuma ama mkwele yote sawa. Lakini Kamwe sio lahisi ama sawa kusikia mgogo kaoa Muhindi,au Mwarabu kaolewa na Mkurya,ila kwa nadra nayo ni kidogo sana tena patakuwa ilikuwa zaidi ni msukumo wa kiuchumi [interest] ukasikia Mwarabu kaoa Mzaramo au Mfipa au Msukuma.

  Lakini hiyo ndio Tanzania iliyotakiwa kujengwa ya matabaka mpaka kimakazi,Mtaani kwangu naishi na watu wa kutoka makabila kibao Tanzania lakini utofauti huo haupo kwa kuwa tunajiona sisi wote tu wamoja ikifika wakati wa kusali wakristu watakutana kwenye makanisa yao waislamu watakutana kwenye misikiti yao kila mmoja akitokea mitaa tofauti.Lakini si kwa wenzetu hawa kwani wao kila kitu si nyumba zao za ibada au biashara zao zote ni eneo moja tu ambalo ni wao wenyewe.

  Sio lazima tufanane na Wingereza au Marekani,laizma tuunde Taifa linalofanana na sisi tulivyo,Taifa ambalo litampa nafasi ya kijana wa Kitanzania Mmatumbi kujumuika na kijana wa kihindi au kiarabu pasipo kujali dini wala kabila.Na kutoa fulsa ya kuunda taifa ambalo ushirikiano wa kiuchumi na muingiliano wa kinasaba utajenga Taifa la watu wa Taifa moja.Ifike Muhiindi au Mwarabu aishi tegete au Mbagara lakini ukifika wakatti wa kusali atatoka uko aende akakutane na wahindi wenzie jamatini kisha aludi kwa Watanzania wenzie anaoishi nao mtaa mmoja.

  Wapewe ajira za kulitumikia Taifa kama Polisi,Madaktari,Walimu,Manesi,Maofisini na shughuri nyingine zote kama Watanzania wengine.

  Na tabia ya hasa wazee wetu wengi waliowatendaji Serikalini ya kuwanyenyekea Wahindi na Waaarbu ,huku wakiiba Mali na fedha ya umma,kwa visingizio kuwa huwa hawatoi siri matokeo yake wakisha mwaga kwenye skendo ya wizi wa umma akiendea pesa yake kwa Muhindi au Mwarabu anazimwa tunaishia kuwaona baada ya muda wamepatwa na kiharusi [stroke].

  Wafanyakazi walio wengi kwenye Mashiriki na ofisi nyingi za Serikali wanajua jinsi wanvyotumika na hawa jamaa [Use and abuses] wanaweza kuwa wema sana ukiwa madarakani,ngoja ustaahafu ama upigwe chini uwaoni,hata vile viitu walikuwa wanakupa bure kukufanya ujisikie na wewe ni mteule kufuri linafungwa na hawakutambui tena.Wako tayari wakutafutie Dada yao feki wakupe akubuludishe wakifanikiwa mikakati yao kupitia kwako wanaondoka na kiburudisho chao walichokuletea ukajiona mteule.

  Yote haya ni upofu wa Watendaji baadhi ya Watanzania na tamaa zao za kutaka pesa za umma pasipo kujali utu wa wengine.Na kwa kuwa waasia kwa tabia ambayo iko wazi kimataifa ni watu wanaopenda sana ushawishi kibiashara kwa kutumia pesa na rasimali yoyote ile [Lobbing].Kwa Wahindi kidogo Waswahili uwa wanaambulia japo lakini wakikumbana na waarabu hapo ndipo viharusi huwa vya kufikia tu,.Kapiga deal au mchakato wake na Mwarabu,na kwa hofu kaacha fedha/hela kwenye akaunti ya mwarabu upepo upite Mchakato umejurikana kibosile kazi hakuna,lakini kesha vuta pesa yake anaenda kuchukua pesa ya kwa Mwarabu,.Mwarabu anamuuliza ulimwachia nani?.Na kwa kuwa ni za kuibia umma adhabu yake inayofuata hana Pesa [Mkwanja] na kazi alishafukuzwa na hawezi kumshitaki Mwarabu kwa kuwa ilikua Mchakato [deal] ghafla Mzee kashikwa na Kiharusi [Stroke] sababu ya dhambi ya mawazo.

  Kwa sababu ya kutokuishi na hawa jamaa kimazingira wakati mwingine wakimsogelea na kumzunguka Mtanzania mmatumbi anapumbazika na hawa jamaa anajiona kama tofauti na kujiona mteule kwa kuwa ni nadra kuwaona katika jumuiko la kila siku la kitanzania kama Misibani, Makanisani, Shuleni, Hospitalini na Mitaani Kwetu.Linakuwa ni tatizo la kisaikolojia zaidi la kuona kama mtendewa kabalikiwa kwa kuwa na ukaribu nao.

  Kwa vijana wengi wa Kitanzania ukiwaweke binti wa kiarabu au kihindi na binti wa kizungu waambie wachukue mmoja wasipendi one day out na mmoja kati ya hao nina hakika wengi watakimbilia kwa Muhundiau Mwarabu pamoja na kuwa kuna Mzungu.Kijana wa kitanzania ana hakika ya kuoa ama kuwa na mahusianao na binti wa kizungu anayetoka ulaya kwa asilimia mia [100%] kuliko binti wa kihindi au kiaarabu anayetoka KARIAKOO Dar es Salaam.

  Kama Serikali inafikilia kuondoa tofauti hizo ni jukumu la mtu binafsi hakika sio kweli,ni jukumu la Serikali ya CCM kutengeneza mikakati na mbinu zenye kuwalazimisha watu hawa kutapakaa kwenye maeneo mabalimbali ya Watanzania wengine,na kuhakikisha hawalundikani pamoja na kuwapa mwanya wa kujitenga na jamii ya Watanzania wengine.Na kama kuna walio raia wa kigeni yaani wanaotoka India na Urabuni Serikali iwarudishe kwao.Na sasa kuna ujio wa Wasomali ambao ukienda maeneo ya kulasini jijini Dar es salaam wameanza nao kuunda Taifa lao [Somalian Kingdom].Kabla ya ujio wa kitambulisho mtaani tuvunje kwanza Mataifa hayo Matatu ndani ya Taifa moja.

  Japo kuna baadhi ya Wahindi wameishi kama Watanzani wa kweli kama Profesa ISSA SHIVJI na hata Rajan aliyekuwa Mkurugenzi wa Haki Elimu sasa Mkurugenzi wa TUNAWEZA.Kwa kutaja hao ni wachache tu.

  Je tunahitaji utafiti wa kina kuona ni jinsi gani tutaunda Taifa moja kwa kuondoa tofauti ya kihaiba kati ya Wahindi na Waarabu dhidi ya Wamatumbi yaani Watanzania.

  Nawasilisha
   
 2. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #2
  Aug 7, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Najibu hapo mwisho kwenye swali. Ndiyo, tunahitaji utafiti.

  Ngoja niendelee na kutafakari.
   
 3. M

  Mkandara Verified User

  #3
  Aug 7, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  DSN,
  Mkuu wangu kusema kweli nimeshindwa kukusoma hadi mwisho lakini inasikitisha sana kuona jinsi ulivyopoteza mwelekeo na imani kwa sababu ya rangi ya ngozi yako. Na hakuna kitu kibaya zaidi ktk maisha ya mwanadamu kama kutumia inferiority complex kujazia mapungufu ya matukio na vitu. Umefikia hadi kumsifia Karume kwa kulazimisha waarabu/wahindi kuolewa na waafrika lakini unapinga waarabu/wahindi kuwalazimisha mama zetu kutembea nao kimwili (utumwani). Neno kulazimisha haliwezi kujengewa nguzo na mapambo lionekane la ujasiri hali lipo ktk maudhui yake yale yasikyokubalika upande wa pili..

  Labda nikuulize wewe, Je ukisema huwezi kuoa mke asiyekuwa kabila au dini yako utakuwa mbaguzi? Na itakuwa vipi ukilazimishwa kuoa mke usiyempenda na kwa sababu hizo hizo! Tatizo lako mkuu wangu unashindwa kuzitenganisha dunia hizi mbili.. wakati ule ndoa zilikuwa hazina mapenzi, ndoa zilikuwa ni swala la kifamilia hivyo mume au mke walichaguliwa na kupitishwa na wazazi, Haikuwa kwa waarabu na wahindi peke yake bali hata makabila yetu haikuwa rahisi kuoa nje ya kabila au dini yako. Huwezi kutoka huko Mbeya ukategemea kuoa mke Mmachame kirahisi na ndivyo ilivyokuwa kila kona ya dunia. Lakini mbona mabadiliko yametokea hapa duniani bila utumiaji nguvu kama wa Karume, leo unaweza kuoa Mmachame, mwarabu, mzungu na kadhalika na wala Karume hakuwa sababu, mfano au chanzo cha mageuzi haya.

  Sasa ukitumia enyenyekevu wako leo ktk maswala ya kijumuiya ukajaribu kutafsiri hali za zamani na sasa, utachekesha mkuu wangu na ndio mwanzo wa kushikwa kichaa bure. Waarabu na Wahindi ni Watanzania ambao wamejikita ktk biashara. Na ktk biashara zipo loopholes kama za mkulima ktk kuiba mbegu za mahindi, kuchuma shamba la jirani na kadhalika, yote haya yanategemea na mfumo wa sheria unaowaongoza.

  Kuwahukumu waarabu na wahindi kwa biashara haramu wakati sisi wenyewe ndio tunaitaka haramu hiyo sidhani kama tunatumia hekima. Na labda nikwambie tu kwamba mkeo au mumeo anapotembea nje ya ndoa, huwezi kuwalaumu wanaotembea naye isipokuwa mkeo/mmeo ambaye anajua fika yupo ktk ndoa na hatakiwi kufanya zinaa. Dunia imebadilika mkuu wangu sio ile ya kisasi, ya jicho kwa jicho bali ni kujitambua umesimama wapi maanake siku hizi ukimpiga mkeo hata iwe kwa zinaa aloifanya unakwenda ndani wewe. Ni swala la yeye kuinua simu na kupiga 911 ooh! 999 na utalala lupango..

  Ndivyo ilivyo ktk utumishi wa serikali yetu, kama wapo Watanzania ambao kwa uroho wa fedha wapo tayari kuifisadi nchi yetu, basi hatuna sababu ya kuwaadhibu waarabu na wahindi isipokuwa kuelekeza lawama zetu kwa jamaa zetu wanaokubali kuihujumu nchi yao. Kuwatazama waarabu na wahindi kwa rangi zao ni makosa makubwa snaa na pengine jaribu kuwahukumu kwa makosa ya kila mmoja wao. Fisadi anaweza kuwa mhindi, mwarabu, Mmatumbi na kadhalika.
  Hata hivyo ukisha waondoa waarabu na wahindi, huyo Mmatumbi atabinjuka wapi usiku wa manane kabla hujasiki - Miji miji hiyo kamata miji!..
   
 4. MrFroasty

  MrFroasty JF-Expert Member

  #4
  Aug 7, 2011
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 702
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  @DNS
  Kazi ya watanganyika ni kukaa na kuanza kujadili vitu wasivyofahamu.Hakuna jema alilofanya Karume katika suala zima la kulazimisha ndoa.Bado nafikiria ndoa ni suala la wapenzi wawili kufanya maamuzi hayo.Kama kuna utamaduni ambao wa kiarabu au kihindi kuolewa na waafrika, sidhani kama kuna umuhimu wa sie waafrika kulazimisha lazima tuwaowe wao.

  Hio itakuwa kwangu ni upuuzi wa kijamii ndani ya kabila hilo linalokataa kuolewa kwasababu za kibaguzi.Lakini haya sidhani kama yamebadilika, waislamu bado wanabagua mtoto wao kuolewa au kuowa mtu asie na dini sawa na yao.Sina uhakika kwa wakristo kama ni hivyo, lakini hili lipo hadi leo na hadi mimi mwenyewe muislamu nitahakikisha binti yangu hailowi na mtu asie muislamu.

  Sasa ukisema aje Nyerere au Karume alazimishe lazima binti yangu aolowe anavyopenda yeye...Mkuu tutafika mbali !
   
 5. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #5
  Aug 7, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Unazungumza vitu gani wewe DSN, mbona hueleweki?
   
 6. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #6
  Aug 7, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Kwa masimulizi ya wazanzibar kuwa waarabu na wahindi waliozwa na karume sio kwa lazima bali ni wale waliokuwa wakiingia kwenye mahusiano lakini wanapofikia kuataka kuona kwa kuwa mmoja ni mmatumbi na mwingine ni muaasia basi kunaibuliwa vikwazo ambavyo ndio karume alivyosiamamia kama wamependana basi kama ni mahari basi dola italipa.

  Pia tambua wao kujua loophores basi na kutumia basi ndio kuwa waanzilishi wa kuhujumu jamii,usiahalalishe matendo ya kiuni ya wizi kuwa ndio mfumo wa maisha ya Watanzania.Unajua kuwa wizi ni kosa la jinai.usialalishe matendo ya machafu ambayo yamekuwa ni chachu ya vitendo vya rushwa kwenye jamii.

  Mkandara si vyema usiitete na kuhalalisha mambo yalipolekea kutufikisha hapa kwa kujua upungufu wa mifumo ya kusimamia jamii kwa faida ya wote wengine wakajinufaisha.
   
 7. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #7
  Aug 7, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Wadau hakulazimisha ndoa halicholazimisha ni ni familia zilizokua zinapinga ndoa,alihakikisha wale wote walioafikiana kama ni Mmatumbi amependa na binti wa kiasia basi waoane pamoja na tofauti ya rangi zao.Lakini kwa kuwa famiia za waasia kwa kusimamia umoja wao na misimamo yao wengi wao walipinga ndoa za mchanganyiko huo.Ila kwa kuakikisha waliopenda wanaoana ndipi Mzee karume napata muona huo wa simullizi hizo kuingilia kati na kuakikisha kuwa watu hawa wenye nasaba tofauti wakiona hata kama ni kwa usimamizi wa Serikali.
   
 8. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #8
  Aug 7, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Nazungumzia tabaka,msilo taka kulitambua na kujua kuwa lipo Tanzania.
   
 9. C

  Choveki JF-Expert Member

  #9
  Aug 8, 2011
  Joined: Apr 16, 2006
  Messages: 448
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Nadhani unachanganya vitu viwili hapo, kwani kama wao ni watanzania wenye asili ya kiasia basi bado atakuwa anafuata mila za kiasia zaid na wala si za kigogo au kimakonde! We fikiria, je unaweza mlazimisha mngoni aache mila zake za kingoni halafu afuate za kichagga?- Kila krismass wachagga wataongozana kwenda kula krisimasi Moshi, je utamlazimisha Mngoni akalie krismasi Songea ingawa si kawaida yake? Je kutokana na kuwa Wachagga/ watu wa Tanga, wazaramo wanaume nk wao kutahiri ni lazima je utaanza kuwalazimasha wajaluo, wahaya, wanyakyusa na wengineo wasiokuwa na utamaduni wa kutahiri wanaume watahiri ili tu waoneshe wanachanganyika? wakati si jadi wala utamaduni wao- Inabidi ufahamu kuwa hakuna utamaduni wa Tanzania bali wa Kitanzania ambao unatokana na jumuiya za watu na mila tofauti zinazoifanya iitwe Tanzania!

  Nishaona matunda ya miungano (ndoa) za wahindi na wabantu au waarabu na wabantu, pia waarabu na wahindi nk na si kitu cha ajabu, na pia nishakuwa na marafiki walotokana na ndoa hizo!
  Nakubaliana nawe hapo kuwa tuunde taifa la umoja, lakini kutokana na hoja zako sijui kama formular yako itaweza kufanisha hili taifa la umoja! Mambo ya vijana wa kimatumbi kujumuika na na wa kihindi yatatokana na upendo utakaoletwa kitaifa na siyo lawama za baadhi ya watanzania, mfano kila leo watu wanalalama kuwa wahindi na waarabu wanahujumu taifa au wanahonga viongozi
  Mimi nimesoma na nimefanyakazi na wahindi na waarabu watanzania na walikuwa kulikuwa hakuna tofauti na mtanzania w=mwingine yeyote! Tatizo nilionalo hapo ni kuwa wengi wao siku hizi wanaamua kujiajiri au kuajiriwa na wenzao kutokana na mfumo wa uajiri wa sasa!
  Sasa kama viongozi wetu wanajipelekesha wenyewe kwa waarabu na wahindi utawalaumu waarabu na wahindi?
  Sasa Mhindi au mwarabu ataenda kwenye msiba wa mbantu ambaye hamfahamu ili tu naye aonekane? Mbona misikitini wanakuwepo na wanakaa sambamba na wabantu wengine? Kitu kinachosababisha wasiwepo kanisani ni kuwa wahindi na waarabu ambao ni wakristo si wengi Tanzania, hivyo inasababisha kanisani wasionekane kwani siyo nyuma zao za ibada!, Je wabantu wanaonekana kwenye mahekalu ya mabuddha au kwenye sherehe zao za dewali?
  Wasomali wamekuwepo Tanzania tangia enzi na enzi kama vile watanzania (kutoka Tanga) walivyokuwepo kule Somalia (maeneo ya kismayu) tangia enzi na enzi. Hiyo kusema kama wanaunda taifa lao sina uhakika, ila je huko Marekani au UK wanastushwa na matawi ya CCM kila kona? Au matawi ya Umoja wa watanzania waishio hizo nchi?
  Hao akina Shivji na akina Rajan wapo wengi tu sema kwa sababu hawapo kwenye viombo vya habari ndiyo maana wewe hujawafahamu!
  Tunachohitaji si utafiti bali upendo wa kweli kwa raia wote bila kujali rangi, dini, kabila au jadi zao!
   
 10. D

  Deo JF-Expert Member

  #10
  Aug 10, 2011
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 1,191
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kwa nini maeneo yote yenye waarabu wenyeji hawaendelei? Angalia Tabora, Shinyaga Sigida, nk kila sehemu ampapo waarabu wapo, hasa kwenye vijiji vyao wenyeji ni maskini wa kutupwa. Kwa nini? NIna jiuliza kwa nini lakini?
   
 11. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #11
  Aug 10, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Huwa wanachakaza maeneo ,walipo waarabu wanao wazunguka huwa maskini wa kutupwa!
   
 12. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #12
  Aug 10, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Asilimia mia hili ni sahihi tembelea maeneo yote hayo,utaona,kidgo siku hizi Wanyantuzu wamebadilisha muonekano wa kabila la wasukuma baada ya kujituma kwa nguvu.Lakini makabila mengi ya mikoa hiyo uliyotaja mengi yako chakali kwa kutawaliwa na waarabu.

  Kwa kuongezea nenda Pwani kama Kisalawe,Bagamoyo,Tanga,Kilwa,Mtwala na Lindi kote hakuna kitu watu wako choka mbaya hawana cha maana kama jamii ya waelevu wenye kupenda maendeleo na kukubali kusomesha watoto wao.
   
 13. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #13
  Aug 10, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145

  Haya choveki ndugu zako wanapeana mafuta wao kwa wao unasemaje hili msome mdau huyu anaitwa Edward Teller [BOFYA HAPA]

  Pia kinachojili wingereza juu ya ndugu zako wahindi nini unaweza kutwambia [BOFYA HAPA]
   
 14. U

  Userne JF-Expert Member

  #14
  Aug 10, 2011
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 895
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kuna haja katiba ieleze kwamba Tanganyika kwa Watanganyika Asilia. Hatuwabagui ila hawawezi kukomba haki zote za Watanganyika Asilia, hata Mungu itampendeza maana yeye ndie Muanzilishi wa Taifa, Rangi, lugha na Jamii. ukiona nyani mweusi na waindia ni muhindi!
   
 15. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #15
  Aug 10, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Ndio maana hawaishi kusema maswala ya dual pass.Jambo hilo liwe historia kwa Tanzania.
   
 16. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #16
  Aug 11, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,192
  Likes Received: 1,914
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  Ni kweli tupu mkuu! hakuna haja ya utafiti hata nyani ya india ni muhindi tu! daah. Wao ndio wabaguzi Wakubwa, manake hatuwaoni huku uswazi, vijiweni, vibanda vya gongo, kuchoma mkaa, segerea! hivi hawa ni vips eeh! utafikiri nchi hii wamerithishwa na baba zao! lazima wavune walichopanda!
   
 17. NGUVUMOJA

  NGUVUMOJA JF-Expert Member

  #17
  Aug 11, 2011
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,353
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Hii thread imejaa UBAGUZI wa rangi haitufai Watanzania jana, leo wala kesho.
  Mtoa mada sio tu uwezo wake wa kufikiri ni mfinyu lakini pia hata lugha bado inampiga chenga loooh!!!!!!
   
 18. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #18
  Aug 13, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Umeskia ya Simon Company UDA na wahindi wako unaowatetea ngoja mwendelee kuona hivyo ni maigizo na ubaguzi,time will tell bro.Pole yako mdau hata hivyo ID yako inaonyesha uwezo wako ulivyo mchache kwa kwenda mbele utaitwaje NM aibu unajua kimoja mengi utajuaje wakati upeo wako ni mmoja.

  Mhindi kwa jina Yusuph Manji kapewa eneo Uwanja wa UDA H 12 kwa shillingi miliion 22 kwa mwaka wakati Simion [Kisena] mmbantu mwenzio kapewa H 3 kwa shillingi millioni 200 na kitu kwa mwaka.Bado uanajiita Mtanzania manji ajiite nani bro.Hiyo ni taarifa ya leo sio jana.Kama umeangalia kipindi cha star TV live kongamano la mahojiano ya Wamilki wa Simion Group pamoja na Wananchi.

  Wakati huo huo UDA wamekopa benki kununua mabasi wakashindwa kulipa wakadanganywa na mdosi wakaweka kuponi kiwanja kwa mhindi na kisha kwenda kulipa deni uanapata picha gani wewe unayesema huo ni ubaguzi,umelala NM vipi wamekuajili nini?Japokuwa siko hapa kujumuisha wahinid wote ila tunazaungumzia walio wengi.

  Taarifa hiyo ya matendo ya Manji na mwenzie Fida Hussein kuiingiza mkenge UDA ndio faida yako wewe mnaoendela badokushabikia upuuzi baada ya kuitoa Nchi matatizoni.

  Mungu atakisikia kilio cha wengi siku moja.Iko siku isiyo na jina.
   
 19. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #19
  Aug 13, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145

  Mkuu mkandara leo I hope umemsikia Simion Group Director Bwana Robert kajaribu kulia uzalendo wa Watanzania huko wapi, Mhindi kwa jina Yusuph Manji kapewa eneo Uwanja wa UDA H 12 kwa shillingi miliion 22 kwa mwaka wakati Simion [Kisena] mmbantu mwenzio kapewa H 3 kwa shillingi millioni 200 na kitu kwa mwaka.Bado unajiita Mtanzania manji ajiite nani Mkandara.Hiyo ni taarifa ya leo sio jana.Kama umeangalia kipindi cha star TV live kongamano la mahojiano ya Wamilki wa Simion Group pamoja na Wananchi.

  Wakati huo huo UDA wamekopa benki kununua mabasi wakashindwa kulipa wakalubunika kwa Mwekezaji wa biashara za Majengo na Viwanja Fidar Hussein wakaweka kuponi kiwanja kwa mhindi na kisha kwenda kulipa deni Benki,unapata picha gani wewe unayesema huo ni ubaguzi?Japokuwa siko hapa kujumuisha wahinid wote ila tunazaungumzia walio wengi.

  Taarifa hiyo ya matendo ya Manji na mwenzie Fida Hussein kuiingiza mkenge UDA ndio faida yao wote wasio taka kuamini kuwa tuna tatizo kubwa Nchini linalotaka lipatiwe ufumbuzi.I hope tumetoka kwenye Mafuta sijui huko mkuu unasema wale ni Watanzania Wamatumbi waliowanyima watanzania wenzao mafuta,ili wateseke wao na familia zao,acha niendelee kuitwa mbaguzi kwa kusema ukweli.Kisena [Simion] group analia kwani vita yake na Watanzania wenzie ni bomu la kibiashara nakumbuka hata Mzee Reginal Mengi alipata kupiga kelele mpaka wenye akili zao wakainglia kati kuona mchezo mchafu uanondelea juu ya Mzee huyo.

  Time will tell kuna mengi sna yanayokuja yanayohusiana na hawa nyie mnaowalazimisha kuwaita Watanzania wenzenu wakati wao hawawathamini ninyi, nanyi mnalazimisha kuwa wao nao mko sawa nao.Pole bro ila kila litakalojili kuanzia na kuendelea nitasema tupime wenzetu uzalendo wa Taifa lao Tanzania uko wapi.Ni kama huu wa kuikamua UDA mpaka inakuwa marehemu.
   
 20. M

  Mkandara Verified User

  #20
  Aug 14, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu wangu tatizo sio manji au hiyo Simion group bali tatizo ni sisi wenyewe.

  Kama umenisoma majibu yangu ktk mada ya Mustakabali wa Zanzibar na Seif Sharriff Hamad, nimeeleza wazi kwamba siku zote HARAMU humfuata MTUMIAJI.. Huwezi uwalaani wahindi waarabu kwa magendo na Ufisadi ikiwa sisi wenyewe ndio wapokeaji wa Ufisadi na magendo hayo. Manji ahawezi kufanya lolote pasipo Mmatumbi kwa nyege zake tumbo kuweka mikataba mibovu mbona hawaendi Rwanda au wanakimbia kwa Mugabe.

  Reginald Mengi alipiga kelele sii kwa sababu Manji alinunua Kilimanjaro isipokuwa Mmatumbi m,wenzake alimyima nafasi ya yeye kununua hiyo Hotel. Na wala sii swla la kuuliza watu kwa sababu tunajua fika kwamba Mtanzania atamwamini Mhindi au mwarabu ktk issue yeyote lakini sii Mmachinga mwenzake na sababu inajulikana. Mmachinga mwenzako atakuuza au kukuibia wewe kwa sababu UAMINIFU hatuna. Umaskini umeondoa kabisa imani ya kiroho na kuoteautajiri wa haraka..

  Wahindi na waarabu sii watu wabaya na wala sii kwamba wanatutumia isipokuwa sisi wenyewe ndio tunawartuhusu watufanye hayo.. Kwa hiari kama unavyotaka kudai hizo ndoa ndoa wakati wa Karume..Ni makubaliano baina ya mmatumbi na mwarabu/mhindi na mara zote sisi ndio hushika ukuta kisha tunataka kujitutumua kuwa wanaume wa kweli kwa visingizio vya kubakwa..Hatuna lolote!
   
Loading...