Sio Kosa la Vyombo vya Usalama,Polisi n.k. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sio Kosa la Vyombo vya Usalama,Polisi n.k.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by eedoh05, Jun 6, 2011.

 1. e

  eedoh05 JF-Expert Member

  #1
  Jun 6, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 633
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Watu wengi tumekuwa tukiwalaumu sana polisi na vyombo vya usalama kwa mambo wanayofanya. Mie naona sio kosa lao, maana hata wao hujuta wanapofanya mambo ambayo baadae jamii ya wastaarabu na dunia ya wapenda haki hulaani. Nadharia za wanafalsafa wa kale kama Plato na Socrates ndizo huwaathiri watu hawa(polisi,usalama,askari). Plato anasema kiakili na kiufahamu watu ni wa aina nne.

  (a) Wenye akili sana. Hawa ni wachache mno. Kazi yao ni uvumbuzi na ugunduzi.
  Hawa kitaaluma hufundishwa katika namna saba tofauti. Hukuuzwa viwango vyao vya kujiuliza kwa nini, na kwa vipi, halafu uwaje, pia hufundishwa kufikiri kimantiki.

  (b) Wenye akili za wastani. Kundi hili liko kwa maelfu. Hawa mara nyingi hujadili na kuzungumzia matukio. Huwa na hamu ya kujua kundi A linaibuka na mapya gani. ( watawala, wanasisa, wanasheria, walimu, madaktari, mainjinia,waandishi, manesi, wafanyabiashara)

  (c) Wenye akili za kawaida. Kundi hili ni kubwa liko kwa malaki. Mara nyingi kundi hili huzungumza na kujadili mambo ya watu wengine. (hawa hufundishwa kilimo, ufundi, ujenzi,udereva,useremala nk)

  (d) Wenye akili ndogo. Hawa ni wengi mno katika jamii. Kwa kuwa uelewa wao ni mdogo, Plato alipendekeza kundi hili lifundishwe kupigana,liunde vikosi vya ulinzi na usalama. Mitaala ya kuwafundisha hawa hulenga kuwaambukiza tabia. Sio kuelewa. Kama unavyoweza kuambukiza sumaku katika chuma cha kawaida.

  Mbinu ya kufundishia kundi hili ni ile ya Pavolov mrusi, aliyetoa nadharia yakuwafundisha wanyama tabia mbali mbali. Hawa hawajiulizi kwa nini, na kwa vipi, kisha itakuwaje, matokeo ya nifanyacho yakiwa tofauti nifanyeje/nitatatueje pasipo kuzua matatizo zaidi( No reasoning, no logical thinking) Kundi hili lipo tu kusikiliza, kutii na kutekeleza amri za wakuu hata kama zinamadhara kwa jamii na kwao binafsi.

  Mtu mwenye akili huwezi kufanya ya Nyamongo-Tarime,unauwa,unapora maiti na kuzitupa barabarani, kupiga mabomu ya machozi na maji ya kuwasha vibabu na vibibi vistaafu vya EAC, kupiga mabomu ya machozi vitoto vya shule ya msingi vilivyokuwa vinapinga dampo karibu na shule yao Mnazimmoja(1998)
   
 2. M

  Marytina JF-Expert Member

  #2
  Jun 6, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  well said
  Hata wanajeshi wana hili tatizo.

  Maofisa wa jeshi wastaafu hawatakiwi kabisa kupewa vyeo vya ukuu wa mkoa na mashirika manake wameishi na mazoba muda mrefu.
   
Loading...