Sintosahau nilivyoachwa park station

Sintosahau nilivyoachwa park station

singsang

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2017
Posts
435
Reaction score
644
Ilikuwa tarehe 25 mwezi wa 5 mwaka 2012 safari yangu ya kwanza kwenda South Africa, nikiambatana na dadaangu ni Mdogo kwangu tukielekea kwa madiba, tena ikiwa yeye dadaangu ndo mwenyweji wangu uko tuendako, japo yeye pia hajawahi kufika.

Lakini mchongo kaitwa na shemeji yangu ambae mimi, simjiu, lkn kwa maelezo ya dada yeye shemeji ananijua, na hata kwangu napoishi na Mdogo wangu alikuwa anakuja akiwa bongo na hata mke wangu anamjua, japo mimi na huyo mtu hatukuwahi kufahamiana.

Turudi nyuma kidogo, kwa kipindi hicho kabla ya safari, mimi nilikuwa nna ofisi ya ufundi wa simu mtaa wa Agrey Kariakoo na huyo dadaangu ndo nilimfanya mtu wa mapokezi, ofisini.

Siku moja ndio ananambia Kaka kuna shemeji yako anaishi South Africa ananiita niende, nikamuuliza unamjua vizuri, akaniambia sana mbona hata wifi anamjua (ambae ni mke wangu), kwamba akiwa bongo anakujaga home ki wizi.

Nikamwambia kwa kuwa yeye nimtu mzima Ana maamuzi yake, anavoona yeye kama inafaa aende tu maisha popote, basi jamaa akamtumia pesa ya passport na mambo mengine.

Wiki moja kabla ya safari dada akaniambia kaka sema kule nasikia kazi za ufundi simu zinalipa vizuri sana, nikamjibu nasikia pia, akaniambia ngoja niongee na jamaa kama vipi twende wrote.

Itaendelea.......
 
SEHEMU YA PILI
Basi kwa kuwa mimi nilikuwa nna passport yangu toka mwaka2010 sikuwa na shida sana, kesho yake dada ananambia kaka kama uko tayari jipange mi nshamaliza kila kitu, mzee wa kazi nikaona ngoja nibadili upepo huenda mambo huko Dzonga yakanyooka.

Basi mishe ya safari ikaanza, kumbuka nna familia mke na watoto wawili, basi nikafanya mambo yangu, nakaacha mzigo wa kutosha angalau miezi mitatu, pesa yakula na matumizi kwa familia yangu, siku ya safari ikawadia, bwana bwana, safari usilolijua........
 
TWENDE
safari yetu tulisafiri salama kabisa, lkn kwa mimi kichwani sikuwa na amani, nilikuwa nahisi kuna vitu vitanitokea ambayo sio vizuri, lakini nikimuuliza sister ananambia nisiwe na wasi wasi kashampanga jamaa na jamaa anajua kwamba tunakwenda wote.

Tuliingia joz kama saa nane au tisa mchana, dada akampigia jamaa, baada ya muda kuna mtu akaja tulipo tukapanda kwenye parking za magari madogo ya watu binafsi wanaokuja kupokea wageni.

Picha linaanza, tulivyoonana for the first time jamaa kama alistuka flani hivi then dada akamtambulisha, huyu kaka yangu daah nikaona jamaa kamvuta pembeni dada, wakachukua kama dk kadhaa kama wanazozana hivi, nikaona apa kishanuka.

Kumbe jamaa haamini kama mimi ni kaka bwana, baadae kuna kijana sijui Mdogo wake, akaja pale waliponiacha akaniambia broh twende, dada nae akaniambia kaka baadae basi, basi nikaingia kwenye ndiga maana zilikuja gari mbili, moja anaendesha shemeji na ingine ndio tupo mimi na uyo dogo, vuuuu mpaka magetoni kipindi hicho ndio naingia Joz nashangaa tu mitaa mighorofa, mi free ways yaani hata sikujua nimefikaje hapo gheto.

wana sijakaa hata dakika tano yani hata viatu sijavua nawaambia oya usikae jamaa kasema turudi kule Park Station, nikaona eheeee mziki umeanza, basi nikainuka najua labda nimeitwa niende kupata msosi maana ndo tumeingia hatujala weee, naambiwa beba tu na ilo begi lako twende, basi tukafika Park Station, naona sister hayupo sawa, aniangalii usoni na wapo pale pale tulipowaacha.

Basi jamaa shemeji akaanza kunichukulia maelezo, huyu nani yako, nikamueleza, akaniambia una sehem ya kufikia nikamjibu no si nimekuja na sister na aliniambia ashakwambia ujio wangu, wee jamaa kauzu akaniambia sina taarifa ya kuja na wewe, pili ntaamini vipi kama wewe ni kaka yake, nikamwambia chukua passport zetu angalia majina, aaah wapi jamaa kakaza tena kauzu ananambia hapa mimi sina pa kukuweka.

Pili sikujui, na mwisho akamuita sister akamwambia chagua moja ubaki na kaka yako hapa mgeuze, au kaka yako ageuze, mimi nikaingilia kati nikamwambia yule jamaa, sikia we si umemuita sister aje, basi we niache nyie nendeni, sister akaanza kulia, nikambembeleza sister asijari mi mwanaume yeye aende na jamaa yake, apo mfukoni nna rand 200 nakumbuka ndio nilibaki nayo,.....
NARUDI
 
TUENDELEE

Basi kweli jamaa akaniita pembeni akaanza kunipa risala kumbe yule jamaa bwana ni mafia, kazi zake ni mchomoko, wizi wa simu yani ana kundi kabisa la vijana wezi yeye ndio boss wakiiba uko wanaleta kwake, kwa hiyo ni gangster fulani hivi, basi nikapigwa mikwala pale, ki ufupi jamaa hakuamini kama mimi ni kaka yake sister, alijua kwamba sister kaja na bwana ake, basi jamaa akaniambia hapa fanya mango rudi bongo tu, nikamwambia hela niluonayo ni ndogo haitoshi kufikia bongo akaniuliza una kiasi nikamtolea apo sijui thamani ya rand, akaniambia okay kutoka hapa mpaka Harare nauli r350 kipindi hicho, mimi nna r200 akaniongezea rand 200, akaniambia apo unga unga ulifika Harare ongea na mabasi ya TAQWA, utalipa ulifika bongo, daaaaaah, nilihisi naota, nikamwambia poa, basi wakasepa, kumbuka sijatia chochote toka tumeingia sijaoga siku 4, sijabadiri nguo, nipo hoi, basi nikashuka zangu tena chini tuluposhushwa na basi kutoka Harare, kuna viti vya kusubiria iyo inaenda saa 12 jioni, njaa inauma, nikaona hapa ngoja nile kwanza, nikaulizia wanapouza chakula cha mama ntilie, maana mule ndani kuna migahawa ile ya bei bei, mimi hela sina, kweli nikaonyeshwa, nikaagiza ubwa ubwa, na mboga zina rangi rangi za blue, bwana uo mchele duh sio mchele ni plastiki, nakumbuka tanzania pia kuna kipindi waliletaga mchele ule, basi huku ndo mchele wao, nilikula kwa kuwa nilikuwa nna njaa sana. Baada ya kushiba nikatafuta benchi moja liko tupu nikasema ngoja nilale kidogo, maana nipo hoi.
NTARUDI NA MNISAMEHE KWA UHANDISHI WANGU, MAANA JAMII FORUM KUNA WALIMU WA KISWAHILI WENGI SANA.
 
Ilikuwa tarehe 25 mwezi wa 5 mwaka 2012 safari yangu ya kwanza kwenda South Africa, nikiambatana na dadaangu ni Mdogo kwangu tukielekea kwa madiba, tena ikiwa yeye dadaangu ndo mwenyweji wangu uko tuendako, japo yeye pia hajawahi kufika. Lkn mchongo kaitwa na shemeji yangu ambae mimi, simjiu, lkn kwa maelezo ya dada yeye shemeji ananijua, na hata kwangu napoishi na Mdogo wangu alikuwa anakuja akiwa bongo na hata mke wangu anamjua, japo mimi na huyo mtu hatukuwahi kufahamiana,
Turudi nyuma kidogo, kwa kipindi hicho kabla ya safari, mimi nilikuwa nna ofisi ya ufundi wa simu mtaa wa agrey kariakoo na huyo dadaangu ndo nilimfanya mtu wa mapokezi, ofisini,
Siku moja ndio ananambia Kaka kuna shemeji yako anaishi South Africa ananiita niende, nikamuuliza unamjua vzr, akaniambia sana mbona hata wifi anamjua, (ambae ni mke wangu) kwamba akiwa bongo anakujaga home ki wizi, nikamwambia kwa kuwa yeye nimtu mzima Ana maamuzi yake, anavoona yeye kama inafaa aende tu maisha popote, basi jamaa akamtumia pesa ya passport na mambo mengine, wiki moja kabla ya safari dada akaniambia kaka sema kule nasikia kazi za ufundi simu zinalipa vizuri sana, nikamjibu nasikia pia, akaniambia ngoja niongee na jamaa kama vipi twende wrote,.
Itaendelea.......

Kabla ya kuendelea jifunze kuandika vizuri

Weka paragraph, sasa unabananisha kama Una upungufu wa makaratasi?
 
Back
Top Bottom