Sio matusi tu alihamasisha kutoa sumu (kuuwa) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sio matusi tu alihamasisha kutoa sumu (kuuwa)

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by babykailama, Apr 3, 2012.

 1. babykailama

  babykailama JF-Expert Member

  #1
  Apr 3, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 241
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Nimehesabu na kugundua kuwa Mh. L. Lusinde katika speech yake ya matusi alitumia neno mimba au ujauzito yapata mara 15 kwa namna ya kukebehi (wanawake maana ndio hupata mimba) au kutukana (mf. tumesha watia mimba!) au kudhalilisha (mf. wenye mimba watafutiwe maembe mabovu).

  Pamoja na mashitaka mengine yatakayomkabili sasa mimi nawaita wanaharakati wote wanaojali uhai (pro- life activists) tumshitaki kwa kutishia maisha akina mama na kuwaogofya kupata mimba kwani yeye anawanyanyepaa na kuhamasisha umma Wajawazito kupewa vyakula vibovu (vyenye sumu) ili baadaye wafe! Wanaharakati hao ni wadau wote wa uzazi salama kama vile Utepe Mweupe, Uzazi wa Mpango, Wakunga, Madaktari, Wazazi , Wanawake na Wanaume wote wanaowajali Uzazi Salama na umuhimu wa mimba salama na kwamba sote tunapaswa kuiheshimu mimba kama chanzo na kitunza uhai wetu kabla hatujatokea duniani!

  Ushahidi : Waliokuwa katika kampeni na Video (kama itakubalika mahakamani).


  Ndg. Nape hivi CCM haiwezi kumsimamisha uanachama wake (pending masahili zaidi) ndg. Lusinde mara moja na kuomba msamahaumma kwa niaba yake. Kazi ya uenezi pia uinahusika na kueneza 'fair play', pia maadili ya Chama na kujali utu wa binadamu au siyo?
   
 2. A

  Aura reader Member

  #2
  Apr 3, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakuunga mkono Mkuu kwa hilo!!
   
 3. M

  MR.SILVER JF-Expert Member

  #3
  Apr 3, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yah,Jamaa nilipata tabu sana kumaliza kusikiliza theother half ndio nimemalizia leo.

  Ki msingi jamaa amedharau sana wake na wazazi wetu,ameongea vitu ambavyo ukiwa mwanaume huta subiri kusema wanawake wamshtaki balikuunganisha nguvu.Na hii nadhani si siasa tena hii ni hata watu wa CCM wanatakiwa kulaani maneno ya huyu jamaaa.Ni juu ya CCMpia kuonyesha wamejali wana nchi wake huyu jamaa asipoweza kuomba msamaha wadhati wamkane kwa kumvua uanachama kuonyesha wao hawako hivyo na hawa support maneno yake.
  Pia sisi na wanaharakati tulaani hii kitu kwa pamoja..........ni muda wa TZ kuheshimiana.
   
 4. t

  true dream New Member

  #4
  Apr 3, 2012
  Joined: Mar 29, 2012
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Thats right!!naamini tanzania ina watu wazima,wasomi na wenye busara!nimetaja mambo hayo kwani unapokua na busara,umeelimika na ni mtu mzima hutavumilia uozo wa maneno kama huo bila kujali itikadi za kisiasa!!ni aibu kwa chama na uongoz mzima uliopo madarakani!kwanza alitakiwa kukamatwa kwa kosa la kutukana hadharani!nashangaa vyombo husika vimetulia tu!naomba raisi kama mwenyekiti wa chama alitolee tamko swala hilo!MUNGU IBARIKI TANZANIA ,MUNGU BARIKI CHAMA CHENYE BUSARA!!
   
 5. babykailama

  babykailama JF-Expert Member

  #5
  Apr 3, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 241
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mama Ananilea Nkya nakusubiri tuyaweke chini katika maandishi haya tushughulike na huyu mzee ambaye naona bado hata hajastuka ni kama yuko usingizini hajui yatakayompata.
   
 6. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #6
  Apr 4, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,726
  Likes Received: 1,633
  Trophy Points: 280
  kasamehe tu aka, ka magamba kwani akana akili kabisa, hata wazazi wake kawazalilisha. Aka ka kichaa ka kuzaliwa mwisho wake ni miaka miwli tu.
   
 7. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #7
  Apr 4, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Kutokujua sheria kwa Lusinde kwa kisingizio cha elimu hakumsababishi yeye ashindwe hata kutambua misingi ya utu ambayo ndio nguzo kuu ktk familia zetu za kiafrika. Lusinde anastahili adhabu ili iwe funzo kwa watu wenye tabia kama hiyo ya kudharau kina mama. Naunga mkono hoja.
   
 8. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #8
  Apr 4, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,828
  Likes Received: 10,134
  Trophy Points: 280
  Laiti akifa leo...sijui atakua mgeni wa nani
   
Loading...