mwengeso
JF-Expert Member
- Nov 27, 2014
- 9,219
- 6,650
Bila kumung'unya maneno wanaodai Katiba mpya ni viongozi wa upinzani wakidhani mabadiliko katika Katiba yatawapa mwanya wa kushika madaraka ya Dola au angalau kugawana hiyo keki ya utawala, na Chama Dola.hakuna kitu pasipo sababu.. unafikiri wanaolilia katiba mpya hawajaona mapungufu yake..?
wanaodai katiba mpya waendelee kudai na wasiodai waendelee kutokudai
Kwa maisha ya kila siku ya Mtanzania, Katiba iliyopo inampa kila mtu haki na uhuru katika nchi yake. Katiba ya sasa, Sehemu ya Tatu: Haki na Wajibu Muhimu, imeboreshwa kidogo sana kwenye Katiba Inayopendekezwa: Sura Ya Tano: Haki za Binadamu, Wajibu wa Raia, Jamii na Mamlaka ya Nchi. Tofauti hiyo kwa Katiba ya sasa haimnyimi Mtanzania Uhiru na Haki stahiki.