Sio kosa langu #10

samnas

Member
Oct 11, 2015
35
1
Fikra za kuwatafuta wazazi wake ziliyeyuka kabisa na kujikuta akipenda kitendo ambacho anakifanya na bi zuwena. Miezi miwili tangu waanze kufanya tendo hilo na wamekua mithli ya mke na mume. Mzee Ochu kwa kipindi kirefu hakuonekana nyumbani hapo tangu asafiri na kuelekea Tanga kikazi. Baada ya hashir kumaliza kazi zake zote siku hyo hawakuingiliana kama ilivyo ada, walipumzika na kuongea mambo mbali mbali kitandani hapo. Wakiwa chumbani hashir aliiona albamu ya picha iliyokuwepo mezani chumbani humo, kwa muda mrefu aliiona hyo albamu na kuvutiwa nayo. Hakusita kumuomba bi zuwena na kuanza kuiangalia, zilikua ni picha za harusi ya mzee uchu na picha nyengine nyingi.
Kwa uchovu aliokua nao siku hyo aliomba aondoke tu nyumbani akapumzike. Bi zai hakumkatalia ombi hilo,na punde tu hashir alijitayarisha na kuondoka zake huku akiwa na albamu mkononi.
Akiwa ndani ya gari aliperuzi zile picha na mwisho aliifunga na kumfikiria jasmin kipenzi chake.
Punde tu aliwasili kwao na kujitupa kwenye mkeka alipokua amekaa bibi yake, alimsalimu na kujilaza pembeni yake akiwa mchovu.
''Mjukuu wangu mbona mapema leo? Bosi hayupp nini?''
''Hapana bibi hakukuwa na kazi nyingi leo,nlipomaliza nliomba nije nipumzike''
''Ooh sawa,naona umeniletea na albamu kabisa leo, em lete tuione..'' (hashir aliichukua albamu na kumpatia bibi yake)
Akiwa anaperuzi bibi huyo moyo ulimpiga PAA!! baada ya kuona kitu kilichomshtua sna moyo wake, hashir alishtuka sana alipomuona bibi yake katika hali hyo.
''Eh...vipi bibi yangu tena? Kuna nini.?..nini tatizo bibi yangu? ''
''Mjukuu wangu?? Umeipata wapi hii albamu? ..''aliuliza bi zai huku akiwa na wasiwasi wa hali ya juu..
'' kwa bosi wangu bibi,kwanini?'' Hashir hakuelewa nini kilimshtua bibi yake na kua na ham ya kutambua nini kilimsibu.
''Ndio huyu kwenye hii picha??'' Bi zai alimuonesha hashir picha ya zuwena aliekua amekaa na mumewe siku ya harusi.
Moyo ulimuenda mbio hashir na kujikuta akipoteza nguvu kidogo kidogo
''Ndio bibi...kwanini bibi yangu? ''
Aliinama bi zai na kulia kwa muda,alijitahidi hashir kum bembeleza bibi yake mpaka pale aliponyamaza na kumsubiri nini angelisema,kitu gani kilimliza bibi huyo ndiolo swali kubwa lililozunguka kichwa cha hashir wakati huo.
''Kweli binaadamu sio kama milima,....... mjukuu wangu huyu si bosi wako.........huyu ni mamaako mzazi....''
Aliishiwa nguvu hashir na kujikuta akiuliza kwa nguvu
'' whaaaaaaaaaaaat????'' Hakuweza kuamini kile alichokiskia hashir na kujikuta akianguka chini kama mzigo na kupoteza fahamu.

****************

Mtoto aliezaliwa na mke wa makamo wa rais mzee muro hakufanana kabisa na mzee muro hata kwa mbali wala mama yake, tendo hilo lilimfanya mzee muro ashangae sana, baada ya kuulizwa nini kilimshangaza,aliwadanganya kwa kuwaambia ameshangazwa na uzuri wa mtoto wake. Walifurahi wote waliokua chumbani humo na kumpongeza makamo wa rais kwa kupata mtoto wa kiume aliyemuita Rashid (chidy), taarifa zilienezwa mitandaoni na magazetini baada ya mke wa makamo wa raisi kujifungua mtoto wa kiume. Ilikua ni furaha ya kila mtu siku hiyo japo kwa upande wa makamu wa rais bado alikua na wasiwasi wa hali ya juu kuhisu huyo mtoto. Hakusita kumuuliza mke wake, ila karima nae alipingana na hilo swala, na kumwambia kua ni wasi wasi wake tu ila mtoto wake kabisa. Karima alitambua ipo siku mzee muro atautambua ukweli na hakujua nini kingefuata baada ya hapo.
Skendo za kua idrissa alilala na mke wa makamo wa rais zilisambaa na kuskika mitaani kabla hata ya mzee muro kupata uongozi aliokua nao wakati huo. Alipokuja kuletewa habari ndipo alipoingiwa na wasiwasi zaidi na kushauriwa na watu akapime damu DNA (Kiwango kidogo cha shirika) yeye na mtoto wake, karima alikataa ombi hilo kwa kujua moja kwa moja ukweli ungelifichuka na jina lake pia lingechafuka pia. Makamo wa raisi alimuona chidy kama kinyesi kwake na kupoteza mapenzi na kichanga huyo asiye na hatia. Ukweli uligundulika mara baada ya rais kutuma watu wamchukue mtoto wake na kumpeleka nae hospitali ili wapime damu. Baada ya kuona mambo yamekaa vibaya karima alimtumia ujumbe idrissa ahame haraka iwezekanavyo, ikiwezekana atokomee na apotee kwenye mji huo wa daressalam.
''What....yule mwanamkee mshenz sana......ok thanks doctor!!'' Mzee muro alimshukuru daktari ambae kwa muda huo alikua na mshangao na maswali yaliokosa majibu baada ya kumpa majibu ya DNA makamo wa raisi na mtoto wake kwamba si mtoto wake wa damu, damu hazilingani. Tayari alikua amechanganyikiwa na hakutaka aendeshwe na mtu siku hiyo, aliendesha gari kama mwendawazimu, haikuchukua muda mrefu tayari alishafika kwake. Aliingia ndani kwa hasira alizokua nazo alimtafuta mke wake alipo na kumpa kipigo mithli ya mnyama..
''We mpuuzi unanichukulia mi mjinga sana sio?? Shenz sana wewe mimi mtu na heshima zangu unataka uniharibie jina langu sio??'' Alimpiga makofi na kum bamiza ukutani. Karima alipoteza fahamu kwa muda mrefu, mzee muro aliwaamuru wafanyakaz wake wamtoe hapo jikoni na wampeleke stoo kwa adhabu zaidi. Aliapa kumuua idrissa na kumtafuta mpka ampate.

Maisha ya karima na mumewe mzee muro yalishatiwa dosari, vilio havikuisha ndani humo pamoja na matusi ya nguoni, damu zilitapakaa baada ya kipigo kikali alichopewa karima na vijakazi wa mzee muro, baada ya miaka miwili ndipo mzee muro aliongeza wake wawili,, fatmah na rukia. Familia nzima ilimchukia karima na kumuona kama nuksi katika familia hiyo.
Pepo la mauaji lilimjaa mzee muro na kuapa kummaliza idrissa kwa mikono yake miwili atakapompata..
Makamu wa raisi alitumia njama ya kumtumia mkewe ili ampate idrisa kirahisi zaidi. Karima aliamuliwa kumpigia simu idrissa na wakutane magomeni lodge (vyumba vya wageni)
. Idrissa bila kujua hili wala lile hakusita kumskiza karima na kufata kile alichokisema. Kutoka keko ilipo ofisi yake mpka hapo magomeni haikua karibu sana, tayari makamo wa rais alishawapanga watu wake usiku huo akiwemo na yeye. Ilikua ni majira ya saa 3 usiku, mzee muro akiwa katika chumba chengine ndani ya lodge hiyo wakimsubiri idrissa atokee. Idrissa alipokaribia na lodge alipatwa na wasi wasi moyoni na moyo wake ulimkataza asiende pahala hapo. Ila kwa tamaa aliyokua nayo ya kumuona karima alijikuta akiingia lodge na kwenda mpaka chumba alichoambiwa na karima.
''Chini ya ulinzi!! Mikono juu!!!.....shenz wewe kaa hapo hapo..
..
..
..
..je wajua nini kiliendelea??? Usikose kufuatilia riwaya hii ya kusisimua sehemu ya #11
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom