Sio kila ombaomba anahitaji msaada- be careful

Malango saba ya kuzimu yalifungwa rasmi kwa moto mwezi uliopita, mashimoni walikuwepo maelfu ya watu walioenda huko kutafuta msaada wa kichawi kwa mungu wa dunia.

Maelfu ya majini ya kuzimu yalikuwa duniani yakifanya uchawi na yameshindwa kurudi baada ya malango yao kufungwa kwa moto.

Kisa cha huyu dada ni moja ya matokeo yasiyo ya kawaida ambayo yatatikisa Tanzania kuanzia sasa, huyu dada uwezekano wa kurudishwa upo.

Kwa sasa yapo magari mazuri sana kutoka kuzimu yanatembea barabarani, yakiendeshwa na majini, usikubali kutoa lift au kupewa lift kabisa kwa mtu usiyemjua.

Malango saba ya kuzimu yaliyofungwa ni haya:

1. Lango la kuzimu la salender bridge - Dar es Salaam, lipo kati ya daraja la salender na bomba la maji machafu, karibu na hospitali ya Ocean road. Mlinzi wa lango hili alikuwa akiitwa Mustara akisaidiwa na majini 12.

2. Lango la kuzimu la Tabora mjini. Lipo karibu na soko kuu la Tabora mjini. Mlinzi wa lango hili alikuwa akiitwa Swahirani akisaidiwa na majini 12.

3.Lango la kuzimu la Tanga, Pangani. Mlinzi wa lango hili aliitwa Rajuni akisaidiwa na majini 12.

4. Lango la kuzimu la Bagamoyo, lipo baharini. Mlinzi wa lango hili aliitwa Zazuni, akisaidiwa na majini 12.

5. Lango la kuzimu la Mwanza. Mlinzi wake aliitwa Gharik akisaidiwa na majini 12

6.Lango la kuzimu la Kigoma, lipo Kibirizi. Mlinzi wake aliitwa Jarafu akisaidiwa na majini 12.

7. Lango la kuzimu la Iringa, Njombe, lipo eneo la Igosi. Mlinzi wake aliitwa Twafifin, akisaidiwa na majini 12

Malango yote haya yamefungwa kabisa, wale wote waliokuwa ndani ya mashimo haya ya kuzimu wakitafuta uchawi wataendelea kubakia huko.

Mizimu iliyokuwa duniani yakakuta malango yamefungwa wameshindwa kuingia, na wana ghadhabu kubwa, lakini vyovyote iwavyo, moto wa Mungu unawawakia.

Sasa huo ni utabiriiiii au?
 
Hii habari kanisa la azania front inabidi watoe ukweli kama ilikuwa story tu au ni ukweli imetokea.
 
MchajiKobe mh kachaji hayo mawazo upya bana, hii nilianza kuisoma kwa michuzi jana nadahni imekuja kama ilivyo huku. Haya mambo so mchezo. au ni ajenda za kuwabania riziki hawa omba omba?
Sasa we unahisi ridhiki ya mchungaji na ombaomba zote zatoka wapi kama si kwa waumini?So hapa mchungaji kaona ugali wake umepungua thats y kaamua kuwaharibia ombaomba!!
 
Dr Mbura, haya malango ni sharti yawe saba tu? Manake kuna sehemu nyingi zenye vioja na ajali za ajabu ajabu hazijatajwa. Kama pale daraja la Mto Kikafu barabara ya Arusha- Moshi. Pia Same, Uchira nk

Kuna kuzimu na vijiji vya kichawi, vijiji vya kichawi vipo vingi sana, kwa mfano katika jiji la DSM kijiji kikubwa cha wachawi kipo Pugu, inakisiwa ndani ya kijiji hiki wapo watu wasiopungua 30,000 na vimetapakaa sehemu nyingi sana nchini.

Mfano wa kikiji cha namna hii kinaitwa Gambushi kipo shinyanga, kijiji hiki mchana ni pori tupu usiku ni mji wenye magari, watu, maduka na shughuli mbalimbali.

Malango ya kuzimu yalikuwepo saba tu nchini Tanzania, kwa sasa tunashughulikia lango la kuzimu la Mombasa nchini Kenya.
 
Polisi wa kituo cha Selander wameshakanusha hii kitu kutokea. Labda kama kuna Selander nyingine!
Mara nyingi habari kama hizi zisizoweza kuthibitika kitaalamu...polisi huwa wanazitolea nje. Sababu kubwa ni kuepuka kuwatia hofu wananchi.
 
Mara nyingi habari kama hizi zisizoweza kuthibitika kitaalamu...polisi huwa wanazitolea nje. Sababu kubwa ni kuepuka kuwatia hofu wananchi.

Nakubaliana na wewe. Lakini tukiacha hilo la mtu kuota manyoya ya paka na kupotea, ishu ya gari kuachwa barabarani karibu na kituo cha polisi nadhani linathibitika kitaalamu! Tungeoneshwa angalau gari lililotelekezwa.

Inashangaza watu hawahawa wanaoamini hizi hadithi nao huwa wanamponda Sheikh Yahya na 'maprofesa' wengineo!
 
Back
Top Bottom