Sio kweli kuwa mwanaume anaweza kupata hedhi

Sio kweli kuwa mwanaume anaweza kupata hedhi

Kuna hadithi ya kweli kuhusu wanaume kuingia mwezini au kupata hedhi ukiachana na porojo za popoma.

Kuna sehemu moja Kijiji au mji ambao ulikuwa na wakazi wengi ambao shughuli yao kubwa ya kuendesha uchumi na maisha ni kilimo cha mpunga.

Basi katika hilo eneo kulikuwa na jambo ambalo si la kawaida ambapo wanaume wakubwa na watoto wa kiume wa umri zaidi ya miaka 9 na kuendelea ilikuwa ni kawaida kwa wanaume au watoto wa kiume kukojoa damu.

Kutokana na hali hiyo ilipelekea wale wanaume ambao hawakojoi damu kuonekana kwamba wao ni tofauti, wengi ambao hawakojoi damu walikuwa ni wageni ila walipokaa muda katika ule mji baadae na wao walianza kukojoa damu.

Mji ulijulikana kama mji wa wanaume wanaoingia hedhi.

Kufupisha hadithi ni kwamba wale wanaume na watoto waliokuwa wanakojoa damu walikuwa na magonjwa ya kuambukizwa ambao unaitwa Bilharzia/ schistosomiasis au kichocho na ulikuwa unaambukizwa kupitia maji kwa wale wakulima wa mpunga wakati wanalima kama tunavyojua kilimo cha mpunga kinalimwa kwenye mabwawa na majaruba. Vimelea vinatokana na watu wanaokojoa kwenye maji na wanaotumia maji hayo kuogelea au kucheza ambao ni watoto wanakua katika hatari ya kuambukizwa kichocho ambacho kinabebwa na konokono. Pia wakulima wanaopalilia, kulima au kupanda mpunga.

Hiyo ndio hadithi ninayoifahamu kuhusu wanaume wanaoingia hedhini

Waliosomo Tropical medicine au communicable disease wanaifahamu hii story.
 
Ngoja waje, dada yao mkubwa Dr. Mariposa atawapiga tafu kwa hoja nzitonzito.
Hapana mwanaume hapati hedhi ila wakati mwengine homons zake hua zinabadilika na kupata dalili sawa na zile dalili za period ya mwanamke, mood swings, angry, low libido, headaches, n.k, wanaita Man Period.
 
🚮🚮
 
ELI COHEN tia neno hapa, na wewe huwa unapata "Man period"??
 
Back
Top Bottom