Sio kila ombaomba anahitaji msaada- be careful

wajinga ndo waliwao, hii habari si ya kweli ni kama zile hadithi za zamani kuwa mama mjamzito haruhusiwi kula maini, mayai kwa sababu atajifungua mtoto mwenye Kipara,hiyo ilikuwa janja ya wezee,hivyo hiyo nayo ndo maneno ya wachungaji wetu wa leo kuhimiza matoleo na hii itakuwa ni pale ubungo kibo maana jamaa kwa jeuri ya pesa anpaki mchuma wake wa bei mbaya pale juu kila mtu auone,ili aweze kupata pesa lzm atunge mambo ya fanane na ukweli poleni sana waumini
 
MWANAMKE ambaye jina lake halikufahamika mara moja, amedaiwa kupotea kimiujizi kwenye gari lake baada ya kumsaidia ombaomba.

Baadaye mwanamke huyo anadaiwa kukutwa jana asubuhi ufukweni mwa Bahari ya Hindi akiwa uchi wa mnyama na hawezi kuzungumza.

Askari wa Usalama barabarani waliozungumza na gazeti hili walithibitisha kuwepo kwa tukio hilo wakisema mwanamke huyo alikuwa akiendesha gari aina ya Rav4 akitokea mjini kuelekea Kinondoni.

Walifahamisha kuwa lilipofika kwenye taa za kuongozea magari katika makuano ya barabara ya Ali Hassan Mwinyi na Umoja wa Mataifa, alisimama na hakuondoka licha ya kuruhusiwa.

Walidai kuwa trafiki aliyekuwa akiongoza magari alimfuata mwanamke huyo na kumuuliza kuna matatizo gani, mwanamke huyo akaonyesha mkono wake uliokuwa umejaa nywele na kusema amepata shida hiyo mara baada ya kumpa fedha ombaomba aliyekuwa karibu na gari hilo.

Kwa mujibu wa habari hizo mwanamke huyo alipotea baada ya ombaomba huyo kumweleza kuwa kama anataka kurudi katika hali yake ya kawaida ambusu na akabubali, lakini mara baada ya kufanya hivyo wakatoweka wote.

Habari hizo zimeeleza kuwa kabla ya kutoweka kimiujiza, ombaomba huyo wa kiume alimfuata mwanamke huyo aliyekuwa akisubiri kuruhusiwa kupita kwenye taa kuongoza magari kwenye makutano hayo na kuomba msaada wa fedha.

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo alisema, mwanamke huyo alimpa Sh500 na mara baada ya ombaomba kupokea, mkono wake (mwanamke) ukaanza kuota nywele nyingi.

Kitendo hicho kilimfanya mwanamke huyo kushindwa kuondoa gari lake baada ya kuruhusiwa na askari aliyekuwa akiongoza magari eneo hilo.

“Baada ya askari huyo kuona gari hilo limeendelea kusimama

katikati ya barabara, alilisogelea na kumkuta mwanamke huyo akiwa ameduwaa kwenye usukani," alisema shuhuda mmoja wa tukio hilo na kuongeza:

"Ndipo trafiki alipomuuliza umepatwa na tatizo gani na mwanamke huyo akasema, baada ya kumpa huyu kaka (ombaomba) Sh500, mkono wangu umekuwa hivi"

Taarifa zimeeleza kuwa baada ya mwanamke huyo kutoa kauli hiyo, ombaomba huyo ambaye kwa wakati huo alikuwa amesimama pembeni mwa gari, alimtaka ashuke kwenye gari na kumbusu kama anataka kuondokana na nywele hizo.

"Kusikia hivyo, trafiki alimwomba mwanamke huyo ashuke na afanye kama alivyoelezwa lakini, alipombusu tu, wote wawili wakapotea," shuhuda huyo alisema.

Imeelezwa kuwa baada ya tukio hilo askari huyo alitimua mbio kuelekea kituo cha polisi cha Selander Bridge kuomba msaada.

Hata hivyo ingawa polisi wa kituo hicho walifika eneo hilo hawakuliondoa gari hilo kwa kuogopa kuingia ndani.

Kutokana na woga waliokuwa nao askari, gari hilo lilikaa hadi jioni na lilizimwa na mmoja wa ndugu zake mwanamke huyo, waliofika katika eneo hilo majira ya saa 12 jioni.

Habari zilisema baada ya ndugu zake kufika walikubaliana kwenda Kanisani na Msikitini kwa ajili ya kuomba na leo asubuhi mwanamke huyo alikuwa ufukweni akiwa uchi.

Hata hivyo Kamanda wa polisi mkoa wa Ilala, Faustine Shirogile alikanusha kuwepo kwa tukio hilo na kusema ni la uvumi.

"Hadi muda huu ninapoongea na wewe hakuna mtu yeyote aliyeripoti polisi kuhusu tukio hilo. Huo ni uvumi na tayari umekwisha enea sehemu mbalimbali hata katika tovuti na internet pia," alisema Shirogile.
 
kama ameshapatikana uchi basi atakuwa anajulikana... hizi hekaya nazo, dah!!

naona kwa wikimbili sasa clouds wanaandamisha kweli mambo ya nguvu za giza kwenye karibu kila kipindi sijui ndio theme yao mwaka huuu au vipi?
 
Wamtegemeao mwanadamu wamelaaniwa, ole wao!
 
Habari nzima haina hata jina la chanzo cha mtoa habari hata mmoja? Huyo mwanamke hana jina? Hao askari walothibitisha tukio hawana majina? Jina pekee tunaloliona kwenye taarifa ni la kamanda anayekataa kuwepo kwa hili tukio!

Bongo tambarare bin shaghalabaghala.
 
Bonge wa Clouds FM alikuwa hapo salender asubuhi hii, hakuna chochote - ni jamaa tu hana kazi akaamua kutunga story yake.

Na kwa kuwa wabongo tunapenda story za uvumi na ushambenga basi mji mzima umekuwa gumzo hilo hilo, badala ya kufikiria vitu vya maana -
 
Hata hivyo Kamanda wa polisi mkoa wa Ilala, Faustine Shirogile alikanusha kuwepo kwa tukio hilo na kusema ni la uvumi.

Hadi muda huu ninapoongea na wewe hakuna mtu yeyote aliyeripoti polisi kuhusu tukio hilo. Huo ni uvumi na tayari umekwisha enea sehemu mbalimbali hata katika tovuti na internet pia, alisema Shirogile.

WABONGO KWA LONGO LONGO HATUJAMBO
 
Ni njia PEKEE - baada ya nyinginezo kushindika - ya kuwaondoa OMBAOMBA mitaaa ya Jiji ya Dar es Salaam!

BTW: Leo mishare ya 6:45am nimepita karibu na Oystebay Police (upande wa USA Embassy) nimekuta mtu mzima kaaguka na nadhani hana fahamu - yupo NUSU uchi - yawezekana ndiye huyo alipotea ki-miujiza!
 
Mmmh hii kali.,na imekatishiwa patamu kweli, sasa walivyopotea walienda wapi?.,kwa kuwa ni ngumu sana kumtofautisha genuine ombaomba na huyo mzee wa busara nimeazimia kuanzia sasa sitoi tena senti zangu kwa ombaomba kudadadeki.

Kuna thread kule imeanzishwa imeeleza eti kakutwa ufukweni mwa bahari akiwa uchi na hawezi kuongea! Kama ndoto vile ni mtunzi gani huyu
 
kama kuna gazeti nilikuwa naliheshimu kwa habari za ukweli na uhakika zilizofanyiwa utafiti wa kina na wa hali ya juu ni mwananchi. lakini cha ajabu na wao wameingia mkenge na kuiandika hii habari yenye utata mwingi (ipo kizushi zushi zaidi ya ukweli) katika gazeti la leo.
 
Ni njia PEKEE - baada ya nyinginezo kushindika - ya kuwaondoa OMBAOMBA mitaaa ya Jiji ya Dar es Salaam!

BTW: Leo mishare ya 6:45am nimepita karibu na Oystebay Police (upande wa USA Embassy) nimekuta mtu mzima kaaguka na nadhani hana fahamu - yupo NUSU uchi - yawezekana ndiye huyo alipotea ki-miujiza!

Ulivyomcheki ki fasta fast - ni mwanamke au mwanaume?
 
Natumaini kwa uwezo wa Mungu mko wazima,

Leo kwenye misa ya asubuhi kanisani Azania Front mchungaji aliyekuwa anahubiri katufunulia siri nyingi sana za sheteni nakutupa shuhuda mbalimbali jinsi shetani anavyofanya kazi.

Moja ya ushuhuda wake ni kisa kilichotokea hivi karibuni hapa Dar es salaam. Napenda nikushirikishe ili uchukue hatua.

Pale salender Bridge ambapo anasimama trafiki akivuta magari, kuna mdada alikuwa ndani ya gari lake kwenye foleni akisubiri zamu yake ya kuruhusiwa na trafiki ifike apite. ndipo aliposogea kaka mmoja ombaomba, akasogea kwenye gari la yule dada na kuomba msaada.

Biblia inasema maskini wapo na wataendelea kuwepo, mwombe Mungu kwanza kila unapotaka kutoa sadaka yako. Mwenye Masikio na Asikie

Yes, sio habari zote utazipata polisi. Ukienda kule wakakwambia hakukutokea kitu. Hayo yapo. Nawajua ndugu zangu wawilin waliokuwa wachakarikaji sana hapa mjini, walipotoa misaada kwa ombaomba tu wakaishiwa kila kitu hata hawawei tena kupata maendeleo hata pesa haipatikani na ikipatikana hawajui inapotelea wapi. Walikwenda kila mmoja wao kwa waganga wa jadi wakaambiwa kila mmoja wao nguvu za kipato ilionekana kuondoka na kwenda kwa ombaomba mmoja ambaye hakutajwa.

Mie napata shida kumpa mtu msaada kwa sababu hiyo, hata kama mtu huyo anakusudia kweli kupata msaada, sio rahisi kujua. Kama filamu ya Yombayomba, ambapo alikuwa anapiga watu viboko akiwalazimisha wamsaidie yeye masikini kwenye mitaa ya DSM katika filamu ya Fimbo ya Mnyonge.
 
An urban legend, urban myth, urban tale, or, more accurately, a contemporary legend, is a form of modern folklore consisting of apocryphal stories that those who tell them believe to be true. Like all folklore, contemporary legends are not necessarily false, but they are often distorted, exaggerated, or sensationalized over time.
Despite its name, a typical urban legend does not usually originate in an urban area. Rather, the term is used to differentiate modern legend from traditional folklore in preindustrial times. For this reason, sociologists and folklorists prefer the term contemporary legend.
Urban legends are sometimes repeated in news stories and, in recent years, distributed by e-mail. People frequently allege that such tales happened to a "friend of a friend"; so often, in fact, that "friend of a friend," ("FOAF") has become a commonly used term when recounting this type of story.
Some urban legends have passed through the years with only minor changes to suit regional variations. One example is the story of a woman killed by spiders nesting in her elaborate hairdo. More recent legends tend to reflect modern circumstances, like the story of people ambushed, anesthetized, and waking up minus one kidney, which was surgically removed for transplantation (a story which folklorists refer to as "The Kidney Heist".)

Source: [ame]http://en.wikipedia.org/wiki/Urban_legend[/ame]
 
Sitashangaa kama hii habari ya kusadikika umesikia kwa Pastor Hammer pale ubungo kwa ufufuo wa misukule.
Habari ilitoka kanisa la Azania Front Lutheran Church kwenye misa ya asubuhi Jumanne tar 16 ikimaanisha kisa kimetokea Jumatatu tar 15 Feb juoni wakati huyo mdada anatoka town akiwa na Rav 4.

According to Mpasha habari wa mwananchi ya leo (uk wa 3) huyo dada alionekana ufukweni jana asubuhi akiwa uchi wa mnyama!
 
Mbura wewe ni mganga wa kienyeji au jadi? Manake nasikia sikui hizi eti mnatofautisha hao watu. Na swali lingine nauliza kwa wote huyu dada kapotea au kafa?

Mimi siyo mganga wa kienyeji ila nayajua malango ya kuzimu yote saba ya Tanznia na majini yake Kimsingi mimi ni mtumishi wa Mungu, elimu hii inanisaidia wakati nawaombea wagonjwa. Najua shetani ndiyo adui yetu kwa hiyo lazima tuzijue mbinu anazotumia ili kumshinda kirahisi.
 
Malango saba ya kuzimu yalifungwa rasmi kwa moto mwezi uliopita, mashimoni walikuwepo maelfu ya watu walioenda huko kutafuta msaada wa kichawi kwa mungu wa dunia.

Maelfu ya majini ya kuzimu yalikuwa duniani yakifanya uchawi na yameshindwa kurudi baada ya malango yao kufungwa kwa moto.

Kisa cha huyu dada ni moja ya matokeo yasiyo ya kawaida ambayo yatatikisa Tanzania kuanzia sasa, huyu dada uwezekano wa kurudishwa upo.

Kwa sasa yapo magari mazuri sana kutoka kuzimu yanatembea barabarani, yakiendeshwa na majini, usikubali kutoa lift au kupewa lift kabisa kwa mtu usiyemjua.

Malango saba ya kuzimu yaliyofungwa ni haya:

1. Lango la kuzimu la salender bridge - Dar es Salaam, lipo kati ya daraja la salender na bomba la maji machafu, karibu na hospitali ya Ocean road. Mlinzi wa lango hili alikuwa akiitwa Mustara akisaidiwa na majini 12.

2. Lango la kuzimu la Tabora mjini. Lipo karibu na soko kuu la Tabora mjini. Mlinzi wa lango hili alikuwa akiitwa Swahirani akisaidiwa na majini 12.

3.Lango la kuzimu la Tanga, Pangani. Mlinzi wa lango hili aliitwa Rajuni akisaidiwa na majini 12.

4. Lango la kuzimu la Bagamoyo, lipo baharini. Mlinzi wa lango hili aliitwa Zazuni, akisaidiwa na majini 12.

5. Lango la kuzimu la Mwanza. Mlinzi wake aliitwa Gharik akisaidiwa na majini 12

6.Lango la kuzimu la Kigoma, lipo Kibirizi. Mlinzi wake aliitwa Jarafu akisaidiwa na majini 12.

7. Lango la kuzimu la Iringa, Njombe, lipo eneo la Igosi. Mlinzi wake aliitwa Twafifin, akisaidiwa na majini 12

Malango yote haya yamefungwa kabisa, wale wote waliokuwa ndani ya mashimo haya ya kuzimu wakitafuta uchawi wataendelea kubakia huko.

Mizimu iliyokuwa duniani yakakuta malango yamefungwa wameshindwa kuingia, na wana ghadhabu kubwa, lakini vyovyote iwavyo, moto wa Mungu unawawakia.
 
Good! Asante .....Songa mbele kijana, walifikiria mimi ni mganga baada ya kuweka mambo ya malango ya kuzima
 
Back
Top Bottom