Naam, Snowhite! Samahani nimechelewa kuja kwenye diskashen, samahani!
Ndio, ndoa yangu ni changa (miezi 6) , lakini tumefahamiana miaka 7 sasahivi. Binafsi, I believe marriage can be one of the best experiences of your life kama wewe na mwenzako mmedhamiria kuwa na ndoa yenye raha, furaha, na mafanikio. Ndoa haiwezi kudumu mtu akiwa mguu ndani, mguu nje. Ndoa haiwezi kudumu kama hakuna upendo na heshima. Hata upendo ukipungua, kama bado unamheshimu mwenzako naamini kwamba mapenzi yatapanda pia. Life is a journey kwahiyo usitegemee honeymoon period iwepo kila wakati. Ndoa zote zitakuwa na matuta... ni kama barabara za bongo. Ukikuta matuta unashuka na kutembea? Unarudi ulikotoka au unasonga mbele? Ukiendelea kidogo zaidi utafika kwenye lami ambako ni rahaaaaa.
Ninachowashauri vijana wenzangu ambao hawajaingia kwenye ndoa au mahusiano ni haya:
-
Chukua muda wako kufahamiana na mwenzako. Usiharakishe mahusiano. Angalia stage mliopo katika mahusiano yenu, na si muda ambao mpo kama girfriend na boyfriend. Unakuta mtu anakuambia within mwaka mmoja anataka mfunge ndoa la sivyo uhusiano basi! Kwa uelewa wangu, mwaka mmoja hautoshi kumfahamu mtu kwa undani kabisa na bado mtakuwa hamjapitia "matuta" pamoja. Matuta ni muhimu kwenye mahusiano sababu unajua mwenzako atakavyoreact mkipata matatizo baada ya kufunga ndoa.
-
Jaribu kuwa marafiki kwanza, na kufahamiana na ndugu na marafiki wa mwenzako. Utaweza kuona jinsi alivyo na wenzake in his/her natural state, bila maigizo. You can judge a person by the company they keep.
-
Mambo ya pesa. Hii mnaweza kukubaliana na mimi au mkalipinga, lakini kina dada msiombe pesa wala kukubali kupewa pesa mapema kwenye uhusiano. Jitahidini kuwa independent kwenye haya mambo. Kutegemea pesa toka kwa boyfriend ni utumwa in a way, huwezi kukataa ombi atakalokutupia baada ya hapo sababu roho itakuambia una deni. Ukiwa na pesa zako Utakuwa huru zaidi katika mahusiano, na itakusaidia kuona ni mtu wa namna gani unae deal nae.
Kina kaka, msitangulize pesa ili kupata msichana unaemtaka. Utaishia kuvutia wasichana wanaokupenda kwa sababu ya pochi. Hata wakikuchoka hawatataka kuachana na wewe sababu unawapatia pesa.
Kwa kifupi, ndoa ni safari ya watu wawili. Tutakumbana na mengi njiani. Cha muhimu ni kusaidiana na kutoelemeana wakati wa safari. Hivi vituko vya vimada, mateso n.k. vinaonesha jinsi mke/mme hamheshimu wala kumpenda mwenzake. Kama wewe na mwenako mnaheshimiana na kupendana na mnataka uhusiano wenu usiyumbe, zingatia hizo point hapo ju, pamoja na ushauri toka kwa waliooa humu JF!
hope this made sense. it's very late inabidi nkachape usingizi.
PIPOOOZ....source 😡lara 1
jamani mada hii nimeidownload kwenye blog flani ya kulee, si wajua mambo ya blue monday ofic inaboa wakubwa wako kwenye vikao so kupass time tunazuga na ishu ka hizi.
nimecopy na kupaste as it is:
Chezea miaka hii ya kuchakachuana na kuchukuliana poa,Vimada kila kona kudadadekiiiii hujali maumivu ya mwenzio,Kilio cha Mwenzio na machungu ya Ndoa kila siku,Uvumilivu sawa hatujakataa ila Wakishatuoa wanatuona Vinyago vya Skauti ndani,Mkishaachana anajirudi atajirekebisha na mambo mengi potelea mbali uonekane Hujatulia kuliko JAKAMOYO Na Maumivu kisa ashajua unampenda wale wanaojifanya wana MAHABA Wako wapi?Ngumu kudumu kuna msemi 1;NIPENDE NITAKUPENDA,NITHAMINI NITAKUTHAMINI,UKINIZINGUA NAKUZINGUA SABABU HATUJAJA DUNIANI KUPATA KARAHA TUNATAKA RAHA.
hivi ndoa za leo ni haya yasemwayo hapa juu tu ama kuna the other side? wenye experience naomba mtoe views zenu jameni!!
HoneyBee my mdogo
hebu toa uzoefu wako japo ndoa yako bado mpya mpya give thm ur skills at least sare za jf women kitchen party ziongezeke mwayego!