Bueno
JF-Expert Member
- Aug 16, 2022
- 34,605
- 59,744
Unajua kuna wasomi wamesoma mpaka Masters PhD ila cha kushangaza mtu huyu anapoambiwa jitambulishe anaanza kwa kusema "kwa majina ninaitwa........" kaka na dada zangu sio kwa "kwa majina" ila unapojitambulisha kwa Kiswahili sahihi unatakiwa useme "kwa jina ninaitwa......" kisha unataja jina lako kamili kama lilivyo lote.
Unaposema "kwa majina ninaitwa...." maana yake unatakiwa utaje majina yako tofauti tofauti yaan ukisema "kwa majina ninaitwa...." basi taja unaitwaje kwa majina tofauti tofauti.
Mfano: kwa majina ninaitwa John Pius Chilangali, John Pius Fransis Chilangali, John Pius Fransis Joseph Chilangali na John Pius Fransis Joseph John Chilangali.
Hayo yote ni majina yako kwa mnyumbuliko tofauti tofauti lakini unapotaja jina moja kamili unatakiwa kusema "kwa jina ninaitwa...." kisha taja jina lako lote yaan jina kamili John Pius Chilangali. Ishia hapo.
Nimesikitika sana nimesikiliza Redio moja wasomi wenye elimu kubwa tu eti wanasema "kwa majina ninaitwa...." kisha anaishia kutaja jina moja ukitaja jina moja sema kwa jina ninaitwa sio kwa majina ninaitwa.
Nimemaliza mjirekebishe.